Elections 2010 Dr Slaa haya maswali nataka unijibu kabla yakuweka vote kwako

Darwin

JF-Expert Member
May 14, 2008
908
56
1.Uchumi au kushuka shilingi ya Tanzania kama iko kwenye victoria falls

Utaukuzaje uchumi wa Tanzania na shilingi ya Tanzania kuwa yenye thamani?

2. Elimu ya Tanzania

Utafanya mbinu gani kukuza kiwango cha elimu Tanzania?
Utafanya mbinu gani kuhakikisha kwamba watoto wakitanzania wanakwenda shule nakumaliza la saba kwenye shule ambazo hawakai chini?
Utapunguzaje uhaba wa walimu shule za msingi na sekondari?

3.Miundo mbinu

Utafanya mbinu gani kuhakikisha kwamba angalau japo kila mkoa wa Tanzania una barabara ya uhakika kutoka makao makuu ya nchi?
Utafanya mbinu gani kupunguza foleni kwenye miji mikuu?
Utafanya mbinu gani kuzifufua hata kama sio kuziendeleza njia za reli za Tanzania?
Juzi kwenye mkutano Kilimanjaro ulikua unazungumzia kufufua uwanja wa ndege wa Moshi, Kabla hujafufua viwanja vya ndege huoni ni muhimu kuwa na usafiri wa uhakika ardhini kwani sio watanzania wengi waliokua na uwezo wa kulipia nauli za ndege?
Kwanini bandari kama Tanga, Bagamoyo, Mtwara hazipanuliwi kuepuka msongamano wa magari makubwa ambayo yote yanachukulia mizigo yao Dar- es- Salaam? Tukikuchagua utafanya nini?

4. Ajali za barabarani

Tanzania inaongoza sasa afrika ya mashariki nzima kwa kuwa na orodha ya ajali za barabarani. Utafanya mbinu gani kupunguza hii chinjachinja inayofanyika kila siku nakupoteza maisha ya watanzania wengi?

6. Afya
Juzi nilisikia kwamba upande wa pili[visiwani] kwamba wananchi wa huko hawapigi hatua nyingi mpaka kufika kwenye vituo vya afya.
Je huku Tanzania bara utafanya mbinu gani kufanya wananchi wawe karibu na vituo vya afya nakutopoteza maisha ya wananchi kabla hawajafika huko?

7.Wakulima wadogowadogo
Utafanya mbinu gani kuhakikisha kwamba mazao yao wanayauza kwa bei yenye faida bila kuwa na ushindani na mazao ambayo yanaletwa kutoka Afrika ya kusini?

8. Watoto wa mitaani na walemavu
Utafanya mbinu gani ili kuwaokoa watoto ombaomba wa mitaani ambao maisha yao yako hatarini kwa kugongwa na magari wakiwa barabarani wakiomba?

9.Tatizo la umeme
Utafanya mbinu gani kuhakikisha kwamba wale ambao wachache wana umeme wawe na umeme wa uhakika siku 365?

10. Muungano
Utafanya mbinu gani kuurekebisha muungano ambao wenzetu wavisiwani wanalalamika kwamba muungano hauna usawa?


11. Maisha ya watanzania
Utafanya mbinu gani kuhakikisha kwamba kila mlipa kodi wa Tanzania anafaidika na kodi zinazokusanywa?

Maswali ni mengi ila naongeza hili ambalo penginepo nilakiupendeleo

Kwanini tumbaku ilimwe kwa wingi Tabora lakini kiwanda kiwe Morogoro na hapohapo watu wa Tabora hawana barabara nzuri zakuunganisha na mikoa mingine?


Jerry
 
Kwanza KATIBA, ataileta tuirekebishe iondoe mianya yote ya ufisadi, baada tunachukua ile siasa iliyomtoa kaburu na vibaraka wake Ian Smith pangoni licha ya maguvu yao, tutahamasisha wananchi wachukie ufisadi kama enzi zile za Azimio la Arusha, sijui kama mnakumbuka jinsi wenye kupenda unyonyaji walivyonyanyasika, USIWE KUPE JITEGEMEE- Tofauti yake this time itakuwa na mkakati wa kuleta maendeleo endelevu, wakati ule mkakati ulikuwa wa kuwaondoa wanyonyaji, wakoloni, mabwenyenye lakin tulisahau wale wanaoingia wangeweza nao kuchukua tabia hio, sasa tutafanya kweli, na tuna mifano ya kuiga kama kule Scandinavia, Sweden in particular.

But kwa nini unamuuliza yeye kama Slaa, vizuri umeelekezwa kwenye ilani ya Chama. Kazi hii ni yetu sote
 

Darwin, Soma sera za CHADEMA hapa:-

Sera, Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki za CHADEMA

Ukimaliza lete maswali au madukuduku yako.
Sera za CHADEMA nilikua sizijui kwani mimi nilikua sina ninaposhikilia popote, sasa nimezisoma zinavutia.

Wengine walitaka nisimuulize Dr Slaa niulize CHADEMA

CHADEMA swali lingine ni hili;

Wako baadhi ya viongozi kwenye CCM ambao tunawajua niwachapa kazi na wanajali maslahi ya wananchi.

Je CHADEMA inaweza kuchukua kiongozi mwingine kutoka kwenye chama kingine kuunda Serikali nzuri? mfano Anne Kilango?
 
Back
Top Bottom