Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuomba hekima kwa Mwenyezi Mungu kutokana na matukio yanayotokea sasa nchini.

Alisema hali inayotokea sasa ni matokeo ya wananchi kupuuzwa na kutokusikilizwa katika suala zima la uwekezaji unaofanyika sehemu mbalimbali za nchi. Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana katika kijiji cha Giroda Babati vijijini, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika ziara yake ya siku tisa ya ujenzi wa Chama mkoani Manyara.

Kabla ya kutoa kauli hiyo Dk. Slaa aliwaomba wananchi wasimame kwa muda wa dakika moja, kuomboleza vifo vilivyotokea mkoani Mtwara.

Aliongeza kuwa kuendelea kuwapuuza wananchi wa Mtwara ni kuendelea kucheza na jipu linalopaswa kutumbuliwa na kwamba njia sahihi ni kukaa na kuwasililiza wananchi katika uwekezaji na kufikia muafaka pasipo kutumia nguvu. Alisema wanachotaka wananchi wa Mtwara ni kujua namna watakavyonufaika kwa kile alichoeleza kuwa katika uwekezaji wowote wanufaikaji wa kwanza wanapaswa kuwa wananchi.

Alisisitiza kuwa katika hali ya Mtwara kulihitajika busara za kawaida za kutatua msingi wa tatizo badala ya wananchi kupigwa mabomu, risasi na kisha kukamatwa.

“Ni jambo la aibu kuwapiga mabomu wananchi wanaodai kunufaika na rasilimali za nchi yao hapa kunahitajika elimu ya kuwafahamisha haki zao ni zipi na siyo mabomu.,alisema Dr Slaa.

Source:Tanzania Daima.
 
huyu mzee anahangaika tu amechoka kuchochea suala la kuchinja sasa kahamia kwingine,swali dogo hivi mzee slaa na jk nani aliyejitenga na mungu,kwa sababu mzee slaa aliasi dini na kufanya uovu mwingi ndani ya kanisa sasa uko wapi uadilifu wa slaa.
 
laana kutoka kwa nani..?

Hivi bado mnadhani slaa alishinda ... Znz kura hazikutosha.. Miji ya pwani hana umaarufu.. Labda kaskazini huko
Hakika wajinga ndio waliwao
 
kwanza anatakiwa akamatwe kwa uchochezi na kauli mbiu zake za uchochezi mfano nchi haitatawalika,mpaka kieleweke.slaa ni janga la kitaifa.
 
laana kutoka kwa nani..?

Hivi bado mnadhani slaa alishinda ... Znz kura hazikutosha.. Miji ya pwani hana umaarufu.. Labda kaskazini huko

Katika watu ambao wakisikia jina Slaa nyongo zinawatoka ni pamoja na wewe....Pole
 
Tatizo la Kikwete ni kuongoza nchi kwa nguvu za giza bila kumtegemea Mungu. Sheikh Yahya alipotamka hadharani kwamba amemtumia majeshi ya mapepo ili kumlinda alichekelea na kuyapokea kwa shangwe, hoihoi, vifijo na ndelemo bila kujua madhara yake. Sasa hayo mapepo ndiyo yanayomtafuna!!
 
MUNGU HACHANGAMANI NA SHETANI!! Kinachotakiwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu ateketeze kizazi chote cha kifisadi ili kuinusuru Nchi!!
 
huyu mzee anahangaika tu amechoka kuchochea suala la kuchinja sasa kahamia kwingine,swali dogo hivi mzee slaa na jk nani aliyejitenga na mungu,kwa sababu mzee slaa aliasi dini na kufanya uovu mwingi ndani ya kanisa sasa uko wapi uadilifu wa slaa.

jipu halina dawa pasi kutumbuliwa!
 
kwanza anatakiwa akamatwe kwa uchochezi na kauli mbiu zake za uchochezi mfano nchi haitatawalika,mpaka kieleweke.slaa ni janga la kitaifa.

mwenzio Ritz na ZeMarcopolo wameamua kurudi CDM baada ya kuona buku 7 haina thamani ya maisha ya watanzania wewe bado unahangaika lumumba?
 
Last edited by a moderator:
huyu mzee anahangaika tu amechoka kuchochea suala la kuchinja sasa kahamia kwingine,swali dogo hivi mzee slaa na jk nani aliyejitenga na mungu,kwa sababu mzee slaa aliasi dini na kufanya uovu mwingi ndani ya kanisa sasa uko wapi uadilifu wa slaa.
Kwa hiyo watu wasiokuwa watumishi wa kanisa au misikiti wamejitenga na mungu? ushauri wa Dr ndio suluhisho la kidiplomasia na si risasii..listen them! Kuwe na transparency kwenye mikataba watu waelewe faida zake...simple! USHIRIKISHAJI UMMA-Maendeleo kwa kila mtu!
au umesahau Mtwar wengi ni CUF na slogan yao inasema HAKI SAWA KWA KILA MTU!!
 
kwanza anatakiwa akamatwe kwa uchochezi na kauli mbiu zake za uchochezi mfano nchi haitatawalika,mpaka kieleweke.slaa ni janga la kitaifa.
Wewe ni maskini wa fikra...aina ya bacteria chafu ndani ya chakula!!
Kama huna cha kuchangia kaa kimya! Humu unajivua nguo kwa comments zako
 
huyu mzee anahangaika tu amechoka kuchochea suala la kuchinja sasa kahamia kwingine,swali dogo hivi mzee slaa na jk nani aliyejitenga na mungu,kwa sababu mzee slaa aliasi dini na kufanya uovu mwingi ndani ya kanisa sasa uko wapi uadilifu wa slaa.
Unatapatapa mithili ya mtu anayekata roho!! Yaani huyo Kikwete anayeua waandishi wa habari na kungo'a watu kucha na meno bado unamuona yupo karibu na Mungu? Mungu yupi? Mbona kila mtu anajua analindwa na majeshi ya majini ya Sheikh Yahya!!!
 
Huu ni mtihani mwingine wa kifikra kwa slaa, hivi anadhani ataendelea kuwahadaa wananchi kupitia matatizo yao hadi lini??? Kwa hiyo anashangilia vifo vya askari na mali za umma zilizoharibiwa???
 
Ukweli unauma . serikari hii haitaki ukweli. viko wapi viwanda Vilivyojengwa maeneo yatowayo dhahabu. GEITA,KAKOLA,KAHAMA. Tunapigwa vumbi tu mwaka wa 13 tangu madini yaanze kuchimbwa. watafute pesa wawaweke wanamtwara fresh kabla . usanii mtupu.
 
Back
Top Bottom