Kwa mwigulu nchemba raisi anabidi afikirie tena uteuzi wa huyu bwana. Ni mtu mwenye kashfa nyingi; fumanizi la igunga, mabomu Arusha, kauli zake za matusi mara kwa mara anapochangia mada mbalimbali bungeni, kashfa ya ugaidi wa lwakatare. Yaani huyu bwana ana msururu wa kuhusishwa na mambo mengi machafu still rais anamteua kuwa naibu waziri. Kweli kwa JK kila kitu kinawezekana.
Mkuu investa.tz, ni bahati mbaya sana kwamba sisi wa-Tanganyika ni DHAIFU sana na JK alishaliona hilo hivyo hahitaji wala kutuchagulia "tusi"!!! Tutalalamika sana humu JF lakini hatutachukua hatua yoyote dhidi ya hizi dhihaka hizi! Pia upinzani nao ni DHAIFU kwani kwa uteuzi huu Upinzani ungekuwa makini ni "kete" ya kutosha kuiporomosha serikali kabla hata ya siku 100! Ushahidi wa kashfa & jinai za Mwigulu viko wazi, hivyo Dr. Slaa & Co. wasibaki kutupa kauli nyepesi nyepesi, wachukue hatua stahiki!!