Revolutionary
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 456
- 86
Hali ya nchi imekua tete sana siku hizi. Dr Slaa na Chadema wameifumuafumua CCM na serikali yake, wamebaki wanahaha kutwa kuchwa kumtafuta mchawi ni nani wakati wamejoroga wenyewe! CCM nako wanajikanyaga kanyaga tu kujivua gamba hakuwezekani kwani gamba linang'oka na ngozi! Ukiachilia unyoka wa CCM kubaki palepale, sijaona gamba hata moja lililovuliwa, wembe wa CCM ni ule ule UFISADI!
Baada ya DR Slaa kuanza kufumua fumu fumu hadharani ufisadi wa CCM tangu alipokua bungeni na Chadema kuendeleza makali hayo kwa kasi na ari zaidi sasa uchafu wote wa serikali hadharani. Kila mwananchi anajua kila uchafu unaoendelea serikalini.
Kwa miaka kadhaa wananchi tulikua tunafichwa UFISADI wa serikali ya CCM, vigogo walijimegea nchi kwa ari ya ajabu kabisa!
Sasa wananchi tunaona na kuelewa Serikali yetu kwa namna inavyonuka hadi nasikia aibu! Rais baada ya kutajwa fisadi na ufisadi wake wa wazi nae anajikanyaga tu hana meno, hana guts za kumwadhibu yoyote kwa uchafu wake binafsi pia,magamba hayavuki basi tu! Kwa kujikomba komba kwa raia na watu anaishia kuwa msanii sanii na kutoa ahadi za kuclick, za uongo uongo hadi namuonea huruma huyu baba aliyewatoa wakwere kimasomaso, nchi inamshinda kwa kasi na ari ya Chadema ambayo imewashika na watanzania sasa inaivuruga vuruga serikali ya CCM hadi nahisi nchi inakwenda mrama sasa!
Nawaomba Dr Slaa na Chadema kuwa jamani eeh waungwana inatosha tosha sasa, have mercy on our president, kasi yenu inafanya taifa halitawaliki kweli, chama cha magamba kushnei!
Chadema naomba punguzeni spidi!
aagh mkuu...umeanza vizuri lakini swala la kusema wapunguze kasi,nalipinga,kwa CCm 1 mistake 7 goals, huu moto ndo ushaanza hivyo na unaendelea,hadi kukipambazuka ...2015 hiyooo!! Bado pande za kusini Mtwara na Lindi hawajaenda!!watu wana hamu kweli ya mabadiliko kule ,sema basi tu hakuna muhamasishaji...!!
Ni kweli dr Slaa kafichua ufisadi lakini nadhani siyo peke yake. Tofauti tu ni kwamba yeye alizua moto bungeni na kwenye mikutano ya hadhara. Ukisoma magazeti, ukinukuu thread nyingi hapa JF hasa za MM utakubali kwamba siyo dr Slaa peke yake. Wote wapewe sifa
Acha aisee Dr ni Dume la mbegu! Mtu mmoja kama CCM milioni moja!Dr slaa ni mwanaume...........
[/COLOR]
Mkuu nakubaliana nawe kabisa kwa yote; ila hapo kwenye nyekundu "sikubaliani nawe". Katika nchi za kiafrika ili tuendelee tunahitaji matumizi mazuri ya rasilimali za taifa. Na ili hili liwezekane, inabidi kukomesha ufisadi wa aina zote. Kukomesha ufisadi si jambo rahisi sana, ni mpaka wananchi waliowengi waamke (awareness) kujua namna viongozi wao wanavyowaibia na wawe na uwezo wa kujua namna ya kuwazuia wasiibe. Kwa msingi huo, elimu inayotolewa sasa na CDM inatakiwa iwafikie kila mtanzania hadi vijijini; na hapo ndo rasilimali za nchi hazitabakwa ki-urahisi na hivyo kutumika kwa maendeleo ya waliowengi-watanzania. Hivyo CDM ongezeni spidi kwenda hadi vijijini kuliko na watu wengi ambao hawajajua vema-na ambao hutumika kama mtaji wa watawala kuudanganya umma.
Ni kweli dr Slaa kafichua ufisadi lakini nadhani siyo peke yake. Tofauti tu ni kwamba yeye alizua moto bungeni na kwenye mikutano ya hadhara. Ukisoma magazeti, ukinukuu thread nyingi hapa JF hasa za MM utakubali kwamba siyo dr Slaa peke yake. Wote wapewe sifa
Mkuu kwa kweli hapo kusema wapunguze spidi ni kwamba namuonea tu huruma rais wetu! Sijawahi ona serikali iliyokosa mwelekeo kama hii!
Halafu Chadema wana potential kubwa sana ukiacha hulo kusini ambako hawajaenda huku mjini tu kuna watu wangependa kuwa wanachama hata leo lakini ndo kama hivyo muihamasishaji hakuna!
lakini hali haitakuwa nzuri kwa CDM kupiga kimya ila kwa serikali kuwajibika. JK bado anao muda na uwezo mkubwa wa kuwanyamazisha CDM na Dr. Slaa kwa kuyashughulikia yale ambayo yanawafanya cdm wazunguke na kuyadai, baadhi ya hayo mambo ni kama:-
Kuboresha hali za wafanyakazi kwa kupunguza kodi na kupandisha kima cha chini cha mishahara, kupunguza ugumu wa maisha kwa kupunguza kodi nyingi ktk bidhaa muhimu kama mafuta.
Kupunguza matumizi ya anasa ya serikali ikiwa pamoja na mishahara mikbwa na marupurupu ya viongozi kama wabunge kuwepo na uwiano kati ya mishahara na kiwango cha elimu na unyeti wa kazi yenyewe.
Kuheshimu na kufata utawala wa sheria watu wahukumiwe ktk muda muafaka maamuzi ya siasa yasibind maamuzi ya mahakama.
Kusimamia maadili ya viongozi kwa ukaribu na athubutu kuwaadhibu na kuwafikisha mahakamani wtuhumiwa wakuu wa ufisadi ikibidi kuwafunga hata kama ni marafiki zake.
Kupitia upya mikataba yoote ya rasilimali za taifa na iandikwe kwa manufaa ya wananchi, pamoja na transparency ktk uendeshaji wa nchi, kupunguza ukubwa wa serikali.
Hayo ni baadhi tu ila kuna mambo mengi mengi ambayo CDM na watz wengi yanawaboa akiweza kubadilisha mbona cdm watacease coz watakuwa hawana la kuishtaki ccm kwa wananchi otherwise this movement is unstopable yaani hata Cdm na Dr wakinyamaza kwa hali ya sasa hata mawe yatapiga kelele
Yani pamoja na matatizo yote tuliyonayo chini ya uongozi wa magamba bila kusahau potential wanayoionyesha CDM bado watu wanahitaji kuhamasishwa???Kweli waTanzania wameridhika......Mkuu kwa kweli hapo kusema wapunguze spidi ni kwamba namuonea tu huruma rais wetu! Sijawahi ona serikali iliyokosa mwelekeo kama hii!
Halafu Chadema wana potential kubwa sana ukiacha hulo kusini ambako hawajaenda huku mjini tu kuna watu wangependa kuwa wanachama hata leo lakini ndo kama hivyo muihamasishaji hakuna!
Slaa amefanya nini zaidi ya kuimba wimbo wa UFISADI? Imebaki atoe wimbo wa Taarab aupe jina FISADI. Alete mambo mapya sio kukalia tatizo moja kila siku. Kila kipanda kwenye jukwaa anatoa list ya watu. Tunataka kusikia chama chake kina fanya nini bungeni? Uchaguzi umepita sasa wabunge wake wafanye kazi yao bungeni, na hii tabia ya kidemu ya kususa
waache.[/QUOTE
Umechangia kisiasa,kihisia pia sidhani Kama utakuwa unaelewa chochote.Kuwa mkweli usiwe mnafiki Ktk hili uliloandiaka