Dr. Slaa kumnadi Magufuli Jumatano

Dr. Slaa kumnadi Magufuli Jumatano

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,178
Baada ya mambo kuwa magumu ndani ya ccm hasa baada ya kuona nguvu ya lowassa ikizidi kuongezeka kwa kasi, sasa aliyekuwa katibu mkuu wa chadema, Dr. Wilibrod Slaa atamnadi mgombea wa urais wa ccm Dr. Magufuli.

Habari kutoka lumumba zinasema kwamba, awali Slaa ilikuwa atumike kuinadi ACT-Wazalendo lakini ikaonekana kwamba asingeweza kushwawishi wapiga kura katika kipindi hiki cha kampeni kuikubali ACT.

Lengo la kuinadi ACT lilikuwa kupunguza kura za upinzani hasa katika mikoa ya kigoma, tabora, ruvuma, kagera na mikoa ya kaskazini, lkn ikaonekana kwamba bado asingefanikiwa kushawishi wananchi.

Hivyo Dr Slaa atatumika kumnadi magufuli chama ambacho yeye amekuwa akikipinga na kusema tatizo sio mgombea bali mfumo wa chama chake ndio mbovu.
Sasa tunashuhudia Slaa akisimamia asichokiamini.

source: mwanahalisi
 
..............
 

Attachments

  • 1444024439149.jpg
    1444024439149.jpg
    48.3 KB · Views: 12,764
Mwacha amnadi tu, sisis ccm tunasema tatizo ni mtu siyo mfumo, chadema na ukawa ni wezi na wauaji, ni hatari kwa usalama wa taifa hamfai kupewa nchi,
 
Slaa akifanya hivyo ataonesha unafiki wake hadharani.
Hata wale wafuasi wachache aliobakia nao watauona usaliti wake.
Na atathibitisha rasmi kuwa ana chuki binafsi na Lowassa na sio zile blah blah zake alizoziongea pale Serena.
 
Slaa akifanya hivyo ataonesha unafiki wake hadharani.
Hata wale wafuasi wachache aliobakia nao watauona usaliti wake.
Na atathibitisha rasmi kuwa ana chuki binafsi na Lowassa na sio zile blah blah zake alizoziongea pale Serena.

Mkuu, yaani kwa kifupi atakuwa amejishushia hadhi yake kwa kiasi kikubwa.
 
Dr. nilifikiri ungeweza kuwa Raisi wa Tanganyika,
Watanzania wamechoka, sio wewe , wewe ni sehemu ya hawa watanzania waliochoka,Jaribu kufikiri kimakini, jinsi upepo unavyokwenda
 
Back
Top Bottom