Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Wanachama, wapenzi na wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kwanza tuanze na salamu za chama.... Peeeeooooppppleeess...
Naweza kufanya kope za macho za watu wachache ziinuke kwa kusema aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Dr. Wilbroad Slaa alikuwa mzuri kabla hajawa mbaya.
Nimeanzisha uzi huu kwa nia ya kuibua mjadala juu ya nafasi ya katibu mkuu kwenye chama kwa sasa.Nitajaribu kufanya kazi hii ngumu ya kukata nyama ya mtu bila kutoa damu kwa imani kuwa nitafanikiwa.
Dr. Wilbroad Slaa aliimudu nafasi ya katibu mkuu Chadema na pamoja na mapungufu machache, Dr. alikuwa moja ya wanasiasa wachache Tanzania wenye moto kwenye matumbo yao~ politicians with fire in their bellies. Dr. alijitahidi kukijenga chama na alifanya kazi kwa nguvu hivyo kwamba chama kilienea harufu yake karibu kila mahali.
Dr. Slaa alijitahidi kupambana na ubaya kabla ya ubaya kumshinda nguvu.Yes Dr. knows the strength of the Germany army because he fought against it before giving in.
Ndoto ya Chama na ndoto ya Dr. ya kukuza chama inaenda kutimia.
Chama kina wenyeviti wengi wa mtaa.
Chama kina wajumbe wengi sana
Chama kina utitiri wa Madiwani
Chama kina Mameya
Chama kina wabunge wengi na wengi wageni.
Chama kina wanachama, wapenzi na wafuasi ambao hawajivungi kuonyesha wazi wazi kuwa wanakiunga mkono chama.
Lakini lazima tukubali jambo, uchaguzi huu umetuunganisha katika Chama kama mayai yalivyounganishwa na tray.
Chama kinahitaji katibu atakayelitambua hili, katibu atakayeifanya kwa ufanisi zaidi kazi ya Dr. Slaa na atakayefaulu pale Dr. aliposhindwa.
Chama kinahitaji usimamizi mzuri kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote, Chama kinahitaji kufikia matarajio ya watanzania waliokiamini sana, Chama kinapaswa kutambua kuwa utitiri huu wa viongozi hautakosa fuko ndani yake.
Chama kinahitaji uwazi, uadilifu na uwajibikaji sasa kuliko wakati mwingine.
Chama kinamhitaji katibu mkuu anayeijua CCM vyema na atakayepanga timu yake vizuri kuelekea 2020.
Hoja ya uwakilishi kikanda nayo ni hoja, japo hoja ya ' a round peg in a round hole' ni hoja zaidi.