wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,550
Gazeti la MKAKATI la Aug 7-13/2015 lina ripoti kuwa umepanga kuzunguka nchi nzima kuhakikisha Lowassa haendi ikulu,eti hutakuwa ktk upande wowote wa chama na utatumia gharama zako,huu ni unafiki mkubwa,tayari hapa unataka ccm ishinde,waungwana tunajiuliza hivi tatizo ni Lowassa au tatizo ni ccm? Mbona hata wewe ulikatwa jina na ccm mwaka 1995 ndo ukakimbilia CDM? Kosa la Lowassa liko wapi? Si dhambi hata kidogo kutumia silaha ya adui ili kushinda vita,na ndo CDM tumefanya,kama wewe unasusa susa tu,Tanzania kwanza kabla ya yote,tunatambua umuhimu wako ndo maana tumekusihi sana urejee lakini bado umegoma basi tuachie nchi yetu maana wewe una mpango wa kwenda kuishi Roma Italy,tumekaribia kushinda vita halafu wewe unajitoa dk za mwisho kwa sababu ambazo hazina mashiko,kama Lowassa alikatwa jina kwa kuwa ni fisadi vp kuhusu kina Pinda,Bilal,Mwandosya,Jaji Ramadhani nao ni mafisadi au hawana maadili? Tunajua fika ni nani alipangwa kugombea ccm huyu John Alcohol alitokea kama zali la mentali tu,iacheni Tanzania.