Lets wait and see,mahali panaponitatiza ni pale ambapo Dk Slaa and Mh Mbowe wanaweza kutofautiana na Mh Zitto kwenye suala la Dowans bila kuathiri mwenendo wa chama,hapo ndo nashangazwa,like i said...Lets wait and see.
Inafaa umuulize yaani kugandamiza kidogo tu jamaa ameshaniona ni kiongozi wa juu tena wa Chama Cha Vita CUF ,hivi hakusikia kama siku CCM ikianguka ndipo nitakapojiunga nayo na kuwa mwanachama nambari one ili kuimarisha upinzani.- Whaaat Mwiba ni kiongozi wa juu wa CUF hii ni kweli au Sasa mzee thibitisha hili au kubali umekurupuka!
Naona kuna makundi Slaa ,Mbowwe na Mwakiembe na upande mwengine kuna Lipumba ,Zito na kundi kubwa katika kikao cha juzi hivyo ni bora tukapata vyama vitatu ,Chadema CUF na Sultan CCM ,halafu tuweke uchaguzi wa haki tuone.
Mwakiembe aende Chadema ,Zittto akimbilie CUF na Sultani abakie kama alivyo akiwa na migogoro kibao ya takirima tuelekee uchaguzi mkuu ,Zitto anaweza kuipata nafasi ya kugombea Uraisi 2010 kupitia CUF ,naamini ni nafasi ambayo atapewa tu bila ya matatizo yeyote na asifanye mchezo wa kuamini kuwa Chadema watampatia sidhani kabisa kwanza kule Chadema kuna ukabila au mnaonaje ?
Labda kwanza tuzungumzie kubadili katiba ili kuwezesha vijana (chini ya miaka 40) kugombea nafasi hiyo nyeti.s 39.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Mzee Mwanakijiji & Invisible,
Nafikiri huu sio tena wakati wa kutoa press conferences maana hazisaidii upinzani kabisaa. Hizi zinawaumiza zaidi CCM na ndio maana Malecela akawakataza wanaCCM wasizitumie na sio wapinzani.
Wapinzani inatakiwa sasa tuanze kuchukua hatua ngangari zaidi za kumuondoa au kummaliza nguvu Kikwete kama maandamano, migomo, mikutano ya hadhara n.k.
Hii ndio njia pekee iliyobaki maana kama tulivyomsikia Mzee Malecela ameshaeleza kuwa Kikwete anachoogopa ni upinzani ndani ya CCM na sio nje yake.
Niweke rekodi ili wachangiaji waweze kujua kilichozungumzwa na kimezungumzwa wapi.
Tangu jana CHADEMA wamekuwa na Kamati Kuu ya chama TAIFA na leo wanaendelea na kikao cha Baraza Kuu la Chama Taifa.
Hivyo basi kutokana na mikutano hiyo Kamati Kuu jana ilifanya maamuzi mengi juu ya mwelekeo wa chama na Taifa kwa ujumla.
Ni kweli jana wanachama 12 wa chama walifukuzwa uanachama kutokana na ripoti maalum iliyokuwa imetokana na KAMATI NDOGO YA KAMATI KUU iliyoundwa mwaka jana mwezi wa kumi na moja ikiwa inaongozwa na mwanasheria mahiri mzee Bob Makani.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa ni pamoja na ;
Prof.Baregu, Mustafa Akoonay ambaye ni wakili wa kujitegemea na mjumbe wa kamati kuu, Edson Mbogoro mwanasheria wa kujitegemea kutoka Ruvuma,Mama Chiku Abwao .
Makatibu wa kamati hiyo walikuwa ndugu Tundu Lissu akisaidiana na Halima Mdee.
Baada kazi ya kamati hiyo walifulkuzwa wanachama 12 ambao walikuwa wakijiita wanachama wa Dar es salaam huku wakuwa wanatumiwa na CCM kukivuruga chama.
Mtakumbuka pia kuwa wakati wa mchakato wa uchaguzi Tarime hawa jamaa ile wiki ya mwisho waliandamana kupinga chama kushiriki uchaguzi Tarime kwa hoja kuwa kilihusika kumuua Wangwe.
Kuhusu Rostam.
Leo Dr.Slaa kaamua kuuvunja mzizi wa fitna pale alipoweka wazi kile ambacho kinaendelea kati ya Rostam , Mwakyembe e.t.c kwa kuweka ukweli hadharani juu ya kampuni ya kuzalisha umeme ambayo inamilikiwa na Rostam inaitwa PE (POWER ENERGY).
Kampuni hii inalitaka eneo la kijiji kinaitwa Kisasida , na kampuni ya Rostam inamilikiwa kwa ubia wa yeye pamoja na Lowassa , na ndio maana utaona jinsi ambavyo mkuu wa mkoa wa Singida alikuwa mstari wa mbele kuibeba kampuni hii ya Rostam na Lowassa .
Hili limepelekea CHADEMA kumfikisha mkuu wa mkoa mahakamani na tangu jana alishapelekewa barua ya kusudio la kuburuzwa mahakamani baada ya kumtukana mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na viongozi wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara.
Kampuni hii ya PE na ile ya wakina Mwakyembe wako kwenye kupigania kupata eneo kwenye kijiji hicho.
Mengine nitawaeleza zaidi baadae.
Hivi Tanzania hatuna sehemu za kusajili intellectual property? Kama vipi unamwacha anaiba plan/idea halafu unampiga bonge la suit.
wewee patamu hapo! chezo ndio kwanza linaanza..![/QUO
Watu wenye mawazo ya aina hii ndio wametufikisha hapa tulipa yaani nchi viongozi mafisadi na wasiojali maslahi ya watanzania.
Ni kosa kubwa sana kufananisha jitihada hizi za wapiganaji wetu kama akina W. Slaa na mchezo wa kuigiza. Hawaigizi,men at work bwana
Hivi Tanzania hatuna sehemu za kusajili intellectual property? Kama vipi unamwacha anaiba plan/idea halafu unampiga bonge la suit.