Dr Slaa Apewe Ulinzi

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Nikiwa nimeshtushwa sana na Ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika benki kuu, na kwa kuwa shutuma zilizopelekea uchunguzi kufanyika zilitoka kwa mbunge Mh dr Slaa,basi mimi nina wasiwasi sana na watu wasioutakia mema uchunguzi huu kuweza kufanya mambo ya kuuzima ama kulipiza kisasi, kwa hiyo mimi ninapendekeza/kuiomba serikali itoe ulinzi wa kutosha kwa mheshimiwa DR Slaa. historia imetufundisha mengi na kwa hiyo hatuna haja ya kutokuchukua hatua mathubuti kwalinda wana wenye uzalendo wa kweli na nchi yetu.
 
Nafikiri watu wa kumpa ulinzi wawe ni WTZ kwa ujumla wao wakisaidiwa na kikosi kidogo cha mabodigadi kwa sababu huko serikalini wamejaa mafisadi na hata hao wanaoweza kupewa kazi hiyo ndio wakammaliza.
 
Ni kweli kabisa CHADEMA inbidi wampe W.Slaa ulinzi wa hali ya juu maana mafisadi wanaweza kukodisha majangili ili wachukue uhai wake. Tumeona juzi jinsi waandishi wa Mwanahalisi walivyotaka kutolewa roho kwa kuandika habari mbali mbali za mafisadi.
 
Lakini Chadema kuna watalaamu wa Ulinzi? kama Wapo wampe kama hawapo serikali ndio kazi yake; ndio maana tunatoa kodi; kama mzee wa Kaya anajua umhimu wa huyu bwana lazima awe na utashi na usalama wa Dr Slaa ili alipue mabomu mengine, najua wanamuwinda mafisadi kwa sasa; hawajapenda
 
Alishasema Bungeni kuwa usalama wake uko mashakani na bado wakubwa wakakaa kimya.Nafikiri ni muda muafaka sasa kwake kuomba ulinzi.Ni haki ya kila raia kupewa ulinzi hata CP.Kuna vigezo vyake na Dr.Slaa amevifuzu vyote.
Namkubali sana Slaa.
 
Hili ni suala la msingi sana, ili huko mbeleni waweze kujitokeza watu wa kuwashughulikia mafisadi/waharibifu bila hofu ya kudhuriwa nao,Serikali isipuuze hata kidogo,ulinzi kwa mheshimiwa Slaa ni jambo la muhimu sana.
 
Ni-kweli mkuu maana yaliotokea kwa wazlendo wenzetu wa-mwanahalisi gazeti.....yanatisha ulinzi ni muhimu kwake.
 
Pamoja na ulinzi kwa mhe. huyu, watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kwa maandamano ya amani, kuzidi kumpa nguvu na imani zaidi.
 
Pamoja na ulinzi kwa mhe. huyu, watanzania tunatakiwa kumuunga mkono kwa maandamano ya amani, kuzidi kumpa nguvu na imani zaidi.

Hilo ni kweli,
Lakini je Tibaigana atatuacha? make naona siku hizi yeye kazi yake ni kusambaza FFU ili yasiwepo maandamano hasa ya vyama mbadala!
 
Apewe ulinzi!Tena wa kutosha!Tusisahahu waandishi wa habari wenyewe maisha yao yako hatarini..na Kikwete alienda pale hospital na kuwaambia waandishi wawe makini?mhn?watakimbili wapi kama topu mwenyewe anawaambia kila mtu kivyake?Wapinzani wasipoitoa CCM madarakani wakati huu wa ufisadi nje nje then siju lini itakuwa possible!
 
Hilo ni kweli,
Lakini je Tibaigana atatuacha? make naona siku hizi yeye kazi yake ni kusambaza FFU ili yasiwepo maandamano hasa ya vyama mbadala!
This time ni lazima wananchi wawe organized wafanye mabadiliko!Lakini upinzani bado wana kazi kubwa kwani katiba yenyewe bado hata haijabadilishwa!
 
Back
Top Bottom