Dr Slaa ampigia mbuzi Gitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa ampigia mbuzi Gitaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Dec 29, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimesoma kwa makini majibu ya Dr Slaa kwa mwandishi Mayage S. Mayage mpaka jana kwenye Gazeti la Raia Mwema, kwa kweli Dr Slaa amemjibu kwa weledi mkubwa tofauti na mimi nilivyofanya huko nyuma kwa kweli nampongeza kwa kazi kubwa anayoifanyia CHADEMA na nchi kwa ujumla wake.

  Binafsi mimi nilimshauri asihangaike kuwajibu watu wa aina ya Mayage kwa kuwa hawa wanakazi maalumu waliopewa na mabwana zao lakini baada ya kusoma makala za majibu ya Dr Slaa nadhani kuna haja ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa aina ile hata kama ni ya mtu mjinga kama Mayage S.Mayage.

  Pia namshauri Dr Slaa asikate tamaa kwa kuwa hoja yako kwa bwana Mayage ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, kama hamuaminii subiri majibu ya huyu bwana huko tuendako.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Acha Mayage apate malipo yake ya upotoshaji kwa umma.
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  weka hayo majibu ya dr.slaa basi
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  kwa kweli nimefurahi sana.Makala za PHD zimenifumbua macho sana.Kuna mambo nilikuwa siyajui.Hongera sana PHD Slaa
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  soma makala za raia mwema za wiki 3 mfululizo
   
 6. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mayage ni nani kwanza?na dr kamjibu nini?ufafanuzi tafadhali,
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mnafiki mkubwa huyu aliyesababisha magazeti ya RAI yachukiwe sana kwa kukumbatia mafisadi.Mtu anayejaribu kuua soko la gazeti la RAIA MWEMA kwa makala zake za kukumbatia mafisadi na kumshambulia yeyote anayepigama vita dhidi ya ufisadi
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  google Raia Mwema
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  kupitia majibu ya Mayage nimejifunza mengi mengi sana ambayo CDM inafanya; tupo wengi tu (kina Mayage) hatujui kwa kina ni yapi CDM inafanya; yapi yamefanikiwa kwa kiwango kipi na je challenges zipi chama kinakumbana nazo; wengi tunajua ya Udiwani Arusha na hili la mropokaji Shibuda; pamoja na suala la POSHO, ila yale ya ndani hasa mipango ya maendeleo na namna ya mkakati wa CHAMA hatujui; namna CHAMA kinavyoongoza halmashauri zake na baadhi ya kata hatujui.

  Kwa mfano nimejifunza kumbe CDM wako tofauti kimkakati na vyama vingine katika kufungua office ya chama (matawi) kila kitongoji nchini; ni mengi tu tumejifunza. Nakuomba DR. kila ukipata fursa naomba uwe unakuandikia ili kupate kujua mengi yaliyomo ndani ya CDM; sisi si wavivu wa kufikiria kama Mayage kwa kukimbilia kutoa tamati bila tafiti la hasha- tunahitaji kujifunza mengi toka makala zako hasa unapowajibu watu kama hao wanaotaka kupotosha umma kwa ujira kiduchu.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  huwa sinunui ili gazeti 7bu Alhaji Membe kashalitia mfukoni. Mnaobisha msiwe na hara mtanielewa muda unavyozidi kuyoyoma
   
 11. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  FUSO,
  Asante kwa kuongeza idadi ya Mashahidi wangu kwa hoja iliyopingwa sana nilipoandika Udhaifu wa Kitengo cha Habari na Uenezi ndani ya CDM. Naomba nisisitize tena na tena; Erasto Tumbo anapwaya sana katika Kurugenzii hii. Hivi kwa nini hawataki kusikia wala kuukubali UKWELI?
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu google utapata makala zake
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  nadhani Erasto Tumbo apangiwe kazi nyingine.Idara hii anatakiwa apangiwe kijana mchapakazi mtaalam wa social media nk. Wapo wengi wanaoweza hii kazi mfano Regia Mtema, Joshua Nassary nk
   
 14. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sio wote wananunulika. Unatumia vigezo gani kusema wamenunuliwa, una ushahidi? Kama Mh. Membe kutokeza mara kadhaa na habari nzuri katika gazeti hilo ndo kununuliwa basi Dr. Slaa atakuwa kawalipa zaidi.
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  mi siko huko mnakotaka kupeleka mada, point ni kwamba kama Mayange angetaka kufanya utafiti kwanza kabla yakuandika makala yake ya kuishutumu CDM ndani ya jamii kama si chama cha kuwavusha watanzania angepata hizi info. na hata hivyo Dr. katusaidia sisi wananchi wa kawaida kujua mengi kuhusu CDM. Hayo mengine ya idara ya habari mimi siyajui nafikiri DR. anaweza kuyafafanua endapo tutamwomba.

  Point yangu ipo pale pale nimejifunza mengi kupitia makala hiyo ambayo nilitamani DR. awe anaandika katika kila toleo la gazeti hili kama ingewezekena kutolea ufafanuzi wa mengi ambayo wananchi wanapotoshwa.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kila mtu anajitahidi kuutafta umaarufu
   
 17. J

  Joblube JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa yako sina umaarufu wowote, na sijulikani popote nnchi hii
   
Loading...