Dr. Slaa, Dr. Kabourou, Zitto Kabwe, ni waasisi wa mageuzi akina Lissu, Mnyika kuleni jasho lao

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
:A S shade:Dr Wilbrod Slaa aliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge mwaka 1995 baada ya kustaafu upadre akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi kupitia tiketi ya CCM na alishinda katika kura za maoni za chama hicho. Vikao vya CCM vilipokutana Dodoma vikamuengua na kumweka tena mbunge anayemaliza muda wake, Patrick Qorro. Wananchi wa Karatu wakamuomba agombee ubunge kupitia chama kingine na ndipo Slaa alipambana na wagombea wa vyama vingine kama CCM, CUF, NCCR MAGEUZI, UDP na aliwashinda wote kwa kupata asilimia 52, akifuatiwa na mgombea wa CCM aliyepata asilimia 44.

Uchaguzi uliofuata, mwaka 2000, Slaa alishiriki na kupata ushindi mkubwa zaidi. Tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 Slaa aligombea kwa awamu ya tatu na kupata ushindi wa asilimia 50 dhidi ya asilimia 49 za Patrick Tsere wa CCM.

Katika CHADEMA amewahi kuwa makamu mwenyekiti kabla hajachaguliwa kuwa katibu mkuu katika mwaka ambao Freeman Mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti nao wameendelea kuongoza kwa pamoja hadi hivi sasa.

:A S 41:Tangu mwaka 1995 Dr Slaa amekijenga chama kwaani chama cha upinzani kilichokuwa maarufu kuliko vyote ilikuwa ni NCCR mageuzi, CHADEMA ilipata umaarufu baada ya Dr Slaa kuwa mjenzi wa hoja na kupambana na wabunge wa CCM waliokuwa 80%, Dr Slaa na Dr Warid Kabour ni wabunge wa kwanza wa CDM kuingia bungeni mwaka 1995. Dr Slaa alipata nguvu baada ya Zitto Kabwe kuingia bungeni hivyo wakasaidia kukijenga chama. Uwepo wa watu hawa wawili bungeni kulisaidia CHADEMA kupata umaarufu sana na kujipambanua kama chama chenye agenda ya kweli kuwakomboa watanzania.

Tunakumbuka baadhi ya hoja zilizotikisa nchini ni ile ya MEREMETA, MKATABA WA BUZWAGI, EPA NA NK. Hivyo huwezi kusema mafanikio ya CHADEMA bila kutambua mchango wa Dr. Slaa. Dr Warid Kabour na Zitto Kabwe. Wabunge hawa ndiyo wanaoujua chungu ya upinzani nchini, Zitto aliwahi kufungiwa kushiriki bunge kwa miezi kadhaa, Dr Slaa aliwahi kupigwa na kuvunjwa mkono wakati Dr Warid aman Kabour alipambana na CCM kwa kupigwa mabomu na fujo nyingi zisizo na kipimo, miaka ya 1995 wananchi na POLISI walikuwa bado na mtazamo hasi juu ya upinzani. Mfano mwaka 1995 jeshi la polisi lilipewa treni mbili za reli ya kati kwenda kufanya operesheni maalumu kupambana na CHADEMA kigoma mjini.

MNYIKA, LISU, LEMA NA WENGINE
Watajwa hapo juu ni matunda ya kazi nzuri ya akina Dr Slaa, Dr Kabour na Zitto, hoja zao za utetezi wa wanyonge ndizo ziliwafanya kujiunga na CHADEMA, wanachama hapo juu ndiyo wameingia bungeni kwa awamu ya kwanza. Pia huwezi kutaja mafanikio ya chama bila kuwataja Mwasisi wa chama mzee Edwin Mtei, Bob Makani-R.I.P, Chacha Wangwe –R.I.P na Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe.

UJIO WA LOWASA NA VIONGOZI WENGINE KUTOKA CCM.
Ni ukweli usiopingika kuwa ujio wa viongozi hawa hasa LOWASA ulikuwa ni mtaji kwa chama kwaani nyuma yao kuna wafuasi wengi. Lakini ilikuwa na mhimu kuangalia na kuheshimu mchango wa akina Dr Slaa. Kumbuka kama alivyokijenga chama lakini anaweza kukibomoa chama pia. Katika harakati za ukombozi ni mhimu sana kuheshimu majeraha ya wapigania uhuru. Ndiyo maana Mwl Julius Kambarage Nyerere R.I.P hakuwatupa wale waliomsaidia kutafuta uhuru. Kumbuka katika baraza lake la mawaziri la kwanza hata wale waliokuwa tofauti na mitazamo yake walipewa uongozi serikalini au ndani nya chama.

Katika hali ya kawaida mtu hawezi kuvuja jasho tena yuko tayari kuhatarisha maisha yake harafu mtu hata kabla hajawa mwanachama awe kiongozi mkuu kuliko waliokaa msituni wakipambana. Kwa miaka mingi akina Dr Slaa wamekuwa wakipambana na akina Lowasa ndani ya CCM, ghafra huyo waliokuwa wakipambana nae anakuja kuwa bosi wao, hapo kama mwanadamu ulitegemea nini? Hata kama ungekuwa wewe kwa hurka za kibinadamu huwezi kukubari.
 
Inaonekana nikawaida ya cdm wakipata mwanachama mpya wazamani hawamsamini Ndio maana cdm kiko kimasilahi zaidi. Hawa simamii msimamo yao walioanza nayo. Mda wowote wanabadilika
 
dhambi ya uwasi haitawaacha wote waliotaka kuiuza CDM .

hata abaki mmoja , lazima hii treni ifike Kigoma .
 
siku zote za maandamano mbowe alikuwaakijificha alikuwa anashawishi watu waandamane wanapigwa na polisi halafu yeye anaibukia kwenye mikutano na waandishi wa habari
 
Adui akikushinda ungana nae, sioni upinzani kwa sasa Ccm walichofanya ni kuwa na vyama viwili afu wanaNchi (wapigakula) waamue wao kama wageuze shilingi au waiache vile vile.
Kweli chama kikongwe ni mbinu sio miaka.
 
Kwa hiyo Dr Slaa anataka tusiichague Chadema na Ukawa.??
Binafsi sijamuelewa , naona analalamika tu kama wananchi tunavyolalamika.
Kiongozi maarufu na anayeheshima kama yeye angetoa suluhisho kwa kutueleza wananchi tumchague nani (au tuwachague kina nani?) ACT? UKAWA? au CCM ambayo kinadharia naona wanamtumia kuharibu vyama vikuu vya Upinzani .
 
Lissu na Mnyika wasubirie tuu maana wanakaribia kuwa wanafiki. hizi sio siasa bali ni biashara ndani ya siasa

Mwigamba alisema Chadema inawenyewe na kuwa baada ya Zito kufukuzwa kwa kuwa na nguvu na mvuto zaidi ya wenye Chadema atakayefuata ni Dr. Silaa..(Nimeambatanisha Source).

Swali ni kuwa baada ya Silaa ni nani atafuata.
Ukiangalia panga linauelekeo wa kumdondokea Mnyika au Lissu
 

Attachments

  • 1441274708056.jpg
    1441274708056.jpg
    75.5 KB · Views: 383
Back
Top Bottom