Dr. Slaa: Kikwete Amerahisisha Urais

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Mwl Jk Nyerere(RIP) aliwahi kusema, urais ni mzigo haukimbiliwi. Na ukweli hiyo ndio sababu kubwa mwaka 1985 hakuna aliyeelezea nia yake ya kuwa rais. Mwinyi yeye aliirahisisha urais sana na wakajitokeza watu wengi sana kumrithi.

Kuna rafiki yangu nilikuwa nazungumza nae kwa simu ananiambia alikuwa na informal conversation na Dr Slaa jana akawa anamwambia kwa jinsi JK anavyoongoza nchi kishkaji kila mtu anajiona anauweza urais. Anasema usishangae wakajitokeza watu mia mbili come 2015 kuutaka urais maana hata diwani nae atataka awe rais. Alikuwa hamzungumzii Zitto lakini inaonyesha hata Zitto ameona kazi ile ni laini sana hata yeye anaweza!
 
Nakubaliana na Slaa ata mjumbe wa nyumba kumi kwa sasa anatamani kuwa RAISI
Kwa sasa iyo TITLE imekosa heshima kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu
Imagine watu wanadiscuss namna ya kukuridhi 4 years kabla ya uchaguzi ujao ni aibu.
Ni sawa na mzazi aliye hai wanawe wanadiscuss namna ya kugawana mali manake wataharakisha mzazi kufa mapema wagawane mali
 
Binafsi sioni km amerahisisha, kwa jinsi JK alivyochemsha kwa mtu mwenye upeo lazma aelewe kuwa urais cyo kila mtu anauweza. Kama wewe ni KJ (Kubwa jinga) huwez kuongoza nchi.
 
siku hizi hata wapiga debe nao wanaona wanaweza kuwa maprezdaa wa hili li tz letu. kweli ya urais taasis imekosa heshima kabisa
 
hata hivyo uraisi rahisi..hata mi naweza kupanda ndege tu kila siku..
 
Mwl Jk Nyerere(RIP) aliwahi kusema, urais ni mzigo haukimbiliwi. Na ukweli hiyo ndio sababu kubwa mwaka 1985 hakuna aliyeelezea nia yake ya kuwa rais. Mwinyi yeye aliirahisisha urais sana na wakajitokeza watu wengi sana kumrithi.

Kuna rafiki yangu nilikuwa nazungumza nae kwa simu ananiambia alikuwa na informal conversation na Dr Slaa jana akawa anamwambia kwa jinsi JK anavyoongoza nchi kishkaji kila mtu anajiona anauweza urais. Anasema usishangae wakajitokeza watu mia mbili come 2015 kuutaka urais maana hata diwani nae atataka awe rais. Alikuwa hamzungumzii Zitto lakini inaonyesha hata Zitto ameona kazi ile ni laini sana hata yeye anaweza!
Hayo ni mawazo yako wala hutakiwi kumhusish Slaa.
 
kupanda ndege ni kazi ngumu?na mimi nautaka urais
Yeah unakaa tu hapo Ikulu unaongoza kishakaji, huumizi kichwa kuhusu matatizo kama ya umeme, maji, migomo nk. Ukiona kuna tatizo unasafiri hadi likitatuliwa ndio unarudi. Kweli urais mtamu, hata diwani ana kazi kubwa kuliko rais
 
Mwl Jk Nyerere(RIP) aliwahi kusema, urais ni mzigo haukimbiliwi. Na ukweli hiyo ndio sababu kubwa mwaka 1985 hakuna aliyeelezea nia yake ya kuwa rais. Mwinyi yeye aliirahisisha urais sana na wakajitokeza watu wengi sana kumrithi.

Kuna rafiki yangu nilikuwa nazungumza nae kwa simu ananiambia alikuwa na informal conversation na Dr Slaa jana akawa anamwambia kwa jinsi JK anavyoongoza nchi kishkaji kila mtu anajiona anauweza urais. Anasema usishangae wakajitokeza watu mia mbili come 2015 kuutaka urais maana hata diwani nae atataka awe rais. Alikuwa hamzungumzii Zitto lakini inaonyesha hata Zitto ameona kazi ile ni laini sana hata yeye anaweza!
Mkuu, kwa hiyo huyo rafiki yako kila anachokuambia unakubaliana nae!
 
Kwani Dr Slaa kama mtanzania anayeiona nchi inavyoongozwa hawezi kutoa maoni kama haya? Je, ni mambo ya uongo kuhusu udhaifu wa Rais hata nafasi ya urais kutakwa na watu ambao hawana uwezo?
 
Binafsi sioni km amerahisisha, kwa jinsi JK alivyochemsha kwa mtu mwenye upeo lazma aelewe kuwa urais cyo kila mtu anauweza. Kama wewe ni KJ (Kubwa jinga) huwez kuongoza nchi.
Hii niliyobold imekaaje mshikaji? Mbona ukizigeuza hizo herufi maana yake inakuwa sooooo zaidi? Omba radhi mshikaji noooooooma!!!
 
Nakubaliana na Slaa ata mjumbe wa nyumba kumi kwa sasa anatamani kuwa RAISI
Kwa sasa iyo TITLE imekosa heshima kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu
Imagine watu wanadiscuss namna ya kukuridhi 4 years kabla ya uchaguzi ujao ni aibu.
Ni sawa na mzazi aliye hai wanawe wanadiscuss namna ya kugawana mali manake wataharakisha mzazi kufa mapema wagawane mali

Urais mzigo. Hata ule wa Tenga tu unamtoa kamasi jamani. Ni kama kuwa mzazi. Watoto wote wanakuangalia wewe. Hawajui umepata au la. Ada lazima itimie na wale pia wavae. Noma.
 
Dr Slaa anahusikaje sasa hapa! Wala usimweke Rais wetu kwenye hili endeleeni tu na huyo rubani wenu...
 
Ni hapa Tanzania tu tunaweza kukuta kuwa urais umerahisishwa kama kazi ya kuuza njugu. Mtu hajiulizi kwanini anataka kuwa rais. ukimwuliza anasema kwamba katiba inampa haki ya kugombea. ukidadisi zaidi utaona upeo wa anayetaka kuwa rais hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi.
 
Hebu fikiria kuna mkutano wa marais alafu nchi kama Uganda inawakilishwa na Y. Mseveni, Kenyatta anaiwakilisha Kenya, Malawi Prof Mtharika, Rwanda Kagame, Zambia M. Satta alafu eti Tanzania tunawakilishwa na Makamba au Kigwangalla. (Kweli!!) Tunataka rais wa kwenda kutoa shikamoo kwa marais wenzake na kuwabebea mafaili? Hawa vijana wamejipima kidplomasia? au wanajipima kwa rais aliyepo? Kiwete kwa maoni yangu hajawafikia marais wote waliomtangulia nchi hii, lakini ni bora mara mia ukimlinganisha na hawa 'watoto' ambao wanatamani ofisi kuu ya nchi hii.

Hawa hawajamaliza hata kipindi kimoja cha ubunge, hawako hata kwenye 20 bora ya wabunge waliopo sasa hivi. Eti wanauota urais (kweli???) Hivi kama Nyerere ndiye angekuwa anaachia kijiti wangejipanga katika mstari wa kumpokea kweli? Hivi wanajiona wangeweza kuvaa viatu kama vya mzee Mwinyi? Urais nchi hii umeshuka kiasi hiki? Kutoka kupanda tumbaku ukaenda chuo kikuu ukarudi kugombea ubunge umeshafaa kuwa rais? (Kweli???) Au kutoka chuo kikuu ukapata nafasi ya kuandika hotuba za rais, ukagombea ubunge umshajiona unafaa kuwa rais? (Kweli???)

Kampeini yangu kuheshimi Ikulu yetu haitakoma leo, tunahitaji kuheshimu Ikulu yetu na mtu anayekaa pale lazima awe na hadhi ya mtazania namba moja kweli. Nchi isiyoheshimu Ikulu kasri yake sijui ni nchi ya aina gani. Nadhani hatukumuelewa Mwl Nyerere aliposema Ikulu ni mahali 'patakatifu' au hatuelewi maana ya 'utakatifu'. Haiwezekani kila mtu ajione anaweza kuwa rais, kwanza ni kumdharau rais aliyepo na kudharau cheo cha urais ambacho ni alama ya nchi kimataifa.
 
Back
Top Bottom