Dr. Slaa makampuni yasiyorejesha pesa za EPA hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa makampuni yasiyorejesha pesa za EPA hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 7, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Slaa alipua kombora jingine
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbord Slaa, amelipua kombora jingine kwa kuziweka hadharani kampuni zilizoshindwa kurejesha fedha za madeni ya malipo ya nje (EPA) kwa kile alichokiita kukingiwa kifua na vigogo wa serikali. Hatua ya Dk. Slaa imekuja ikiwa ni siku mbili tu tangu alipomshukia Rais Jakaya Kikwete akimsakama kwa kushindwa kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi na kutatua matatizo ya kiuchumi ambayo yameiyumbisha nchi. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Dk. Slaa alisema kuwa pamoja na kauli za ukali zilizotolewa na Rais Kikwete muda mrefu uliopita, akiwataka waliokwapua fedha za EPA kuzirejesha kwa hiyari yao wenyewe na kutishia kuwachukulia hatua za kisheria, hadi sasa ni kampuni nane tu kati ya 21 zilizorejesha fedha hizo.


  Alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa Rais Kikwete amekaa kimya bila kuchukua hatua wala kusema chochote dhidi ya kampuni zilizodharau agizo lake na kwamba inaonyesha ni jinsi gani serikali na CCM imeelemewa na ufisadi na imeshindwa kuchukua hatua kwa kuwa ufisadi umejikita katika mfumo mzima unaowagusa pia viongozi waandamizi katika chama na serikali. Alionya kuwa kwa kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu huo, namna pekee ya kusimamia uwajibikaji ni kwa kuunganisha nguvu za wananchi katika kutetea rasilimali za taifa.


  Slaa alitaja kampuni zilizorejesha fedha hizo na kiasi katika mabano kuwa ni

  • Bencon International Ltd iliyorejesha sh bilioni 7.96 kati ya bilioni 10.56 ilizokwapua;
  • Njake Hotels and Tours & Njake Enterprises Ltd iliyorejesha fedha zote sh bilioni 2.225; na
  • Ndovu Soap sh bilioni 1.548 ambazo ni kiasi chote ilichokuwa imekichukua.
  • Kagoda Agriculture, (bilioni 34.781),
  • VB & Associated (bilioni 9.227),
  • VB Holdings Ltd (bilioni 5.148),
  • Venus Hotels & Apartments Ltd (bilioni 4.050) na
  • Bora Hotels & Apartments Ltd (bilioni 5.779).

  Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50. Dk. Slaa alidai kuwa CHADEMA ilitarajia kwamba mwaka 2011 ulikuwa wa kukamilisha uchunguzi na uchukuaji wa hatua dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali ili kurejesha utamaduni wa uwajibikaji. Badala yake serikali imeendelea kuahirisha kuchukua hatua kamili serikalini, bungeni na hata ndani ya chama chenyewe.


  Aliongeza kuwa katika hali ya kusikitisha Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa ya Disemba 31, 2011 hakuzungumzia hatua ambazo serikali yake imefikia katika kushughulikia mafisadi. Juzi akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na hotuba ya Rais Kikwete ya kufunga mwaka, Dk. Slaa alidai kuwa hali ya uchumi inazidi kudorora na serikali haionyeshi mikakati yoyote ya kulinusuru taifa. Alisema kuwa badala yake, Rais Kikwete amekuwa akitoa majibu yanaisukumia lawama hali mbaya ya uchumi ya kidunia, wakati angeweza kufanya jitihada za kuondokana na hali hiyo, na hasa kuwachukulia hatua watu wote wanaotuhumiwa kuhujumu mali ya taifa.   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunaiomba sasa serikali itoe maelezo ya kuridhisha kuhusu taarifa ya Dr Slaa
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jk na washirika wake wana roho ngumu sana! Hivi wataficha wapi nyuso zao? watajisafishaje mbele ya jamii?

  Tanzania kama tuijuavyo!
   
 4. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa taarifa nzuri sana ila tunaomba uwe wazi hapa:

  (Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50.)
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mbona hayako hadharani, majina wanayo.
   
 6. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Usanii mkuu, sio kwenye luninga tu!
   
 7. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa staili hii serikali inapumua kwa shida.Dr endelea kutujuza zaidi.
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali ya JK aibu ilishafutika katika nyuso zao, subiri tu utakuja sikia wanaibuka kwa kuwahutubia wazee wa DMS
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Viva sana Katibu wa Chama!
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Safi sana Dr.Slaa
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Aisee, waandishi wa Tanzania kiboko; kwani kile kilichosemwa wakati ule wa uwakilishi wa repoti ya tume ya Mwanyika, Mwema sijui na nani yule ilisema je?

  Report ilisema makampuni mengine yalishindikana kupatikakana kwa kuwa hata hayo makampuni ya nje hayakuweza kupatikana ili kuwezesha kufuatilia ukweli;


  Sasa hapa news ni nini? Jamani yani hata kukiwa hamna cha kuandika lazima muandike tu?
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Natumaini inaeleweka kutokana na kitu kinachoeleweka kama uamuzi wa busara kutoweka hapa, ila ipo siku mambo yatawekwa hadharani. Gazeti kama mnavyojua tasmini ya wahariri wanapoweka kitu hadharani lazima utafiti ufanyike na kujiridhisha, vinginevyo wakigeuziwa kibao hawatakuwa na pakutokea ingawa Dr. ameanika hadharani.

  Nadhani Vyombo vya habari vinafanya jitihada kuhakiki makampuni hayo yasiyolipa na ukweli utaanikwa hadharani punde tu. Thanks.
   
 13. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kauli kama hizi ndizo zinazoendeleza rushwa na kurudisha maendeleo nyuma.
  Kauli hii haina tofauti na mchakato umeanza, upembuzi yakinifu unaendelea, mfadhili anatafutwa , wananchi watafahamishwa, siri ya serikali..bla bla kibao,
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Serikali na TAKUKURU ilikuwa wapi siku zote hadi Dr Slaa alipoibua kashfa hiyo? Bila jitihada za Dr. Slaa kashfa hiyo isingeibuliwa, na kwa kutetea wahusika Kikwete aliwakingia kifua na kuwaomba warejeshe pesa kwa hiari badala ya kuwaamuru warudishe pesa na kufunguliwa mashtaka ya wizi.

  FaizaFox acha mipasho wakati tunapojadili mambo muhimu yenye masilahi kwa taifa na taifa linapoathirika we ni mmoja wapo. Umeona Wabunge wa Dar walivyoungana na hata CCM dar ilivyoungana na wanachi wa Kigamboni kudai na kutetea unyanyaswaji wa serikali ya Kikwete, hivyo ndivyo inavyotakiwa kufanya na kuungana tunapotetea maslahi ya kitaifa kuliko mwelekeo wako wa kimipasho tu bila kujadili hoja kwa kuangalia cause and effect.
   
 15. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Hebu peleka kule umagamba wako,karibuni litatangazwa,miaka inakatika tu..Dr wa ukweli endelea kutwanga,tupo nyuma yako!
   
 16. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona gazeti limetuficha hizo kampuni ambazo hazikurejesha fedha zetu jamani, nina hiamini JF ni jukwaa huru, naomba mtu mwenye hayo majina ya hizo kampuni ambazo hazikurejesha pesa zetu hatuwekee hapa Jamvini;

  "Hata hivyo, alizitaja kampuni 13 ambazo zimegoma kurejesha fedha hizo (majina tunayo) na kwamba hazijalipa jumla ya fedha zote zinazokisiwa kufikia sh bilioni 50"
   
 17. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huyu Slaa hana mambo mengine ya msingi ya kufanya? Anachoona TZ hii ni ufisadi na EPA tu?
  Ni muda muafaka kwake kubadilika, tunataka kusikia mambo mapya kutoka kwake, siyo haya ambayo yameshaota sugu masikioni mwetu!!
   
 18. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mwito kwa vyombo vya habari hebu msikimbizane na issue za Magufuli na "Wakazi bandia" wa Kigamboni mf. Mtemvu et al.

  Iandikeni sana hii kitu from different angle and with diffent approaches. Msisahau ile ya GGM, Posho, Kufilisika kwa Serikali, Ububu wa Ikulu na Kigugumizi cha ofisi ya Waziri Mkuu juu ya kushughulikia majanga na madai ya wafanyakazi (walimu, madaktari wanafunzi-interns), Mfumuko wa bei na kuporomoka hali ya maisha ya Mtz.

  Kimbizeni na hayo mambo mpaka watatafutana huko ndani hadi kutoa vichwa na kutajana wahusika wa kila madudu.

  Kuushughulikia uhuni na wahuni wa kupeleka watu wapandishe mwenge mlima Kilimanjaro kwa pesa ya Kodi ya Mtanzania halafu wasifike na kutuletea picha kanyaboya unatija kwa watz kuliko kupanda nauli za kivuko(hili lina namna bora ya kulishughulikia hata sasa kuliko mipasho yao)
   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,754
  Likes Received: 6,029
  Trophy Points: 280
  Hebu tujuze Mkuu maana inaonekana wewe uko huko jikoni; "karibu" ndio lini? Hiyo karibu isiyofikia tamati ndio ipi? Au ndio yale yale ya "tumpe rais muda"? Amini usiamini awamu hii itamaliza muda wake ikiacha suala la EPA bila tamati.
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nadhani tusuburi jumatano Mwanahalisi watachapisha majina yote
   
Loading...