Dr. Slaa alituokoa katika nchi ya utumwani, Lowassa anatupeleka katika nchi ya Ahadi

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Wakuu,

Hii ni combination nzuri iliyojaa manukato, iliyojaa matamanio na matarajio ya watanzania milioni 45.

Harakati za kuikomboa Tanzania ilianza miaka mingi nyuma, kuanzia Mrema wa NCCR Mageuzi enzi hizo, CUF mwaka 2000 na sasa CHADEMA kuanzia mwanzo kabisa wakiwa washirika wa CUF baada ya kumuunga mkono Lipumba 2000.

Kama mnavyojua na kwa kujikumbusha, CHADEMA ilipanda mdogo mdogo kuanzia mwaka 1995 ikiwa na wabunge watatu, 2000 wabunge watano, 2005 wabunge 12, na 2010 wabunge 49. Dr. Wilbrod Slaa ambaye tunamheshimu na kumpenda, baba yetu tunayemlilia kwa mapenzi aliyonayo kwa chama chake na watu wake, Dr. Slaa ambaye hata likizo yake aliyonayo hivi sasa tunaiona imekuwa mateso kwetu kwakuwa tunapenda kusikia kauli yake inatamka nini, ndiye aliyekuwa mmoja wa wabunge watatu wa kwanza kabisa wa CHADEMA kuingia bungeni, hadi hapo mwaka 2010 alipoacha kugombania Ubunge baada ya kupitishwa na chama kugombania urais wa jamhuri ya muungano.

Safari hii ya ukombozi wa pili kwa taifa letu pamoja na changamoto nyingi iliyochagizwa na dhiki na mateso mengi waliyokumbana nayo viongozi wa CHADEMA kutoka kwa serikali dhalimu ya CCM, viongozi ambao wamevuka milima na mabonde, viongozi ambao wamepitia katika vivuli vya mauti kwa mateso na dhihaka kutoka kwa serikali ya CCM na usalama wa taifa, bado hawakuthubutu kukata tamaa ya kuendelea kupaza sauti yao kutusemea sisi wanyonge wa nchi hii.

Dr. Slaa anafahamika kwa ujasiri wake wa kuwa msemaji wa wasio na sauti katika nchi yake anayoipenda sana, alifanya kazi kubwa akishirikiana na Mwenyekiti wetu Kamanda Mbowe na viongozi wote na makada wa chama chetu kuipigania nchi hii hadi leo tunafikia hatua ya kwenda kuingia ikulu oktoba mwaka huu.

Dr. Slaa tunaweza kumfananisha na mtu anayetajwa katika kitabu kitakatifu cha biblia anayeitwa Mussa, ambaye yeye aliwatoa wana wa Israel kutoka katika mikono ya Farao, Mussa ambaye aliwakuta wana wa Israel walikuwa hawaelewani, maana kulikuwa na makabila 12 za wana wa Israel, kila kabila lilikuwa linaongea lugha yake. Jambo la kwanza alichokifanya Mussa ilikuwa kuwaunganisha makabila yote 12 wajitambue kuwa wao ni ndugu, ilikuwa kazi kubwa na ngumu maana walikuwa hawapatani, lakini alifanikiwa kuwaunganisha. Ilikuwa furaha ya Farao alipotaka kuwatawala wana wa Israel alikuwa anawagawa kwa makabila yao, yaani kabila la yuda, sijui kabila la benjamin nk.
Lakini siku wana wa Israel walipojitambua kuwa wao ni ndugu, ilimuwia vigumu Farao kuwatumikisha tena wana wa Israel, hadi Mussa alipofanikiwa kuwatoa kutoka katika nchi ya utumwa.

Wana wa Israeli wa leo wanaweza kuwa vyama vya upinzani ambao wao kwa wao hapo awali walikuwa wanarushiana vijembe, ikawa ndiyo raha ya CCM kuendelea kutawala. Siku vyama vya upinzani hasa vyenye uwakilishi bungeni vikiongozwa na chama kikuu cha upinzani bungeni yaani CHADEMA, ilikuwa shida kwa CCM kuendelea kutupa vijembe vyao, vyama sasa vinaongea lugha moja, vinamtambua adui yao ni moja tu, ambaye ni CCM na serikali yake ya kifisadi.

Kiongozi wetu Dr. Slaa ametufikisha hapa tulipo leo, sasa jukumu la kutupeleka katika nchi ya ahadi, nchi iliyojaa maziwa na asali amepewa Kamanda Edward Ngoyai Lowassa, mzee wa maamuzi magumu, mzee ambaye nakumbuka alipokuwa mkurugenzi wa AICC alikuwa anapanga foleni kuchukua motisha pamoja na wafanyakazi wa kawaida kabisa.

Lowassa tunaweza kumfananisha na Joshua, aliyepokea kijiti kutoka kwa Mussa njiani, akawapeleka wana wa Israel katika nchi ya Kana.

Hata hivyo Edward Ngoyai Lowassa tunaweza kumfananisha na mtu moja katika biblia alikuwa anaitwa Sauli (Matendo 9:1-43), huyu alikuwa jemedari wa jeshi aliyekuwa anapinga na kuwaua wale wote wanaohubiri habari za Yesu. Lakini hali akiwa njiani amepewa kibali na kuhani mkuu ili kwenda kuwateketeza akina Petro na Yohana waliokuwa wanahubiri habari za Yesu katika Dameski, ghafla akakutana na Yesu Kristo njiani, akamwambia Sauli Sauli mbona unaniudhi? Mungu akampa upofu kwa siku tatu hakuweza kuona, kutoka hapo Mungu akamwambia inuka sasa nitakupa kazi ikupasayo kufanya, na kuanzia sasa hautaitwa Sauli tena, bali utaitwa Paulo

Nami natamka kwamba Edward Lowassa siyo yule aliyekuwa ng'ambo ile, huyu ni Edward Lowassa mpya aliyezaliwa upya baada ya kutoka kwenye chama cha kifisadi cha CCM, Eddo sasa mwendo mdundo tunatembea tunaringa, tunajivunia na Eddo.

Eddo anatupeleka Nchi ya Kanaani.

Kwa usimamizi madhubuti wa Mtendaji Mkuu wa Shughuli za CHADEMA chini ya Katibu Mkuu Dr. Slaa, tunaamini serikali inayotokana na CHADEMA itakuwa serikali ya mfano, Rais Lowassa atawajibika moja kwa moja kwa katibu mkuu Dr. Slaa, naye Dr. Slaa atakuwa bega kwa bega na team yake kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CHADEMA na UKAWA.

Twendeni na Edward Lowassaaaaaaaaaa!!!
 
Dr Slaa alituongoza kutupeleka katika nchi ya neema na sasa UKAWA wanaenda kutuvusha mto salama tuweze kumiliki nchi yetu yenye kila utajiri wa maliasili
 
Gizani ukitaka unakwenda mwenyewe.... awamu hii sijui mtaficha wapi nyuso zenu

mie nimo humu jf... kama kawa.. ila unaandika kusadikika sana kamanda.. safari njema ..muendako....
ukweli lazima tuseme hata kama mchungu kusikia mshateleza mkubali na matokeo....
dr slaa ndio keshawatema huo ndio ukweli...tungepunguza porojo... tu..
hapa walau tuelezeni hiyo mikakati ya safari ya gizani
 
Mkuu Mungi heshima kwako, hakika ni ufafanuzi maridhawa kabisa........naamini hukk aliko Dr Slaa anatafakari tulipoanzia mpk hapa tulipo, imani yangu anakuja kuweka mambo sawa na Farao (CCM)anakwenda kuangamia pale kwenye sanduku la kura........MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI UKAWA.
 
Ni sawa kabisa. Twende na Eddo, kanaani kula kila kitu, asali na maziwa. Wtanzania tuache kula mana!
 
Mkuu Mungi umemaliza kila kitu,atakayetaka na aelewe asiyetaka akale malimao! mabadilko hayazuiliki!
 
Wakuu,

Hii ni combination nzuri iliyojaa manukato, iliyojaa matamanio na matarajio ya watanzania milioni 45.

Harakati za kuikomboa Tanzania ilianza miaka mingi nyuma, kuanzia Mrema wa NCCR Mageuzi enzi hizo, CUF mwaka 2000 na sasa CHADEMA kuanzia mwanzo kabisa wakiwa washirika wa CUF baada ya kumuunga mkono Lipumba 2000.

Kama mnavyojua na kwa kujikumbusha, CHADEMA ilipanda mdogo mdogo kuanzia mwaka 1995 ikiwa na wabunge watatu, 2000 wabunge watano, 2005 wabunge 12, na 2010 wabunge 49. Dr. Wilbrod Slaa ambaye tunamheshimu na kumpenda, baba yetu tunayemlilia kwa mapenzi aliyonayo kwa chama chake na watu wake, Dr. Slaa ambaye hata likizo yake aliyonayo hivi sasa tunaiona imekuwa mateso kwetu kwakuwa tunapenda kusikia kauli yake inatamka nini, ndiye aliyekuwa mmoja wa wabunge watatu wa kwanza kabisa wa CHADEMA kuingia bungeni, hadi hapo mwaka 2010 alipoacha kugombania Ubunge baada ya kupitishwa na chama kugombania urais wa jamhuri ya muungano.

Safari hii ya ukombozi wa pili kwa taifa letu pamoja na changamoto nyingi iliyochagizwa na dhiki na mateso mengi waliyokumbana nayo viongozi wa CHADEMA kutoka kwa serikali dhalimu ya CCM, viongozi ambao wamevuka milima na mabonde, viongozi ambao wamepitia katika vivuli vya mauti kwa mateso na dhihaka kutoka kwa serikali ya CCM na usalama wa taifa, bado hawakuthubutu kukata tamaa ya kuendelea kupaza sauti yao kutusemea sisi wanyonge wa nchi hii.

Dr. Slaa anafahamika kwa ujasiri wake wa kuwa msemaji wa wasio na sauti katika nchi yake anayoipenda sana, alifanya kazi kubwa akishirikiana na Mwenyekiti wetu Kamanda Mbowe na viongozi wote na makada wa chama chetu kuipigania nchi hii hadi leo tunafikia hatua ya kwenda kuingia ikulu oktoba mwaka huu.

Dr. Slaa tunaweza kumfananisha na mtu anayetajwa katika kitabu kitakatifu cha biblia anayeitwa Mussa, ambaye yeye aliwatoa wana wa Israel kutoka katika mikono ya Farao, Mussa ambaye aliwakuta wana wa Israel walikuwa hawaelewani, maana kulikuwa na makabila 12 za wana wa Israel, kila kabila lilikuwa linaongea lugha yake. Jambo la kwanza alichokifanya Mussa ilikuwa kuwaunganisha makabila yote 12 wajitambue kuwa wao ni ndugu, ilikuwa kazi kubwa na ngumu maana walikuwa hawapatani, lakini alifanikiwa kuwaunganisha. Ilikuwa furaha ya Farao alipotaka kuwatawala wana wa Israel alikuwa anawagawa kwa makabila yao, yaani kabila la yuda, sijui kabila la benjamin nk.
Lakini siku wana wa Israel walipojitambua kuwa wao ni ndugu, ilimuwia vigumu Farao kuwatumikisha tena wana wa Israel, hadi Mussa alipofanikiwa kuwatoa kutoka katika nchi ya utumwa.

Wana wa Israeli wa leo wanaweza kuwa vyama vya upinzani ambao wao kwa wao hapo awali walikuwa wanarushiana vijembe, ikawa ndiyo raha ya CCM kuendelea kutawala. Siku vyama vya upinzani hasa vyenye uwakilishi bungeni vikiongozwa na chama kikuu cha upinzani bungeni yaani CHADEMA, ilikuwa shida kwa CCM kuendelea kutupa vijembe vyao, vyama sasa vinaongea lugha moja, vinamtambua adui yao ni moja tu, ambaye ni CCM na serikali yake ya kifisadi.

Kiongozi wetu Dr. Slaa ametufikisha hapa tulipo leo, sasa jukumu la kutupeleka katika nchi ya ahadi, nchi iliyojaa maziwa na asali amepewa Kamanda Edward Ngoyai Lowassa, mzee wa maamuzi magumu, mzee ambaye nakumbuka alipokuwa mkurugenzi wa AICC alikuwa anapanga foleni kuchukua motisha pamoja na wafanyakazi wa kawaida kabisa.

Lowassa tunaweza kumfananisha na Joshua, aliyepokea kijiti kutoka kwa Mussa njiani, akawapeleka wana wa Israel katika nchi ya Kana.

Hata hivyo Edward Ngoyai Lowassa tunaweza kumfananisha na mtu moja katika biblia alikuwa anaitwa Sauli (Matendo 9:1-43), huyu alikuwa jemedari wa jeshi aliyekuwa anapinga na kuwaua wale wote wanaohubiri habari za Yesu. Lakini hali akiwa njiani amepewa kibali na kuhani mkuu ili kwenda kuwateketeza akina Petro na Yohana waliokuwa wanahubiri habari za Yesu katika Dameski, ghafla akakutana na Yesu Kristo njiani, akamwambia Sauli Sauli mbona unaniudhi? Mungu akampa upofu kwa siku tatu hakuweza kuona, kutoka hapo Mungu akamwambia inuka sasa nitakupa kazi ikupasayo kufanya, na kuanzia sasa hautaitwa Sauli tena, bali utaitwa Paulo

Nami natamka kwamba Edward Lowassa siyo yule aliyekuwa ng'ambo ile, huyu ni Edward Lowassa mpya aliyezaliwa upya baada ya kutoka kwenye chama cha kifisadi cha CCM, Eddo sasa mwendo mdundo tunatembea tunaringa, tunajivunia na Eddo.

Eddo anatupeleka Nchi ya Kanaani.

Kwa usimamizi madhubuti wa Mtendaji Mkuu wa Shughuli za CHADEMA chini ya Katibu Mkuu Dr. Slaa, tunaamini serikali inayotokana na CHADEMA itakuwa serikali ya mfano, Rais Lowassa atawajibika moja kwa moja kwa katibu mkuu Dr. Slaa, naye Dr. Slaa atakuwa bega kwa bega na team yake kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CHADEMA na UKAWA.

Twendeni na Edward Lowassaaaaaaaaaa!!!

I think you have a squint mind and thinking brother
 
Hivi mmeishajiuliza nini hatma yenu CDM katika miaka miwili ya kwanza kama anapewa urais japo hilo halipo ama mko mnawaza ya leo tu kama funza?
 
Kamanda Mungi umenena vema, umeihusisha post yako na maandiko matakatifu na kutuleta kwenye wakati uliopo. Naamini hata Dr. Slaa akiipitia hakika atalegeza msimamo wake.
 
Mkuu Mungi umemaliza kila kitu,atakayetaka na aelewe asiyetaka akale malimao! mabadilko hayazuiliki!

Nape aliyesema mafuriko ameyazuia kwa mikono inampa taabu sana. Wamefarakanishwa hata sema yao, jana Katibu wao amewaita makapi wale waliogombea nafasi mbalix2

Jahazi la CCM limetoboa maji yanaingia abiria wanashangaa hata life Jacket hawataki kuvaa hakika wanaenda kuzama.
 
Back
Top Bottom