Dr. Slaa awa gumzo ndani ya CCM

Dr. Slaa awa gumzo ndani ya CCM

Wa mmoja

Member
Joined
Aug 4, 2009
Posts
99
Reaction score
0
MGOMBEA urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amekuwa gumzo ndani ya CCM kiasi kwamba mwenyekiti wa chama hicho tawala, Jakaya Kikwete na katibu wake mkuu, Yusuf Makamba walishindwa kujizuia kutumia muda mrefu kumzungumzia, huku wakiwataka wana-CCM kutodharau changamoto iliyo mbele yao.

Dk Slaa, ambaye anaonekana kuwa alifanya kazi kubwa katika Bunge la Tisa, hakuwa akitajwa sana kugombea urais, lakini baada ya Chadema kufanikiwa kumshawishi aingie kwenye mbio za Ikulu, ameonekana kuongezeka umaarufu wa haraka na sasa Chadema inaonekana tishio kwa CCM.

Sasa mheshimiwa anazikumbuka kura za wafanyakazi aliokataa kuwapandishia mishahara,na kudai kuwa hata wasipompigia kura,hana shida na kura zao....Jeuri mbaya kweli,sasa inataka kumtokea puani,eti watanzania walimuelewa vibaya....Kazi kweli kweli!!!
 
Na mbado ataji JK kidogo sasa?Time will tell.Watakula mafi yao.:mad2:
 
Na mbado ataji JK kidogo sasa?Time will tell.Watakula mafi yao.:mad2:

Kwanza Karibu sana JF uwanja wa waungwana.
Hilo lazima awe Gumzo kabisa maana amegusa penyewe, na hata hivyo wanajua kuwa ndo rais anayetakiwa kwa sasa. Sema tu hawawezi sema kwa vile wanachama chao CCM
 
kwanza karibu sana jf uwanja wa waungwana.
Hilo lazima awe gumzo kabisa maana amegusa penyewe, na hata hivyo wanajua kuwa ndo rais anayetakiwa kwa sasa. Sema tu hawawezi sema kwa vile wanachama chao ccm
siku zote mwisho wa ubaya ni aibu na kikulacho ki nguoni.uso kwa uso jk+ufisadi+uswazi management+dr slaa+sizitaki kura zenu wafanyakazi=no prezident at all.
 
:confused2: hivi ccm wanadhani watanzania wote ni vilaza kama wao!! :mad2: eti watanzania wamemuelewa vibaya JK alipokuwa anaongea na wazee wa ccm pale diamond akawa anapigiwa na makofi na vigelegele alidhani watanzania wanacheza mdundiko! hiyo imekula kwake watanzania hasa wafanyakazi HAWADANGANYIKI
 
aaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhh........jk na makamba wanapanga mbinu mpya za kuiba kura...si ajabu pamija na slaa kuungwa mkono karibu na wananchi wemgi lakini jk akashindwa kwa vishindo vyoopoote yaani kimbunga, sunami,nk
 
Kazi ni kubwa mno kwa kwa CCM kwani nimeongea na wanachama wengi sana wa CCM na wamesema kura watampa Slaa!!!
 
:becky:"Always vote for principle, though you may vote alone, and you may cherish the sweetest reflection that your vote is never lost."~John Quincy Adams
 
Back
Top Bottom