DR.Slaa awabagua Watanzania.

DR.Slaa awabagua Watanzania.

Status
Not open for further replies.

tata mura

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2012
Posts
275
Reaction score
49
Nimesikitika sana kiongozi mtarajiwa kutoka Chadema , kutoa kauli ya kushabikia na kutetea maandamano yaliyofanywa na wananchi wa Mtwara. Nanukuu kauli yake; (Siyo kwamba nashabikia bali natete maslahi ya wananchi). Sasa niulize hivi kweli wanamtwara watakula Gas ama lazima tutegemeane wananchi wote kwa pamoja?. Au hajui kuwa kitovu cha Maendeleo ni Dar, kama sivyo mbona hajaenda kuishi Moshi, Mbeya, Mtwara na kwingineko akakimbilia Dar?.

Nafikiri hoja za wanasiasa lazima wafikilie zaidi kwa kulinganisha pande zote. Mimi nilifikiri wangeunga mkono na kubana bei ya umeme ishushwe mara moja kwa sababu umeme unapatikana kwa wingi ila wao wanashabikia kwa mgongo wa kujifanya wao ni wema kwa wananchi. Najua mwenye akili mgando kwa Chadema atauliza amebaguaje sasa! Kitendo cha kusema Gas ni mali ya Wanamtwara ni zaidi ya Ubaguzi. Je Mikoa mingine inayotegea huduma ya Umeme kutoka Dar. ifanyeje. Ni lazima tujue kuwa si wote wakushangiapo pindi unaonge ukajilizisha kuwa wamekukubali bali wapo wengine wanakuchukulia kama mwigizaji na mchekeshaji kama walivyo wengine.

Leo hii Chadema ukituhumiwa na wafuasi wa Dr. Slaa tu ujue kuna kutishiwa kufukuzwa kwenye Chama, basi kama ndivyo Chadema ni mungu watu. Kwani hata Mungu huombwa msamaha kwa imani na binadamu hujilizisha kuwa amemsamehe. Nirudi kwenye maada Madiwa wa Mwanza hadi sasa wamechonganishwa na Wananchi huku wengine wakiwachukulia kuwa wanafuata pesa tu kwenye vikao kwa kusaini na kutoka nje bila sababu kwa shinikizo la Dr. Slaa, huku wa ukanda wa Kusini wenyewe wanakumbwa na Kashifa kubwa kubwa mambo yao yanaisha kimya kimya. Mfano Madiwani wa Moshi waliokuwa wanalazimisha zipitishwe zaidi ya Million 200 waende kutalii Rwanda imekuwa kimya na hata wa hivi karibuni Karatu tumeishia kusikia Mbowe alienda kusuruhisha. Sijajua alienda kusuruhisha Ufisadi ama alienda kusuruhisha nini. Je unafikiri wananchi wa Ukanda wa Ziwa wanayachukulia haya matukio pamoja na Ukanda wa kusini?.

Huwezi kuhamasisha kiongozi asitambulike huku nawe ulisema humtambui Rais Kikwete hadi leo kimya sijui ulipoenda Ikulu ndo ulimtambua! Kama ndivyo ulipaswa uje utujulishe kuwa sasa unamtambua ili tusiendelee kubaguana na kunyoshea vidole kuwa wewe ccm ulituibia kura zetu. Nafikiri ni muda mwafaka kutatua matatizo yanayokabili halmashauri tuanzotawala kuliko kuwadanganya wananchi kuwa Chadema hakina matatizo kila uchwao na wakati tunatimuana. Je waweza kumpa mkeo talaka bila kutofautiana?. Kauli yaweza kujenga ama kubomoa ingawaje leo hili haliwezi kuonekana machoni kwa sababu watu wakimbilia madaraka kwa mgongo wa kumkandamiza mwananchi wa kipato cha chini.

Mwisho wafuasi toeni matusi lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kujenga nyumba moja kwa kila mjenzi kugombania fito na kuvutia upande wake tu.
 
wewe ndo mbaguzi, unataka maendeleo ya wakwere tu kwani wamakonde siyo watu, acha chuki binafsi kaka.
 
Watu wengine mnakurupuka hoja yako ni ipi hasa,be specific!
 
Kuna misukule humu ya cdm kila anachosema babu kwao sawa,sio kwamba hawaelewi ila kwao wao furaha yao inchi isitawalike, watashindwa kwanza wamalizane na ya ndani kwao.
 
ukishakosea hata herufi moja kunukuu kauli ya mtu utakua unapotosha watu..iyo nukuu umetia yako apo..
 
mtwara kunakaa kila kabila. hata kabila lako lipo huko. siku zote hatua inaanzia nyumbani kwako. kule nako kuna vijana wanataka akira so wawatengenezee hata kiwanda kimoja. hii itapunguza wimbi la vijana wanao tafuta ajira dar. mia
 
slaa anamifanyaa msipatee usingiziiii duuu dr tunakutakiaa safarii njemAAA KATIKAA SAFARIII HII YA MAJUNGUUU NA UNAFIKI WA WATZ WALIO WENGI WANAANGALIAA PESAA MBELEE KULIKOO FIKRAAA
 
Dr Slaa hajasema gesi iliyopo Mtwara ni ya wanamtwara, ila amesema wananchi wa Mtwara nao ni lazima wafaidike na gesi inayotoka mkoani kwao. Mbona makampuni ya madini yanayofanya uchimbaji mikoa ya Shinyanga na Arusha yanawaajiri wananchi wa maeneo hayo na kuchangia huduma za jamii? Sasa kama gesi itatolewa Mtwara bila taarifa yoyote ya ni vipi wananchi wa Mtwara watafaidi, itakuwa na faida gani kwao? Ukizingatia hata umeme unatumiwa na asilimia ndogo tu ya wanamtwara?
 
Kuna misukule humu ya cdm kila anachosema babu kwao sawa,sio kwamba hawaelewi ila kwao wao furaha yao inchi isitawalike, watashindwa kwanza wamalizane na ya ndani kwao.

bora kuwa msukule wa Dr. kuliko kuwa msukule wa Nape vuvuzela
 
Naona umeweka vitu vingi pamoja,hueleweki mkuu,sioni nichangie kipi na niache kipi, tulia usitumie jazba.
 
kuhusu swala la gas ya mtwara, yeyote anayewapinga wananchi wa mtwara kudai haki yao ni muuaji mkubwa.
sijasoma hii thread kwasababu unamtetea shetani.
 
Jaribu tena baadae huja convince mtu hapo. Karudie utungaji upya labda utafanikiwa!!!
Lengo si kukuconvice ila ni kukuelza uozo wa dr.slaa,kweli huyu babu yetu ana mapungfu mengi saana ila taratibu mkuu tutamshauri
Wengi humu wanaamin kuwa dr. Slaa hawez kukosea na ndo maana ikiletwa mada inayozungumzia uozo wake aslmia kubwa wanapinga.
 
kama vile kuna ukweli fulan: hiv aliwahi kuzungmza kwenye media yeyote kuwa anamtambua rais? hivi alipoenda ikulu alisema anaenda kumtembelea nan? hizi siasa za bongo zinaniumiza ni zaid ya uzijuavyo.
 
Ukiona unapost thread inashindwa hata kupewa shavu na wapambe wa magamba ujue umechemka
 
come what it may, the doctor is the greatest thinker. Hatulali mpaka kieleweke na mpaka magamba tuwaage.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom