Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama
hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia
masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho
hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea
busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya
kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha
uwakilishi wa wananchi.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara jana katika maeneo ya Ngalangala,
Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba
ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima
wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. Moja
ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano
wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi
wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si
vinginevyo.
Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye
Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa
utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia
mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze
nini kisemwe. Hakuna, alisema Dk. Slaa. Alisema kuwa baada ya
mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja
kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata
moja.
Source:Nipashe Jumanne.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.
Akizungumza katika mikutano ya hadhara jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.
Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna, alisema Dk. Slaa. Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.
Source:Nipashe Jumanne.
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.