Dr Slaa na Tanzania yenye neema... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa na Tanzania yenye neema...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eiyer, May 9, 2011.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Wakati anaamua kuachana na kazi ya kiroho,hakuiacha kwa kashfa mbaya,bali aliamua kufanya shughuli nyingine ya kuisaidia jamii,alipoingia kwenye siasa akagundua mambo hayaendi sawa,yeye kama Mtanzania na binadam amechukua jukumu la kuimbia jamii uovu unaotendeka,amewataja wanaoidhulumu jamii kwa majina,bahati mbaya hawajachukuliwa hatua zozote coz wanaotakiwa kushtakiwa ndo haohao washitaki,wamedai wamechafuliwa,wameshindwa kujisafisha bado wapo madarakani wanaendelea kuivuruga nchi,maisha ya Watanzania hayana mbele wala nyuma,asilimia 85 ya watanzania wanaishi bila umeme na kwenye nyumba za matope,Dr Slaa akawaambia hawa wanyonge kwenye kampeni za uchaguzi kuwa atawashushia gharama za ujenzi ili wanyonge hawa watoke kwenye matope,wezi wa haki za wanyonge wakamwambia anachofanya ni ndoto ya mchana,akawaeleza namna atakavyopunguza gharama hizo na pia atafanya elimu bure kutoka darasa la kwanza mpaka form 6 wakakosa hoja,wakadai ameiba mke wa mtu walipoona hoja hiyo haina mashiko wakamuibia kura akawaambia wazi wahusika,wameingia madarakani wamepandisha zaidi gharama za maisha,Dk Slaa amewaambia watanzania wasikubali kwa maandamano wamemuita mtu hatari kwa taifa,15% ya Watanzania ndo wana umeme,hata hao wachache wameshindwa kuwapa huo umeme,unakuwa wa mgao kila siku ili wauze magenereta yao,huduma za jamii wamezifanya kuwa za wenye hela yaani anasa,ukitaka kuwa na umeme,matibabu mazuri,maji safi ya kunywa,usafiri wa uhakika,shule nzuri n.k ni lazima uwe kwenye"sistimu"hii chafu au uwe mwizi wakukamate wajisifu wamekamata jambazi wakati na wao ni majambazi wakubwa,jamani nasikia kizunguzungu hivi nisaidieni
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Umenena vyema kwan ipo siku tutakombole toka haya magamba_dalil zimeanza kuonekana. Umesikia jk anasema uwongo ukisemwa sana watu huamin,bila kuutaja huo uwongo inalekea alikuwa ndotoni.Dr Slaa atadumu kunena yote waloyaficha watajulikana tu,kila kitu kitakuwa waz hata walifiche litajulikana tu.
   
 3. O

  Omr JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahaha, wewe lazima utakua umetumwa na kina Slaa. Unajua kwenye Siasa kuna ulaji mzuri kuliko kanisani?
   
 4. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mbona twadanganyana kama watoto. Mbona yajulikana wazi kuwa Askofu wa nyumbani kwao alikataa kumpokea kwa sababu ya kashfa ktk ziara ya Pope miaka ya 90. Wadanganyeni watoto wa vyuoni na sekondari
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Hujui unachozungumza,pia huju kuwa kama angekuwa na tamaa ya hela angebaki kwenye dini ambako hela zina ukaguzi mdogo,lakini hebu jiulize kwa moyo wa ukweli kama yanayosemwa na slaa ni uongo hebu nenda hata sokoni kaseme Kikwete ni mwizi kama hatujakusahau,wanamwogopa Slaa coz ana ushahidi,lakini wewe unawapenda watanzania wanaoishi kwenye nyumba za matope bila umeme wakiwa na hofu ya kupata maradhi ya kuambukiza kutokana na ufukara unaotokana mfumo mbovu wa uongozi?
   
 6. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 643
  Trophy Points: 280
  nielezee kinagaubaga jinsi ambavyo elimu itakuwa bure mpaka form six.....tell me how,emperically!
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  wasalaam;
  mara baada ya salam mie mzima wa afya.


  napita tu jamani
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Elimu itakuwa bure kwa kutumia vizuri rasilimali Tulizonazo ambazo kwa sasa zinatumika ndivyo sivyo,ila jibu zuri waulize chama cha magamba kuhusu kuifanya elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi form 4,waliamua kuwaambia Watanzania hivyo baada ya kumshkia Slaa na sera ya elimu bure,sijui kama watafanya hivyo maana hawa ni waongo sana
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Siku zote palipo na ukweli uongo hujitenga na ndiyo maana uongo wa ccm wa zaidi ya miaka 40 unazidi kujitenga na ukweli unaofunuliwa na chadema unazidi kusambaa na kukubalika na watz wote
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Elimu itakuwa bure kwa kutumia vizuri rasilimali Tulizonazo ambazo kwa sasa zinatumika ndivyo sivyo,ila jibu zuri waulize chama cha magamba kuhusu kuifanya elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi form 4,waliamua kuwaambia Watanzania hivyo baada ya kumshkia Slaa na sera ya elimu bure,sijui kama watafanya hivyo maana hawa ni waongo sana
   
 11. O

  Omr JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo lenu nyie ni wepesi wa kudanganyika, ccm wamewadanganya kwa miaka 40 sasa hawa CDM wamekuja na staili yao, mwisho wake ni uongo uleule kwa njia ofauti.Elimu ya bure nyie mnaijua?
  Sisi tunataka waache kelele za mikutanoni na wakawajibike bungeni, tatizo la CDM wanataka wao wakiongea washabikiwe sasa huko bungeni inakua ngumu na ndio maana hawaishi kuzira.
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe Omr ni nabii mpaka uweze kujua mambo ya mbele?Unaitabiria chadema kuwa haitakuwa tofauti na ccm,nani amekuonesha hiyo future?Pia inamaana huoni kazi ya wabumge wa chadema bungeni japokuwa ni wachache?Acha mambo ya ajabu
   
 13. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #13
  May 9, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bila shaka wewe ni mmoja wa wanachama wa chama chenye Magamba...
  Waliambiwa kodi ya kichwa ifutwe wakasema, serkali itapata wapi mapato...
  Leo hii hakuna kodi ya kchwa na serikali bado ina mapato.....
  Wakaambiwa elimu ya msingi iwe bure wakasema haiwezekani...
  Leo hii elimu ya msingi ni bure na mambo megine yanaenda.....
  Kama hayo yaliwezekana bila kupunguza gharama serikalini,
  Basi hilo la Elimu bure mpaka kidato cha 6, bila shaka linawezekana!?
   
 14. J Rated

  J Rated JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  We upo tz ya wapi mbona elimu bure kwa sekondari halmashauri ya moshi inayoongozwa na cdm wameshaanza kulitekeleza hili mkuu...amka na uchukue hatua,ccm wameshaturudisha nyuma vya kutosha
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Bora uwaambie maana kuna watu wana akili na kumbukumbu kama samaki!
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  May 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  May 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Mimi nimetoka Mbulu, acha kuwadanganya watanzania. Dr Slaa hana kashfa yo yote kanisani.[/QUOTE]

  Nakushuktru ndugu ukweli uko wazi,angekuwa na kashfa wangeitumia kumchafua
   
 18. M

  Mabula Member

  #18
  May 9, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  hivi hili suala la kuamua kumlipa dr slaa mshaahara na marupurupu ya mbunge kwamba hakuamua yeye kwenda kugombea urais isipokuwa aliombwa maana yake nini?linatoa mwelekeo gani kwa chama,?na hili suala la ununuzi wa fuso kwa milioni mia nnee nalo limekaaje? huu siyo ufisadi mwingine tena wa ovyo zaidi kwa vile unaharalishwa kupitia katika vikao. hawa ni viongozi maslahi au tueleweje? kuna msemo unasema nyani haangalii kundule.watu wanacheza ngoma wasiyo ijua.kumbe dr hakuwa na dhamira ya kugombea urais kwa vile alijua akikosa maslahi yake ya ubunge angepoteza hivyo ikabidi apewe ahadi ya fidia! chaga development manifesto! pesa kwanza. inasikitisha ,inakinaisha,inaudhi nakuchefua! vyama hivi si sijui twende wapi? chama cha mabadiliko hakijazaliwa kwa mwendo huu. kila mtu akilipwa fidia za kisiasa mbona chama kita collapse! ikaragabao
   
 19. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nampongeza mwandishi wa thread hii,mwenye macho haambiwi tizama.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kura za Slaa hazitatosha hadi cdm wamuweka mtu neutral asiyefuata maagizo kutoka vatican period...si kila mtu ni mjinga
   
Loading...