Dr Slaa na Chadema sasa basi, inatosha!

Yani pamoja na matatizo yote tuliyonayo chini ya uongozi wa magamba bila kusahau potential wanayoionyesha CDM bado watu wanahitaji kuhamasishwa???Kweli waTanzania wameridhika......

Lizzy kipenzi...kuhamasishwa ni muhimu tofauti na unavyofikiria...wazee wengi hata kama hali ni ngumu huwa hawapendi mabadiliko, wengi wanachojali siku imeanza ,siku imeisha..na wengi wanafikiria nchi ikiongozwa na chama kingine tofauti na CCm basi patatokea vita kubwa na nyie mnaoishi daslama mtapanda ndege na kukimbilia huko mbali...mkiwaacha wazee wanakufa huku. Hii ndio theory iliyokuwepo kwa wakazi/wazee/vibibi wengi wa pande za kusini mtwara na lindi. Bila kuhamasishwa dizain hii ya watu, ule kalaghabao!!
 
^ wewe sema hao wazee hawana imani na hiki chama usilete hadithi ya vita. Ni vijana wenye mawazo ya kimaskini ndio washabiki.
 

Haya maneno akiyaona Msekwa na Nape watfurahi sana mpaka gego zitaonekana
 

Ndugu umeainisha vizuri sana,
Ila ukifikiri zaidi utagundua msingi wa yote hayo ni MFUMO WA UTAWALA!
Kitu ambacho kilifumwa na serikali za ccm toka mwanzo!
Si JK wala yeyote wa ccm kwa kutumia mfumo tulionao (walioufuma) atafanya chochote zaidi ya danganya toto!
Ila nakubaliana na wewe kwamba, kwasasa ni lazima harakati ziendelee kuelekea mfumo mpya wa maisha.
 

Hayo ni mawazo yako tu! Sioni spidi yoyote ya CDM zaid ya kupoteza muda wao na fedha za ruzuku
 

Mngejua hali ilivyo mbaya kwa CCM mbele ya wananchi ni balaa nini uhakika asilimia milion 10 kwamba CCM ndo mwisho na ndo mwanzo wa kuwashitaki hawa mafedhuli na mwisho wao ni uhamishoni au behind the bars ninaomba iyo siku ifike maana kila lona CCM haitakiwi
 
Yani pamoja na matatizo yote tuliyonayo chini ya uongozi wa magamba bila kusahau potential wanayoionyesha CDM bado watu wanahitaji kuhamasishwa???Kweli waTanzania wameridhika......

Lizzy, waTz washahamasika, sasa Chadema watumie vizuri hii opportunity kutap wanachama na wapiga kura!
Si unajua mapenzi yanaponoga watu ndo hutangaza ndoa!
 

Mkuu umenena vyema, natumani Lizzy kaelewa somo! Nashukuru binafsi amehamasika!
 

kati ya mazumbukuku ndo wewe yani slaa akaimbe taarab na huyo mwenyekiti wa magamba taimba nini? Amefanya ikulu kama gheto anaingiza wasanii ikulu sijawahi ona hata UGANDA na ujinga wao hawako ivo
 

Nafurahi kina mama wamehamasika pia, Juzi juzi mama yangu mkubwa na rafiki yake walikua wanasema Yaani hawampendi Kikwete, kiasi kwamba akimuona anaongea kwenye TV anaizima!
 
Mimi nilikuwa mwanachama wa CCM lakini sasa nimebaki njiapanda, kwa uchungu wa nchi yangu inavyoangamia kwa uvivu na ufisadi lakini hasa hao waliokalia madaraka kutokuwa na nia ya kweli ya kuwakomboa kwa haraka Watanzania basi mimi nakubali Moto wa Dr. Slaa uendelee mpaka kieleweke, iwe kwa vyovyote ile, kwani mpaka sasa na utulivu wetu pamoja na shida je tuna faida gani? kama ni unyanyasaji wa polisi ni vitu vya kawaida, mabomu uzembe yalipuka kila siku? style ya kitunisia ya Maandamano mi naikubali, na nakiri mimi ni CCM, japo kwa sasa sijui, simlaumu JK peke yake, kwa uozo uko popote Tanzania, mimi ningeshauri kuokoa nchi Dr Slaa apewe ukuu wa serikali, yaani Waziri Mkuu, badala ya mkulima wa kulia lia akiona tatizo badala ya kutoa amri
 
Hayo ni mawazo yako tu! Sioni spidi yoyote ya CDM zaid ya kupoteza muda wao na fedha za ruzuku

Mkubwa you think so! Najua wangeweza fanya vizuri zaidi lakini kama huoni kitu una walakini!
 

Nakupongea kwa kuusemea moyo wako vyema. Miaka kadhaa iliyopita watu tulikua tukiipenda CCM unconditionally kumbee kumbeee tulikua hatuijui!

Slaa akichua uwaziri mkuu hapata noga! Aingie mjengoni kabisa pale magogono street!
 
Kinachofanya CDM na Dr. wasiache kupambana na ufisadi ni kutokana na watawala kuzoea kuishi kwa kutegemea hela za ufisadi kwa hiyo inakuwa vigumu kwao kuacha kukwapua rasilimali za taifa. Ninachopenda kuwaambia watanzania ni kwamba dawa ya ufisadi ni kubabadili mfumo wa utawala kwani utawala wa ccm hauwezi kusogeza taifa hili mbele hata ipate viongozi wa namna yoyote ile. Simnamuona JK tulimwamini mwaka 2005, pamoja na kuonesha utashi wa kubadili maisha ya watanzania amefanya nini? Mambo ya gamba ni uzushi mtupu na njia ya kuwaadaa watz. Ufisadi upo hadi kwa wafanyakazi nani atawakemea wakati na viongozi ni watuhumiwa WA UFISADI.
 
Sina kadi ya chama chochote lakini CDM wananikuna kichwa ile mbaya ,ila ilijukumu ni kubwa tusiwaachie baadhi ya watu kuliendesha tuungane wote ili tuweze kulifikisha hapo tunapotaka ,"if you don't want change,change will change you"
 
Tunajua wazi kuwa ukisema ukweli juu ya ubovu wa Slaa basi unaitwa mnafiki. Endeleeni kumtukuza na siku akiwaharia ndio mtajua kwamba yeye ni mwanasiasa na wala sio malaika kama mnavyo amini..

Naomba unatajie uzuri wa JK!
Sio uzuri wa sura na tabasamu
 
moto wa ukombozi huwa haupunguzwi. ukishaleta ukombozi moto huo hutumika kuleta maendeleo na taifa bora zaidi. hakuna kupunguza spidi bali inapaswa kuongezwa. wanaoshindwa kutawala wajitoe waje wawezao kutawala. nao wakishindwa wanatolewa. hawekwi mtu madarakani kwa personal liking yake bali kwa uwezo na upo wake wa kuongoza watu. kama hawezi hapewi nafasi ya uongozi. hiyo ndo kanuni ijayo
 
Mwacheni JK na watu wake wapate dozi, kwani nchi imewashinda.

Mfano; JK anasema kwenye sherehe za meimosi kuwa hawezi kukubali mtanzania kuwa mtumwa kwa mwajiri wake ndani ya nchi yake (yaani TZ), hivi kweli anajua anachokisema huyu mkuu wetu? Kuna viwanda vingapi vya wageni/wanyonyaji (wao wanawaita wawekezaji) mfanyakazi kibarua miaka nenda rudi, hakuna mkataba, hana medical insurance, mafao ya uzeeni na mwajiri anakufukuza siku yeyote akijisikia. Kuna kiwanda kimoja maeneo ya Vingunguti kibarua wa miaka rukuki alikufa kwa ajali akiwa kazini ikabidi mwajiri wake amwajiri siku ile baada ya kufa ili kukwepa taabu ya kisheria iliyokuwa mbele yake!

Mwacheni Dr. Slaa na Chadema wafanye kazi yao. CCM nchi imewashinda na hawana jipya leo, kesho wala keshokutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…