Dr. Slaa ni mjamaa, gumzo kuhusu anavyoishi Canada linathibitisha ujamaa wake

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Jana na leo kwenye gazeti la Mtanzania kuna habari kumhusu Dr Slaa na anavyoishi akiwa ughaibuni.

Inasemwa, kuwa kuna wenye kumshangaa Dr Slaa kufanya kazi ikiwamo ya kwenye duka kubwa huko aliko.

Dr Slaa kupitia majibu yake kwa mwanahabari wa gazeti hilo ameweza kuweka wazi umuhimu wa kazi na kuthamini kazi. Umuhimu wa kujitegemea na kusimamia kanuni zinazokuongoza mwanadamu katika maisha.

Ameliona pia tatizo kubwa tulilo nalo sasa na kutaadharisha tabia ya Watanzania kutafuta njia za mkato kwenye kupata mafanikio.

Amenukuliwa akisema; " Kila mara nimekuwa nikiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi, kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mitandao wala propaganda."

Dr Slaa huko aliko ajue tu, siku hizi huku nyumbani vijana wamejikita pia kwenye kucheza kamari/ kubeti na kuigeuza kuwa ndio ajira.

Dr Slaa aliachana na siasa za vyama Julai 28, 2015 kwa madai ya kuona misingi ya chama alichoshiriki kukijenga imepotoshwa. Ni pale CHADEMA ilipomkaribisha Mheshimiwa Edward Lowassa. Dr Slaa aliweka sharti akiitaka Chadema imtake Lowassa kujisafisha kwanza dhidi ya tuhuma ya kashfa ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Nakumbuka nilimsikiliza Dr Slaa akiongea na Taifa akitangaza rasmi kuachana na siasa. Nikaandika, kuwa binafsi naamini Dr Slaa hajaachana na siasa, bali siasa za vyama.

Kwamba siku zote, kiongozi makini ni yule anayejijua na kuujua wakati unaomzunguka. Nikampongeza ndugu yangu Dr Slaa kwa maamuzi yake yaliyotokana na kusukumwa na dhamira yake. Mchango wake kwa ustawi wa nchi yetu utaendelea kuhitajika.

Nilivyokutana kwa mara ya kwanza na Dr Slaa..

Juni , 2004, nilitambulishwa mara ya kwanza kwa Dr Slaa na ndugu yangu na Mjamaa mwenzangu, Zitto Kabwe. Nikiwa ofisini kwake pale Mtaa Togo, Ndugu yangu Zitto alinishawishi sana nijiunge na Chadema, nikamwambia, asihangaike sana, hilo haliwezekani.

Chadema kwangu ni chama chenye kufuata itikadi ya Kihafidhina ( Kibepari) na mimi ni Mjamaa, na zaidi Social Democrat. Isitoshe mimi naamini mtu anaweza kushiriki siasa hata bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Naamini pia, kuwa kushiriki uongozi si lazima mtu uwe Diwani au Mbunge.

Mathalan, siwezi katika maisha yangu kufikiri kuwa kwenye msafara wa chama kilichokaribishwa kwenye kongamano la chama rafiki cha Republican cha Donald Trump!

Kwa siku mbili, Desemba 31, 2010 hadi Januari Mosi, 2011, nilipata fursa ya kuwa na Dr Slaa pale Mikumi National Park. Ilitokea tukakutana pale, mimi nikiwa na familia yangu na yeye na familia yake. Ilikuwa ni mapumziko ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Nilipata kuongea kwa kirefu sana na Dr Slaa. Nilimfahamu zaidi Dr Slaa katika siku zile mbili tukiwa pamoja kwenye mazingira ya kawaida kabisa na ya kifamilia.

Dr Slaa ni mtu makini sana. Ana uzoefu wa mambo mengi. Ni mcheshi na hakujisikia vibaya hata nilipomkosoa kwenye baadhi ya mitazamo ya Chadema.

Kwangu mimi Dr Slaa ni Mjamaa mwenye kuamini pia kwenye kujenga misingi ya kujitegemea. Ni Social Democrat pia kwa maana ya ni mtu mwenye mwenye kufikiri zaidi kwenye ustawi wa jamii pana badala ya ustawi wa wachache. Dr Slaa ni Social Democrat pia katika kuamini kwenye misingi ya uwepo wa demokrasia na kuruhusu uhuru wa fikra.

Nakumbuka, mama wa familia moja iliyokuja Mikumi kwa mapumziko alikuja na binti yake na kukaa jirani na nilipokaa mimi na Dr Slaa.

Mama yule akasema;

" Mheshimiwa, mimi na mume wangu ni Wana-CCM, lakini binti yangu huyu anaipenda sana Chadema kwa sababu yako!"

Dr Slaa, alifurahi sana na akamwambia mama yule;

" Tafadhali naomba nipige nae picha!"

Na ni nani wa kuipiga picha hiyo, kama si mimi ' Mwenyekiti Wenu!"

Naam, huyo ndio Dr Slaa ninayemfahamu mimi, maisha yake anayoishi huko aliko ni sehemu ya mafundisho kwa wananchi wa kawaida na viongozi.

Tuthamini kazi, tuhimize watu wetu kufanya kazi, na kwamba hakuna njia za mkato katika kujipatia mafanikio, iwe kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Maggid Mjengwa.

0688 37 36 52 ( Whatsapp)
 

Attachments

  • 02.jpg
    02.jpg
    51.3 KB · Views: 84
Mzee Ni bingwa wa kuharibu mambo Yale

Alinazia Chachi, akaja kitaa, akaingia siasa, halafu akavuta mboga ya mtu

Na mwisho kabisa kaishia kukimbia nchi

Ni a wasiwasi Sana jamaa anaweza Kuna kukimbia hata huyo mke na Canada kea ujumla
 
Anazugaaa huyooooo.....
Hiyo dola 10/hr wanaoweza kumudu nayo maisha ni watoto wa chuo sio mtu mwenye familia tena ya wake wawili Canada na Karatu.
Kwa heshima aliyonayo angekua na furaha zaidi...nyumbani..tatizo mke mdogo anazuzuka na kukaaa Toronto
 
Mimi Dr nitaendelea kumheshimu kwa jinsi alivyojitolea ili kuleta mabadiliko ya kweli ktk siasa za nchi hii (Tz). Pia alikuwa mjengaji wa hoja mzuri kabisa. Lakini ktk siasa hakuna kuzira, hasa watu wanapotafuta ushindi kwa gharama zozote. Alitakiwa kujua hitaji la chama wakati huo (numbers)

Pili cdm kupitia wazee, walifanya kila aina ya juhudi kuhakikisha Dr anabaki cdm. Bahati mbaya mpinzani mkuu (CCM) walionayo ufa huo, na kutumia mwanya huo kumpandikiza chuki dhidi ya nyumba yake alioijenga mwenyewe (CDM)
 
maggid huko chamani kwenu kwani hamkumlipa Mzee wa Watu kwa kazi aliyoifanya?

Au ndio anakaribia kurudi nchini sasa inatumika hii mbinu ili kutakatisha "Mabilioni" ya Malipo yake yaliyotokana na ile kazi?
Mama alishasema siasa wameacha kwa hiyo watawekeza ktk Mashule na Hospital .Fedha wanazo ila maisha ya kuakti kwa mtu aleamua inawezekana.
Akirudi atapewa Ukuu wa bodi au ukatibu wamepewa wangapi mpaka Dr akose ktk teuzi wakati alipambana vya kutosha na Lowassa. Je fadhila yake kwa kazi aliyoifanya nini
 
"Nakumbuka nilimsikiliza Dr Slaa akiongea na Taifa akitangaza rasmi kuachana na siasa. Nikaandika, kuwa binafsi naamini Dr Slaa hajaachana na siasa, bali siasa za vyama." Sasa unasema uongo ili iwe nini? Kila mtu alisikia Dr. Slaa akitangaza huo msimamo,acha kujikweza.
Mjamaa anayemiliki chombo cha habari Tanzania!!!
 
Mjamaa gani anayesema ana miliki magari mawili mazuri ya kisasa tena akiwa ughaibuni?
Kwanini asiishi kwa kupanda usafiri wa kawaida wa umma tu(treni na mabasi) ambao kwa Canada uko vizuri, uhakika na nafuu?

Mjamaa gani huyo anayeweza kuikimbia nyumba yake na kwenda kuishi hoteli ya nyota Tano hapa Tanzania. (Kumbuka 2015 Dr. Slaa alikimbia nyumbani kwake na kwenda kuishi Movenpick Royal Palm Hotel kwa zaidi ya wiki mbili).

Mjamaa gani huyo msomi wa Phd aliyesomeshwa kwa kodi za maskini na wavuja jasho anayeweza Kuikimbia nchi yake mwenyewe yenye Ardhi ya Kutosha, Rutuba, Mvua, Maji nk ili kwenda tu Amerika kuuza maduka ya wazungu ili kupata pesa za kujikimu yeye na familia yake tu, huku akiacha jamii yake nzima ikilia shida na magonjwa?

Tuwe wa kweli, Dr.Slaa sio mjamaa, hajawahi kuwa mjamaa, na wala hajawahi kuamini katika maisha ya kijamaa, na kwa sasa anapambana na hali yake huko Canada kuishi kibepari.
 
Mbona unajichanganya sana unasema Dr Slaa ni mjamaa na mtu makini lakini wewe ulikataa kujiunga Chadema kwa sababu ya itikadi yao sio ya kijamaa so ilikuaje mjamaa makini akawa Katibu Mkuu wa chama kisicho cha kijamaa?
 
Mzee alipewa chake akatembea na sasa anaishi ughaibuni, anazuga tu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona unajichanganya sana unasema Dr Slaa ni mjamaa na mtu makini lakini wewe ulikataa kujiunga Chadema kwa sababu ya itikadi yao sio ya kijamaa so ilikuaje mjamaa makini akawa Katibu Mkuu wa chama kisicho cha kijamaa?
Hapa ni ujanja wa kuangalia namna ya kumrudisha Tanzania aje kupiga tena tukumbuke 2018 up to 2019 sio mbali inatafutwa namna ya kumrudisha kwa njia ya kumwona huruma.
Dr kinachomumiza ni dhamira tu kwani haamini alichoshiriki cha kuwasaliti wenzake
 
zuga tu hiyo anataka kutakatisha mshiko haramu aliovuta..kibabu kama yeye akafanye supermarket
naona ccm wanaandaa mazingira ya kumrudisha kwa ajili ya kampeni za 2020
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom