Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 13,808
- 27,619
MWENYEKITI mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, amesifu kampeni za aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akisema zimetoa fundisho kubwa kwa vyama na wagombea wao.
Dk. Bana, ambaye amemmwagia sifa Dk. Slaa, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC).
Alisema kuna haja ya kujiuliza kwanini CHADEMA ambayo katika uchaguzi wa mwaka 2005 ilishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 668,756 sawa na asilimia 5.8, lakini katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu imepata kura zaidi ya milioni mbili, sawa na asilimia 26.5.
"Hili ni jambo zuri, linatufundisha nini, ukiwa na timu nzuri ya kampeni ukatembea maeneo mengi na kutoa sera zinazowagusa wananchi, utasikika na kuna uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri kama tulivyoona kwa CHADEMA, hili ni fundisho kubwa hasa kwa wagombea na vyama vyao," alisema Dk. Bana.
Alisema Dk. Slaa alidhihirisha umahiri wake wakati akiwa bungeni, hasa aliposimamia kidete suala la ufisadi, ambalo wakati wa kampeni alilinadi pia kwa wananchi na kuahidi kulitatua iwapo atapewa ridhaa ya kuingia ikulu na wananchi.
Alibainisha kuwa kama wagombea wote wangekuwa kama alivyokuwa Dk. Slaa, uchaguzi wa mwaka huu ungekuwa na ushindani mkubwa na hata rais angepatikana kwa tofauti ya kura chache kama ilivyotokea Zanzibar.
Alisema miongoni mwa sera za CHADEMA zilioonekana kuwagusa wananchi ni utoaji wa elimu bure, ambayo hata hivyo ilikuwa ikibezwa na baadhi ya wagombea na makada wa vyama Fulani, kwa madai kuwa haitekelezeki, bali ni hadaa ya Dk. Slaa na chama chake ili wapate kura.
Alisema matokeo ya uchaguzi ambayo yaliipa CHADEMA viti visivyopungua 22 na Chama cha Wananchi (CUF) viti 24 yatachangia kwa kiasi kikubwa kuleta upinzani wa hoja bungeni na kulifanya Bunge litakaloanza kesho mkoani Dodoma kuwa la uwajibikaji zaidi, tofauti na ilivyozoeleka kipindi cha nyuma.
"Profile ya wabunge hasa wa CHADEMA na NCCR Mageuzi ni nzuri, inavuta na kutia moyo, tunatarajia Bunge lenye mvuto na ushindani mkali wa hoja ," alisema Dk. Bana.
Katika hatua nyingine, Dk. Bana alielezea kukerwa na tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali kutumia magari ya umma kuendesha kampeni za aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete.
"Vyombo vya serikali kutumika katika kampeni si jambo zuri katika uwanja wa siasa, hili linawanyima fursa wagombea wa vyama vingine kushiriki kwenye uwanja ulio sawa," alisema Dk. Bana.
Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu mwamko mdogo wa wananchi kujitokeza kupiga kura, alisema jambo hilo linatakiwa kufanyiwa utafiti wa kina ili kubaini chanzo cha watu kutojitokeza kupiga kura, licha ya kuwapo idadi kubwa ya waliojiandikisha.
Alibainisha kuwa pamoja na wagombea kuzunguka maeneo mbalimbali ya hapa nchini kwa kutumia usafiri tofauti ukiwamo wa magari, helikopta, ndege, pikipiki na vifaa vinginevyo ili mradi kuwafikia wananchi, bado wahusika wameshindwa kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la upigaji kura.
Dk. Bana pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia suala la uharibikaji wa kura za urais, ambapo alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu tatizo hilo limepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na chaguzi zilizopita.
"Kura zilizoharibika kwa mwaka huu ni 227,889 ambazo ni sawa na asilimia 2.64, tofauti na mwaka 2005, ambapo asilimia ya kura zilizoharibika ilikuwa 4.9, nawapongeza wahusika kwa hatua hii," alisema Dk. Bana.
Alibainisha kuwa kuna haja ya elimu ya uraia na ya uchaguzi kuwa endelevu ili kuwafanya wananchi kupata uelewa wa kutosha badala ya elimu hiyo kutolewa kwa mtindo wa zimamoto kila unapofika wakati wa uchaguzi.
Aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kurekebisha kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi huu, pia kuwataka wananchi kutosubiri kusukumwa hasa katika kufanya jambo lenye maendeleo.