Dr Shika amekamilisha leo malipo ya bima kwa ajili ya kutumiwa fedha zake kutoka nchini Urusi

Ziara ya Waziri na Uwepo wa Shika is it coincidence? Majirani wanasema huwa wanamsaidia chakula, leo ana dola mia! Shija alirudishwa nchini 2004 leo ndo anafanya mchakato wa kutumiwa peaa zake! Hivi waandishi wa habari siku hizi hawana maswali au uwezo kufikiria umeshuka?
Nikipata nafasi ya kumuuliza Shika maswali, swali langu la kwanza kwake nitamuuliza mara ya mwisho alikuwa Urusi lini? Je, kampuni yake ipo hai au imekufa? Kama ipi hai nani anaiendesha? Kwa muda wote aliokuwepo hapa nchini amekuwa akifanya nini?

Kuna kideo cha shingogo mbona ameelezea hayo.. pia ingia kwenye website ya kampuni ujisomee.
 
Nina mashaka sehemu moja hivi...wale wezi wa mtandao hawatumii bank ata siku moja mara nyingi wanatumia western unuion au njia nyingine kama hizo maana ukitumia bank ni rahisi kudakwa. Pili hizo dollar mia katoa wap wakati wanaomkejeli wanasema ata pesa ya kula hana ata kodi ya nyumba hana? Tusubirie kidogo tu
hilo la kudaiwa kodi ya nyumba lilikuja kukanushwa na hao hao waandishi MAKANJANJA.
 
Dah aisee sasa hawa matapeli wanaotumia bank nadhani wanajiamini sana mara matapeli wengi niwajuao wa kinaijeria hawatumii bank kufanya miamala
kwa kumsikiliza Dr shika na uwezo wake wa kuzungumza na experience aliyonayo ya kuishi nje ya nchi ni vigumu yeye kutapeliwa. Kuna jambo.
 
Kumbe tunao ishi kwenye chumba kimoja na bafu la nje tunadharaulika hivi!!!lakini nakuhakikishia hata ukimiliki ghorofa kama la Lugumi bado utalala chumba kimoja

Mkuu sijadharau watu wanaoishi chumba kimoja cha kupanga. Lakini, lazima tukubaliane kuwa watu tunatofautiana kwa kipato.

Kama mtu una $10million kwa nini upange chumba badala ya kujenga au kununua nyumba yako?!
 
Yani nashangaa ambao bado hawajaona dr alivyopigwa.
Bima ya millions of dollars unailipia Bima cia moneygrm wakati hiyo ela itapita bank?
Na bado watu wanaona dr kaula.
Huyu Dr na yule babu wa Loliondo ni sawa moja. Nashangaa wameweza kuwaokota na watu wenye akili na elimu yao!
 
isiwe mafisadi wanataka kurudisha hela kupitia huyo dr wenu, maana wameona za bongo zimekazwa sasa wakatafuta namna ya kurudisha. siku zote alikuwa wapi hadi asubiri mnada?

Labda wanafanya uchunguzi maana kwa kujisifia wana weledi wa kutosha na majibu ya "Hana hadhi hata ya million moja"
 
Kwa utapeli anaofanyiwa huyo dr. Shika na waandishi walivyo shikwa masikio.
Mambo ya kiongo tu hayo..hana pesa wala nn..hayuko sawa hata km ni dr. Apimwe akari vzuri, itafahamika tu
 
Ayaaaaaa...dr. shika mgonjwa kapigwa...km kakopeshwa hyo pesa kwa ahadi ya kulipa pesa yake ikija...nae kapigwa.
Afu bado watu hawajaelewa tu....
Kweli nchi hii ina mburura wengi
 
Billion 21 uzipate kindezi namna hyo...dr kapigwa hzo hela za bima....na usawa huu all around the world hakuna mtu wa kutuma such amount of money kimama mama hivyo...kiasi cha hela cha namna hyo lazima kiwe approved na benki kuu ya nchi husika na source yake ijulikane....kama alikuwa jasusi watampaje hzo hela hao warusi?? .sio kwa urahisi huo....go to the hell dr Shika
 
Back
Top Bottom