Dr. Slaa Apokewa Kifalme Nchini Marekani !

Dr. Slaa Apokewa Kifalme Nchini Marekani !

Rtackket

Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
74
Reaction score
373
Ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kiafrika kupewa mapokezi makubwa ambayo Dr. Slaa ameyapokea katika ufunguzi wa mchezo wa mpira maarufu kama football. Dr. Slaa alialikwa na Chancellor pamoja na Rais wa chuo kikuu cha Alabama kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo baina ya Alabama na Georgia State. Kiongozi huyo wa Chadema alipokewa na viongozi wa ngazi mbali mbali wa kitaifa na wa jimbo la Alabama

Akimkaribisha Dr. Slaa katika chakula cha asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake, Chancellor wa chuo hicho, amemfananisha Dr. Slaa na Nelson Mandela kutokana na juhudi zake za kupambana ufisadi nchini Tanzania. “
Tunajua jinsi polisi wanavyowaua raia na kuwakamata wapinzani” alisema kiongozi huyo. Kadhalika kiongozi huyo amemsifu Dr. Slaa kutokana na msimamo wake, sera zake za kulikomboa Tanzania kutoka katika umasikini licha ya chama chake kutungiwa kesi za ughaidi.

Kwa upande wake, wakiwa kama moja ya vyuo vikuu nchini marekani, wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Dr. Slaa hasa katika sekta ya elimu. Wamemuomba ajisikie nyumbani na kufurahia mchezo wa American football.
Kwa unyenyekevu Dr. Slaa aliwashukuru governor, na viongozi wengine kwa kuwa wakarimu sana kwake na mkewe na watu wa Tanzania. Amefurahishwa jinsi wamarekani wanavyokuwa na hamasa na kuipa kipaumbele michezo.

Nimejifunza kwamba michezo ni moja ya mbinu ya kuiunganisha taifa hasa tunapokuwa na changamoto nyingi kama za kwetu alisema Dr. Slaa. Kadhalika amesema kwamba, chama chake cha Chadema ina sera ya kukuza vipaji kupitia taasisi za michezo nchini Tanzania na siyo kuwaleta Makocha wa kigeni, mmoja baada ya mwingine na kuwapeleka Ikulu kula pilau na kupiga picha.

Nilichojifunza ni kwamba, lazima nirudi na ujumbe kwa watanzania kuweka mifumo endelevu ya michezo kuanzia shule za misingi hadi vyuoni. Nilichoona hapa ni mfano wa kuigwa alimalizia Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa na Mkewe wakilakiwa na Rais wa Chuo
attachment.php

Moja wa mamea mashuhuri marekani akimsalimia Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa akikaribishwa Ukumbuni kwenye Chakula cha Asubuhi iliyoandaliwa kwa ajili yake
attachment.php

Moja ya Viongozi wa Juu Nchini Marekani
attachment.php

Dr. Slaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi ya Masenators walioalikwa kujumuika naye
attachment.php

Watoto nao walijitokeza kumsalimia na kupiga picha na mgeni mashuhuri Dr. Slaa
attachment.php

Watu wengi mashuhuri walioalikwa walimiminika kusalimiana na Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa na Senator Shelby wakibadilishana mawazo wakielekea uwanjani
attachment.php

Msafara wa Dr. Slaa ukiwasili uwanjani
attachment.php

Watu wa kila aina mashuhuri walifika kumsalimia Dr. Slaa
attachment.php

Dr. Slaa na Gavana
attachment.php

Dr. Slaa akisalimiwa na mmoja wa US congressmen waliohudhuria mchezo
attachment.php

Mshindi wa Nobel Peace Price na Dr. Slaa ndani ya Chumba cha watu mashuhuri wakijadili neno
attachment.php

Viongozi Mashuhuri wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza. Dr. Slaa ndiye mgeni Rasmi. Hapa ni chumba maalum cha rais kwa ajili ya wageni mashuhuri
attachment.php

Uwanja ulijaa hasa. Watu zaidi ya laki moja walihudhuria
attachment.php


wakiwa katika chumba cha watu mashuhuri. Baadhi ya watu mahuhuri kama yeye hawakujizuia kwenda kumsalimia. Akifungua mchezo wa leo, Dr. Slaa alirushwa moja kwa moja na moja ya luninga kubwa zaidi nchini marekani​
 
Ndo wananchi wanataka viongozi si watawala ambao hawajui umaskini unatokana na nini!
 
Hizi ni dalili njema kwa watanzania kuwa na kiongozi wa chama anaekubalika kimataifa, na ukiona hata wazungu wamekubali ujue uwezo wa huyo mtu ni wa hali ya juu kila laheri Dr. W.P Slaa
 
MUNGU pamoja nawe Dr Slaa....!
 
waambie masisiemu yanaujali mpira wa miguu tu. tukichukua nchi tutajaribu na mchezo huo
 
Dr. Slaa kafunika Mwigulu amebaki kuwa dagaa.
 
Kumbe Slaa anaota ufalme! Ndio maana Josephine anajiona yuko above the law!!!
 
aisee nilikuwa sina appetite ya chakula sasa naenda kula, ipo siku hatutarudi nyumba kwa mabomu ya machozi na siraha za moto tutasonga mbele, Martin Luther king, MalcomX, Bob Marley etc
 
Back
Top Bottom