Dr Slaa akata anga Usukumani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa akata anga Usukumani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masanilo, Sep 9, 2010.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dk Willibrod Slaa ameingia mkoani Shinyanga kusaka kura za urais. Na Chopper yake imeanza kazi upya baada ya kufanyiwa matengenezo madogo kwa siku nne zilizopita. Wananchi waliochoshwa na usanii na uwongo waCCM, kwa kauli moja watampatia kura za ndiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hali tete ya Afya ya Kikwete inawatisha wananchi wengi.

  Mch Masa Kwenye Msafara wa Slaa  Source: Ngurumo Blogspot
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145


  Tunamtakia kila la kheri Rais mteule,

  Aendelee kumwaga sera za ukweli kwa maendeleo ya watanzania wote, ili wale waliofungwa na minyororo ya chama cha mafisadi wafumbue macho na kupiga kura yao kwa kiongozi makini na sahihi kwa manufaa ya watanzania wote, hapo tarehe 31 october.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wasukuma wamebadilika sana si wale wa kupewa chumvi na pombe za kienyeji! Mwaka huu hawafanyi makosa waliambia Mwanza itakuwa kama California wameona alichokifanya kwa miaka mitano! Aibu

  Slaa for a change! Wasukuma Can be part of that Change
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mchungaji Sanate kwa habari,

  Ni dalili nzuri pale inapoonekana wasukuma kushtukia ahadi za mkuu wa kaya, aka mzee wa ahadi.
  Patachimbika mwaka huu!! Tujuze mchungaji wetu, tena ikibidi kwa picha.
   
 5. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Rev M .. tupe picha mkuu...!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Msiwe na wasi wasi picha na clips mchungaji ataziweka! Kanga na Kofia na Tshirts za CCM hazina soko huku! Hazitakiwi hata bure
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  leo mko maeneo gani mch.

  hakikisheni mnafika hadi kijiji cha masanzakona.. huku ndo nilipo
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Tafuta clips za wananchi kukataa picha na kanga!!
   
 9. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Live kakutana mjamzito akiwa kabebw kwenye mkokoteni wa kukokotwa na ng'ombe akipelekwa hospital na JK kaahidi bajaj, sijui afadhali nini sasa hapo.Pipooooooooooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaa.
   
 10. n

  nmaduhu Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa hahitaji nguvu kubwa huko, tayari kazi nishaifanya, yeye awasilimu tu, ccm pia ishamsfishia njia,
  bei ya pamba ni aibu kubwa kwa wakulima, asisahau kuwakumbusha masuala makubwa ya ufisadi, mambo
  ya chunvi sasa basi........

  yale mabomu yake 20 lini ataanza kuyalipua?? alipue japo mawili shinyanga.....

  ccm byebyeeeeeeeeeeeeee.
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Huko inabidii akaze buti kweli kweli, maana madudu yote ya ufisadi yamekuwa na adhari kubwa saana kwa mkoa huo, mfano usafiri wa reli, ukosefu wa umeme, matokeo mabaya ya shule, kiwanda cha nyama alicho uziwa ......., shule ya kiingereza sijui ya nani ambapo mkuu wa mkoa alitaka kuwauzia serikali, buzwagi ambayo haiwasaidi wananchi, mwadui ambayo mapato yake haijulikani vizuri yapo wapi, mkoa licha ya kuwa ni tajiri wa kutupwa hata scanner hawana, airport yenyewe mpaka ijengwe na mwekezaji? mwadui mine, na waka mleta rafiki yao el hilala mines? kuchimba hayo madini yule walio muuzia jengo dar kwa ku under value? sijui ili sakata liliishiaje.
  na npenda zoe wanaye na shibuda huko ni kuwapiga shule kwa kwenda mbele, pili wawaambie hao ccm wanaojisifia kwamba wamefanya vizuri ya nini kutumia mabilllioni ili kushinda? kama sio ghiliba.
  na huyo kiongozi wa ccm anayetembea na pipi ili kuwapa watoto na kuwa kumbatia watu wa chini akijifanya anawapenda mbona basi asitoe huduma milele badala ya kuwapenda kwa dakika mbili za kupiga picha nao na kuwapa "rushwa" ya pipi au bicycle au kumlipia matibabu, mtu moja wakati ni watanzania wangapi wenye kuhitaji hiyo huduma. akiwa ni baba mzuri ataangalia zaidi ya mtoto moja na itakuwa ni mradi wa kuwasaidia wengi na utekelezaji wake ufanyike sio hadithi, na wizi.
  mfano hiyo barabara ya shy -mza imechukua miaka mingapi na wizi mkubwa, je walio husika wamechukuliwa hatua? tabora-shy napo ni hivyo hivyo, je barabara ya lamadi musoma?
   
 12. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wasukuma bila pombe za kienyeji hazipandi na bila ya kuinywa hasa siku za uchaguzi hawakupi kura hivyo ni uwamuzi wa Padre Slaa kumwaga pombe za kienyeji kwa Wasukuma au akose kura! CUF najuwa hawana uwezo wa kutumia Helkopta wala kutoa pombe za kienyeji kwani baadhi ya JF members wameshafanya utafiti wao na kugundua viongozi karibu wote wa CUF wana harufu ya Uislamu na Pombe ni haramu kwa mujibu wa Uislamu!

  Hivyo wanaotegemewa kugawa pombe za kienyeji ni Padre Slaa na Chadema yake au JMK na CCM yake! kazi kwa Padre ataweza kazi hiyo?
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Jamani mtauwa ccm jamani,ioneeni huruma.............mnajua ccm wakijua kuwa hawakubali kiasi hiki nina wasiwasi wataacha kampeni kabisa na kuanza kuandaa mbinu chafu za kuiba kura wakati sisi tumewachoka......
  We are more than very tired..
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Vp wasukuma sikuhizi hawataki hata pilau za ccm?....km ndivyo basi mabadiliko ni makubwa.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,907
  Likes Received: 12,046
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mgombea Urais Kupitia Chadema Mheshimiwa Dk Willibrod Slaa leo ameingia mkoani Shinyanga kusaka kura za urais kwa kishindo.Na Helikopta yake imeanza kazi upya baada ya kufanyiwa matengenezo madogo kwa siku nne zilizopita
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  CUF si yakubeza mkuu! wananguvu ya ajabu kule Tabora jimbo la Urambo Mashariki na hata kule aliko Kapuya Kuna jimbo wanaweza zoa huko!
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kama ni hivyo ni vizuri chadema wakayaachia hayo majimbo, ili kuwaondoa hao vigogo wa chichiemu
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Dk. Slaa: Nitafumua mikataba ya madini

  [​IMG]
  Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, amesema ikiwa atashinda kiti hicho, serikali yake itafumua mikataba ya madini na kufuta misamaha ya kodi katika sekta hiyo.

  Dk. Slaa alisema msamaha wa kodi katika kampuni za madini, unapoteza Sh bilioni 700, fedha alizosema serikali yake itazielekeza kwenye elimu. Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kwideko mjini Ngudu wilayani Kwimba jana, Dk. Slaa alisema inasikitisha kuona wageni wanafaidika na rasilimali za taifa huku Watanzania wakibaki masikini.

  Alisema takwimu zinaonyesha kwamba madini yanaendelea kwisha lakini hayajawanufaisha Watanzania.
  "Misamaha ya kodi ya mafuta kwenye makampuni ya madini inapoteza zaidi ya Sh. bilioni 700 kwa mwaka, kama zisingesamehewa sidhani kama leo tungechangishwa kujenga shule," alisema.

  Aliongeza: "Madini hayaozi, hata Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema."
  Pia Dk. Slaa alisema akichaguliwa mishahara ya ‘vigogo' serikalini na wabunge itapunguzwa kwa asilimia 20. Alifafanua kuwa taarifa ya serikali iliyotolewa Julai mwaka huu bungeni, inaonyesha kuwa wilaya ya Kwimba ina jumla ya shule za msingi 150 na walimu 109, idadi isiyoendana na hali halisi.

  Aliongeza kuwa takwimu hizo ambazo zilitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, zinaonyesha wilaya hiyo ina shule za sekondari 35 na walimu 41. "Hizi sio takwimu za Dk. Slaa ni za serikali, sasa ujiulize haya ndiyo mafanikio ya CCM, haya ni sawa na majosho ya ng'ombe unampeleka hapo suala la kupe kufa halikuhusu, ni aibu miaka 50 baada ya uhuru adui ujinga bado anatutesa," alisema.

  Dk. Slaa ambaye alilakiwa na umati mkubwa wa wananchi, alisema wakati Mpango wa Maendeleo ya Shule za Sekondari (MMES) ulipoanza, Bunge liliidhinisha fedha za kusomesha walimu 15,000 na mwaka uliofuata zilitengwa kwa ajili ya walimu 10,000 ambao hata hivyo hawaonekani.

  "Takwimu hizi zinaonyesha pia kuwa mwaka jana watoto waliomaliza darasa saba zaidi ya nusu hawakupata nafasi ya kujiunga sekondari, hawa tumewaharibia maisha yao...mnaweza kujiuliza taifa linakwenda wapi," alihoji. Alisema njia pekee ya kulikomboa taifa ni kurekebisha mfumo wa elimu.

  Dk. Slaa alisema shule ni lazima ziwe na miundombinu muhimu pamoja na vitabu na walimu.
   
Loading...