Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,449
- 283,760
ni katika viwanja vya NHC , njia panda ya uwanja wa Taifa karibu kabisa na CHUO KIKUU CHA UALIMU - DUCE , kwa mujibu wa matangazo kutoka kwenye gari la matangazo mkutano huo utaanza majira ya saa 8 mchana . wito wangu kwa wana Temeke TUSIKOSE KUHUDHURIA MKUTANO HUU , KUTEMBELEWA NA DR SLAA NI BAHATI KUBWA NA HESHIMA KUBWA SANA KWETU , HUYU NDIYE MKOMBOZI HALISI WA NCHI , KILA MAHALI NCHI HII WANAMLILIA , PIIIPOOOOZZZZZ !!!!!
==========
UFAFANUZI
==========
==========
UFAFANUZI
==========
Wakuu.
Kuna taarifa imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii (Jamiifroums ikiwemo) kuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atafanya mkutano mkubwa wa hadhara kesho wilaya ya Temeke.
Kwa heshima na taadhima naomba kukanusha na kuweka kumbukumbu sawasawa kwa kusema mambo mawili ya muhimu.
1. Ni kweli kuwa kesho jumapili tarehe 11 Mei, 2014 CHADEMA kitafanya mkutano mkubwa wa hadhara wilaya ya Temeke kama jinsi kinavyo fanya mikutano kwenye maeneo mengine kwa madhumuni ya kujenga na kueneza falsafa, itikadi na sera za chama kwa wanachama, wapenzi, na mashabiki wake maeneo mbalimbali .
2. Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa hatakuwepo kwenye mkutano huo wa Temeke kesho bali watakuwepo viongozi na maafisa wengine wa chama. Dr Slaa kwa sasa pamoja na makatibu wenzake wa vyama vingine (vyama vinavyounda UKAWA) wana majukumu ya UKAWA ambayo anaendelea nayo.
Hivyo ni muhimu kila aliye pata taarifa za uwepo wa nguli za siasa za upinzani Tanzaniza (Dr Slaa) kuwa atakuwepo kwenye mkutano wa hadhara wa kesho unaotarajiwa kufanyika wilaya ya Temeke afahamu kuwa hatakuwepo kama ilivyo tangazwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, lakini nadhibitisha kuwa mkutano huo utakuwepo kama ulivyopangwa.
Tunaomba wanachama na wapenzi wetu wapokee taarifa hii kama taarifa rasmi na tunawapo pole kwa usumbufu wowote ambao utakuwa umejitokeza na nawakaribisha sana kwenye mkutano huo.