Dr. Slaa atakuwa adui namba 4 kati ya maadui wa 3 wa Mwl Nyerere

mimi napata mashaka hivi uhu upenzi wa na usemewaji wa dr slaa, na ccm umetoka wapi?

Hembu tujiukize juu ya lile bandiko la dk slaa hapa (jf) akimjibu kamanda (yeriko nyerere)

embufikiri sana wanachadema wenzangu, kwa nini dr slaa hasiwajibu ccm na gazeti la Raia tanzania kwa kupiga propaganda juu yake? ihishie kumjibu mwana chadema mwenzake, bw yeriko!!!!!!!!!!!!!!!

Hapa kuna ishu inaendelea siyo bure.

Ifike maala wanachadema na viongozi wakuu wa chama waachane na dr slaa, dr slaa atapita na chama kitabaki tena imara zaidi na zaidi,

ila dr ajue ametukera sana tena sana maana ni mtu ambaye tulimweshimu sana,

ahache chuki zisizo na maana yoyote kwa lowassa, chuki hazijengi maana binadamu siye muhukum bali ahukumuye kwa haki ni MUNGU,
 
Wakati Dr Slaa anahamia CHADEMA,CHADEMA hakikuwa kikubwa na maarufu kuvizidi vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi.Ni Dr Slaa na Zitto ndio walioifikisha CHADEMA hapa ilipo kiasi cha kila mtu kuiongelea na kuitamani,angalia malipo wanayoyapata wanasiasa hawa wawili,ni matusi na lugha za kejeli.Lowassa anahamia CHADEMA kikiwa kimeishaimarika tayari,kama anakubalika hivyo kwanini hakwenda ACT akaimarishe kama alivyofanya Dr Slaa.Dr Slaa angeweza kwenda NCCR au CUF ambavyo vilikuwa na nguvu tayari,akachagua kujiunga na CHADEMA chama ambacho kilikuwa bado kichanga wakati huo.
 
Yaani nashindwa kuelewa wafuasi wa Chadema sijui wenzetu ubongo wao una mafuta ya taa au ni wa ndege maana hawakawii kusahau.Leo mnamtukana slaa kisa lowasa.nawafananisha na mwanke anaesaliti ndoa yake kisa kapewa sh 10000/=ya Mara moja na kusahau Huduma za mumewe za kila siku.

Mkuu sababu iliyowafanya wasiwe na Akili wana Chadema ni hii hapa, Angalia FISADI Anavyogawa MAPESA,

http://youtu.be/Q5Kf7Y6vt9w
 
Dah! Slaa Kaamua kutokusaliti anachokiamini kwa kujitenga na Maamuzi ya Mbowe na Mtei aliyeleta Jina la Lowassa kupitishwa kuwa Mgombea Urais siku 4 kabla hajahama Ccm kwenye Kamati Kuu ya Chadema ili iridhiwe, Slaa hajatukana mtu wala kushutumu yeye Kaamua kujitenga nayo kwan tatizo nn
 
Kwamba amekataa kupokea fedha za fisadi Lowasa au Dr. Slaa hanunuliki mkuu usipoteze muda

Fedha huleta usaliti,Hii picha ukiitazama kwa jicho la ndani Dr anaweza kuwa kashapokea kitu kutoka Ccm
Na ndio maana wanaCcm wanamwona ni mtu hodari kwa sasa wakisahau vita waliyompiga siku za nyuma
Siasa za ccm ni nyepesi sana,Na kwa karne hii hazina mashiko wala nafasi tena.
 
Nashindwa kuelewa hulka zetu sisi binadamu, tunapenda tu watu wafanye tunayotaka sie
Dr. Slaa kuwa katibu wa chama hakumnyimi haki ya kupinga chochote asichokiafiki kwenye chama, bado ana haki ya kusimamia misingi, misimamo na falsafa anazoziamini, sio kila mtu ni cheap kiasi cha kuweza kula matapishi yake
Lowasa kaja yeye kaona haafiki na hawezi kufanya nae kazi kaamua kupisha wengine wafanye, na anafanya haya bila kuchafua chama wala kuhama chama, sasa tatizo linatoka wapi mpaka wewe umfanye adui yako, sasa kila utakae tofautiana fikra uki mbrand ni adui uta brand wangapi!
Katika malezi niliyopitia mimi binafsi principle ni kitu cha msingi na chakufia, mtu akifanya jambo jema kwa kuvunja principal tuna tambua hiyo kazi njema pamoja na kumuwajibisha kwa kuvunja principles.
Mwacheni Dr Slaa afanye maamuzi yake na pia maamuzi hayo tuyaheshimu kwa sababu ni haki yake
 
Naungana na Wanachadema wenye mapenzi mema na nchi yetu kumwomba DR.Slaa aliyekijenga CDM kwa muda mwingi na hatimaye ikapata heshima na kuaminiwa na Watz, Dr jitokeze hadharani utuambie UKWELI, Ninalaani wale wote waliomtukana na kumkejeli Dr Slaa

Sasa Dr. Slaa toka hadharani sema hukupenda nini katika ujio wa Lowasa, sisi wanamageuzi tujue tutapima wenyewe. Kama yale tuliyokuwa tunayakemea yameingia kwetu sema,
 
Ukitoa wale maadui watatu aliowasema Mwl Nyerere yaani Ujinga,Maradhi na umasikini adui namba nne ni Ufisadi Dr.W.Slaa na Chadema kwa ujumla ndio waliokuwa mstari wa mbele kupambana na huyu adui namba nne na moja ya watu aliokuwa akipambana nao kama kinara wa ufisadi ni EL leo kaingia chadema ndani ya siku tatu kapewa nafasi ya kugombea uraisi haya ni matusi mazito kwa Dr Slaa.

Angalau basi angekaribishwa tu akawa mwanachama wa kawaida eti wanampa kabisa nafasi ya kugombea uraisi?? kuna watu hapa watasema aaahh mbona watu wanatubu na wanasamehewa! ni kweli lakini ukiungama unaendelea tu kuwa muumini wa kawaida na siyo kuutaka tena Upadri/uchungaji

Kuna watu wanasema eti akiwa raisi hawezi kuwa fisadi kwa sababu chama kitamdhibiti kwelii??? Yaani mtu mmkabidhi Usalama wa taifa, JWTZ,Magereza,Polisi na kila kitu wewe ubakie na Kamati kuu,Halimashauri kuu na Mkutano mkuu halafu utegemee kumdhibiti mtu kama huyo mnatania nyie.
 
Last edited by a moderator:
yeye alipokelewa vilevile akapewa nafas ya juu na bado akapata fursa ya kupeperusha bendera ya chadema 2010..sasa tatizo liko wap lowasa akipewa..basi tuache kupokea wanachama wapya kama ndo kususa kiivyo..siamini ka lisemwalo lipo kwel Dr???
 
Dr Slaa hakuzaliwa wala kukulia Chadema.Naye alikaribishwa kama mwenzie lowassa Na hakuna aliyepinga kupokelewa kwake hata kidogo.Chadema walienda mbali zaidi na kumpa dhamana ya kuwa Katibu mkuu wa chama.

Nikiwa kama mwanachama hai wa Chadema niliyezaliwa na kukulia ndani ya chama hiki,Nasema"Endapo Dr slaa atakigeuka chama wakati huu mzuri tukiwa tunahitaji mabadiliko na fikra mpya.Atakuwa ndio adui wangu namba moja wa siasa za mabadiliko tanzania tunazozililia kwa miaka 20 sasa.

Dr Slaa ni nani hata apingane na wengi,Tena kamati kuu ya chama?

Dr Slaa ni nani apingane na nguvu kubwa ya mabadiliko na ukombozi wa kiuchumi?

Bila shaka nipo tayari kuamini ipo nguvu kubwa toka chama tawala inayomshawishi Dr kufanya haya kwa masilahi yake na yao binafsi.Na si wengine ni Ccm,Baada ya muungano wa Ukawa walikosa usingizi na sasa rasilimali zao zote zikiwemo rasilimali fedha na watu wameziamishia kwa Dr ilimradi tu ndoto hizi njema zisitime.

Sipo tayari na naomba wana Chadema wote tuungane kwa hili.

Na kama Dr atatusaliti tumwainishe katika maadui wakubwa kati ya wale maadui aliowataja mwalimu Nyerere.

Maradhi,Ujinga na Umasikini adui wa nne tutamwongeza Dr Slaa asiposikia vilio vya wapenda mabadiliko.

Hii ni kazi ya lumumba na ya kupuuzwa, wanajua Dr. anaingia humu JF. Kwa taarifa tuu IQ ya Dr. iko juu na nina hakika keshagundua kuwa hii ni janja ya kumgombanisha na makamanda wenzake ndani ya CDM.
 
mkuu dr. slaa...piga moyo konde
njoo tumalizie mbio hizi kwani
twakaribia ukingoni.
 
Mimi majibu ya Lowasa kuhusu tuhuma zake za ufisadi popote anapozisema nakua sipati majibu mazuri na kumwelewa,dr slaa hakutoka ccm na kashifa kama za Lowasa,mimi kwa mtazamo wangu nahisi mzee hajaridhika na majibu ya mwanachama mpya Edward ndo akamua bora apumzike.
 
Hizi mada za Dr daa kila saa kila wakati mnalipwa shilingi ngapi maana mnajuhudi. Niwapongeze maana bila kumwandika mkono hauendi kinywani japo nikitambo tu daa itakula kwenu. Ushauri mfikilie mwingine mbadala mwa kumzushia uongo ili msife njaa.
 
Dr. Slaa siyo mtu wa unafiki, alichokisema jana ndicho hicho hicho atakachokisema kesho na kuendelea, kwa sasa mtamtukana sana lakini historia imeshaandikwa tayari kuwa Dr Slaa huwa anasimamia alichokisema

Hata mimi nakubali,dr huwa harudi nyuma, akiamua ameamua, mfano akiamua kuchukua mke wa mtu harudi nyuma, atamchukua tu na harudi nyuma. Hata akiwa rais akiamua kuchukua wake zetu atawachukua ti,hakuna ujanja.
 
sasa ni dhahiri chadema wanataka kwenda kufanya biashara ikulu. waepukwe kama ukoma. mbowe baba mkwe et al wamemtumia slaa na vijana zitto etc ili kushika ikulu kumbe ili kwenda kuigeuza pango la walanguzi.
 
Fedha huleta usaliti,Hii picha ukiitazama kwa jicho la ndani Dr anaweza kuwa kashapokea kitu kutoka Ccm
Na ndio maana wanaCcm wanamwona ni mtu hodari kwa sasa wakisahau vita waliyompiga siku za nyuma
Siasa za ccm ni nyepesi sana,Na kwa karne hii hazina mashiko wala nafasi tena.

Kibo10. Kuna mawazo mchanganyiko hapa na wenye hekima wataamua kwa uhalisia. Kuna baadhi ya vyombo visivyoaminika vinasema mwenyekiti wenu kanunuliwa, na hilo ulotaka kusema wewe kwamba Dr Slaa huenda kapewa kitu na ccm sintaliamini.

Kwa kuwa Dr. Slaa yupo naamini si muda mrefu ujao tutajua ukweli wa mambo haya. Hekima pia ni kunyamaza kuliko kumshambulia mtu with no evidence.
 
Mshamuita msaliti kama ilivyokuwa kwa zzk!Chama cha familia hiki Mbowe, Mtei na Ndesamburo nini ukimuita adui!Atajulikana adui wa kweli mwaka huu
 
Back
Top Bottom