Dr. Slaa Hatatuangusha Watanzania

Dr. Slaa Hatatuangusha Watanzania

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,872
Imenichukua miezi 36, kujifunza ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo( chadema), nimejifunza mengi.

Tangu kuondoka kwa ward Kabour aliyekuwa katibu Mkuu kutokea kigoma na nafasi yake kushikwa na mtaalamu wa sheria,na falsafa ya theolojia,Dr wilbroad Slaa,nimeona hakika kiongozi huyu ni wa kutukuka.

Kuonesha kuwa amefanya kazi kubwa pale alipofanya yafuatayo:

KUIMARISHA TAASISI ZA CHAMA

Alianza na kuwajengea uwezo watumishi wa makao makuu katika nyanja ya kitaalamu na kitaaluma,akawapa nafasi kwenda nje kusoma,akaanzisha kurugenzi ya sheria,kurugenzi ya habari,kurugenzi ya ulinzi na usalama,kurugenzi ya fedha,na kurugenzi nyingine nyingi ambazo zimeiweka chadema kuwa taasisi.

Usishangae unapoona timu ya Tundu Lissu,Tumaine Makene, Mohamed Mtoi,Lwakatare,na John Mrema ( kutaja wachache), ccm imepata kazi kweli kiasi cha kuishi wasiyoyatengeneza.kwa mujibu wa katiba ya chama aliitekeleza


KUUNDA TAASISI

Baada ya kazi hiyo,alianza kujenga taasisi za Bawacha,Bavicha,Chaso na Baraza la wazee..

Hii ilikuwa kazi yake aliyopewa na wanachama wa chadema.amefanya kazi kubwa sana.

Bawacha ambaye ilikuwa na wanachama laki tano 2000,imepelekea kuwa na wanachama milioni tatu nchi nzima.2015

Baraza la vijana,Bavicha kutoka wanachama laki mbili,2000, kwa sasa wanachama wamefikia milioni moja. Na si kuongezeka kwa idadi tu,bali pia mabaraza haya yapo ngazi za chini kabisa ya tawi nchi nzima,huwezi kwenda Itungu,Ikungi,mahaha,longido,kyaka,matemanga,nyamagoto, Misenyi,Madabank usikute ofisi za bawacha na bavicha.

Haikutosha akishirikiana na Mh.Mbowe,na timu yake,waliona chama bila wasomi, akaunda chaso ambaye kusema kweli limekuwa zao la vijana wabunge akina Kafulila,Zitto kabwe, Halima Mdee,Mnyika na wengineo wengi wanaotarajiwa kuwatumikia watanzania kupitia Udiwani na Ubunge Mwaka huu 2015.

Baraza la wazee amelifanikisha kuliimarisha likikishauri chama kwa kiasi kikubwa.
Dr.Slaa akiamini nidhamu,uvumilivu,utu,kiasi na umoja ndio njia ya kujenga Taifa lenye Usawa,na uchapakazi alishauri chama kuwa mwaka 2013 kisingefanya uchaguzi bali kiende ngazi ya kata,tawi na kisha msingi.Uchaguzi wa serikali za mitaa umeonesha matunda ya ushauri wake.kwani chadema imeshinda kwa kishindo kuliko wanavyojinasibu ccm kuwa ushindi mdigo,maana yapo maeneo ambapo tangu uhuru 1961 ccm imekuwa ukitawala vijiji,vitongoji na mitaa,lakini safari hii maeneo hayo yameenda na chadema yote.

Watu makini,kwa kazi makini,hakika Dr.Slaa ni mtu makini asiyeyumba kwenye kusimamia kanuni,katiba sheria na taratibu. Kiongozi ambaye ni very strategic katika mipango yake.
Inaonesha,katika mahojiiano binafsi niliyofanya na watumishi wa serikali ya Tanzania,wanamuona kama kiongozi wa kupigiwa mfano ameijenga chadema viliyo kutoka falsafa ya mtu,kwenda falsafa ya kitaasisi.

Si ajabu unapoongea na watu kupitia mitandao ya kijamii nje na ndani ya nchi, kwenye twitter,facebook,jamiiforum na sciber utakuta wanasema" Dr Slaa ni hazina ya watanzania,
Na hata angepewa nchi hatawaangusha watanzania"

Chadema Kwanza
 
mkuu umenena vema Sana Dr slaa ni hazina tuliyopewa na Mungu
 
CCM wanalitambua hili,
wewe waache waendelee kuzunguka na mafisi kama wao walivyo mafisi
 
Kamanda hivi UKAWA wasipomchagua Dr.Slaa mtavunja huo umoja wenu wa maghumashi?

Ritz
endelea kuwa kama fisi anayesubiri mkono wa binadamu udondoke.Ndio hivyo nchi tunaichukua.Jifunze.kusoma alama za nyakati
 
Dr slaa na mh mbowe
wamefanya makubwa sana kukijenga chama cha chadema jambo la kuwasifia sana ijapo kuna watu wanadhani kuwa kuendesha vyama vya upinzani ni kama kuanzisha saccos wakae wakijua kuendesha vyama vya upinzani ni kazi kubwa na ni ngumu sana kwa mafanikio waliyoyapata sio haba katika kuleta mabadiliko ya taifa hili
 
Uzuri wa Pro-Chadema mwenzao yeyote akija na pumba kama zinawafurahisha uwa hawezi kuhoji zaidi ya kishangilia tu bila kutimia akili zao.

Huyu mleta mada anawadanganya wenzake kuwa Bavicha na Bawacha wana wanachama milioni 4.

Ukiangalia uchaguzi mkuu ulioshapita Dr.Slaa alipata kura milioni 2 tu Tanzania.
 
Dr slaa ni mtu makini mno hata ukifatilia utendaji wake wakati akiwa katibu mkuu TEC,inasemekana hakuna kiongozi km slaa aliewahitokea TEC
 
Uzuri wa Pro-Chadema mwenzao yeyote akija na pumba kama zinawafurahisha uwa hawezi
kuhoji zaidi ya
kishangilia tu
bila kutimia akili zao.

Huyu mleta mada anawadanganya wenzake kuwa
Bavicha na
Bakwata wana
wanachama
milioni 4.
Ukiangalia uchaguzi mkuu ulioshapita Dr Slaa alipata
kura milioni 2 tu Tanzania.

Mkuu mbona umeandika kama vile umepakata Kinana bariidi halafu mkono mwingine ile sigara nene!?

BAKWATA inaingiaje tena
hapa!?

Anyway,ktk hizo milioni 2 umejumlisha na mlizochakachua!?
Halafu tumia hata akili kidogo pia,toka 2010 hadi sasa ni miaka mingapi imepita!?
 
Kama jamaa hana hoja anyamaze na asichangie anajidihihirisha kuwa ni mkaukiwa hoja
 
Back
Top Bottom