Dr Slaa kufikishwa Mahakamani!

Dr Slaa kufikishwa Mahakamani!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
WanaJF,

Kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo Dr Slaa amezielekeza kwa mkuu wa nchi, rais wa JMT, Dr Kikwete, wadau mbalimbali wamejipanga kuhakikisha Dr Slaa anapelekwa mahakamani kwa lengo moja tu, nalo ni kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya mkuu wa nchi.

Dr Slaa ambae ni katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini (CHADEMA) ameelekeza tuhuma nzito kwa rais Kikwete bila kutoa ushahidi wowote wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya alhamisi ya tarehe 16/10/2014.

Wadau hao wamesema kwa kipindi kirefu tu wamekuwa wakimpuuza Dr Slaa kutokana na tuhuma zake hewa dhidi ya CCM na viongozi wa serikali, lakini wadau hao wameongeza kwamba, kwa hatua ambayo Dr Slaa ameifikia sio tena ya kupuuzwa, bali anapaswa kuwajibishwa.

Aidha, itakumbukwa kuwa ni desturi ya Dr Slaa kuongea maneno ya hovyo kutokana na tabia yake ya kuokoteza habari za vijiweni ambazo kimsingi hazina tija yoyote kwa Watanzania. Hivyo wadau hao wameazimia kumuadabisha kutokana na tabia yake.
 
Kweli chuki ya moyo husomeka usoni. Kuswekwa mahakamani ni kitu gani?


Ninyi mnamwajibisha Dr. Slaa kama nani?
s
Kwa akili zenu za panzi unadhani Dr. hana ushahidi au anaogopa kwenda mahakamani?

Mara ngapi mmeambiwa kama mnabisha muende mahakamani lakini mnaishia kuuf.....ta kama allivyosema waziri wenu wa maji na nishati mtarajiwa Asha Bakari.

Tena mmechelewa na hilo ndilo hasa la ninyi kwenda mahakamani tunalitaka ili mzidi kuumbuka. Mtatembea uchi hadi mkome, wenda wazimu!
 
Kama ni habari za kuokoteza mnataka kumburuza mahakamani kwa vigezo gani?

"Ukiwa unasikiliza wimbo na ukaguswa na maneno ya huo wimbo lazima adondoshe chozi la furaha ama la hudhuni"
 
Hamida bwana , nakumbuka ile list of shame mlisema mtampeleka Dr slaa mahakani...mpaka leo Magamba hamjasema kitu...uzuri wa Dr Slaa huwa ana data zote....ni vizuri kama kweli magamba mnajiamini nendeni mahakamani..ama kweli Dr Slaa ameyashika Magamba pabaya...pole hamida
 
Hapa kawafunua tu wamebaki nusu uchi, sasa waende mahakamani wakaachwe uchi wa mnyama kabisa. Siku zote walikuwa wanaogopa kwenda huko mahakamani wasije umbuka zaidi eti wanajikosha "tumekuwa tukimpuuza kwa maneno yake ya kuokoteza" leo wanajitoa ufahamu na kwenda huko, haya yetu macho.
 
Kumbe bado unaexist? mzima lakini? Manake wewe umekuwa kazi yako ni moja tu kuapmbana na dr slaa. Ila kwa muda haukuwepo hewani au ulikuwa unakuja kwa ID tofauti. Au wewe ni Nape?
 
Ni upuuzi kumpeleka mahakamani huyo mwehu. Anatafuta umaharufu wa bure. Ni sawa na kumkimbiza mwehu aliyepeleka nguo zako ulipokua unaoga mtoni.
 
Ni upuuzi kumpeleka mahakamani huyo mwehu. Anatafuta umaharufu wa bure. Ni sawa na kumkimbiza mwehu aliyepeleka nguo zako ulipokua unaoga mtoni.

Eti mwehu?? mpelekeni basi msikie mziki wake!
 
Sister HAMIDA acha kubwabwaja kama BATA apelekwe mahakamani kwa kosa gani hasa?
 
the country of drama, cat & rat tom & jerry.
hivi lile saga la dogo (waandish makanjanja) liliishia wapi maana nayealimfungulua Dr, kesi ya udhalililishaji hukumu yake bado hadi leo. au jaji alitoroka na faili.
 
Sema wewe ndio utaenda kufungua hiyo kesi, unaruhusiwa na siyo unatudanganya eti wadau! Mbona una act kama gazeti la uhuru? Bytheway ulipotelea wapi?
 
Ni upuuzi kumpeleka mahakamani huyo mwehu. Anatafuta umaharufu wa bure. Ni sawa na kumkimbiza mwehu aliyepeleka nguo zako ulipokua unaoga mtoni.

Ok unamwita kiongozi wetu mwehu nasi tukiamua kumwita jk mwehu utafurahi? Mbona mnakosa uvumilivu jamani?
 
Mmezidi na tishia nyau. Sana sana mtaishia kutuma policcm kukamata computer za cdm. Kwa taarifa yako kila kitu ni cloud siku hizi. Upo hapo?

Acheni kutumika nyie manyang'au.
 
Ni upuuzi kumpeleka mahakamani huyo mwehu. Anatafuta umaharufu wa bure. Ni sawa na kumkimbiza mwehu aliyepeleka nguo zako ulipokua unaoga mtoni.

Dr.Slaa inatakiwa apelekwe mirembe akatibiwe.
 
Back
Top Bottom