Kama kawaida yake anaenda kuwakumbusha wanachuo waanze kufanya maandalizi ya maandamano. Kwa maana halisi kwamba huyu mzee huwa kazi yake ni matukio hataongea cha maana zaidi ya Katiba na mambo ya Mbunge wa NCCR-MAGEUZI Kafulila. Wakati sisi tunategemea azungumzie kinachojili ndani ya chama. Kwanini viongozi na wanachama wa Chadema wanaondoka kila kukicha na kuamia vyama vingine? Je ni kweli wamekosa strategies mbadala kama alivyosema Kitila na Mwigamba kwenye waraka wa mabadiliko 2013? Au ni kwasababu ya udikiteta wa Mwenyekiti na Katibu kukataa kuitisha uchaguzi wa Viongozi wakuu wa chama? Kilichobaki sasa hivi ni kila kukicha wanakuja na ratiba ya uchaguzi ambayo haitekelezeki.