Dr. Salim A. Salim aula Mo Ibrahim

Mtanzania pekee aliyewahi kutuwakilisha kimataifa, msafi, na bado anang'ara internationally. Go Dr. Salim tunakuheshimu.
 
Jamaa ni kichwa na anaheshimika sana kwenye Jumuiya za Kimataifa. Ni CCM pekee haithamini na kuheshimu kipaji chake!!
Hongera sana Dr. S.A.S

Mkuu sio kwamba CCM walikuwa hawathamini bali walijua jamaa akishika urais wale mafisadi CCM bara na Visiwani watakuwa hawana chao maana jamaa ni muumini mzuri wa maadili kazini. Nyerere aliwahi kumwambia Salim laiti isingelikuwa umri na ujana angelimwachia urais akiondoka yeye. Kumbe ilikuwa mistake kubwa alipokuja mwinyi ufisadi ukaanza, mkapa akuukuza, Kikwete akamaliza kabisaaa. Ndio hivyo basi tubakie kulalamika na kusikitika tu maana tumemkosa yeye na mzalendo mwengine Dr Slaa yaani Tanzania saa zengine unaweza kusema sijui tuna laana!!!!
 
Mtu yoyote mwenye P.hD ya kusaka mwenyewe bila kutafutiwa Data ni kichwa. Check Silaa, SAS na Magufuli. Ila serikali yetui haiwakubali kabisa inakumbatia mahonorarial P.hD. Inasikitisha sana jinsi taifa linavyoelekea.

SAS songa mbele, mtandao wa 2005 ulikupaka matope ila sasa unatoka, endelean na Mungu hana hiyana utakula kivulini.
 
Msharika na wengineo kuweka rekodi sawa Dr Salim Ahmed Salim hana PhD ana Honoraria Doctorate lakini aliyofanya nadhani makubwa kuliko hata hao walio na PhD wakaigeuza kuwa title ya kisiasa. Nilikuwa naweka sawa taarifa tu tusimkweze sana.
 
Dr. Salim tuna imani kubwa na wewe ktk kuongoza jumuiya kubwa kama OAU, lakini cha ajabu CCM hawaoni umuhimu wako katika taifa hili, ka vipi jiunge na kambi ya upinzani tukupe rungu kwani mchango wako ni muhimu kwenye taifa letu lililochafuliwa na ufisadi.
Ni ushauri tu nakupa.
 
ccm haipendi watu makini na wenye uwezo kama SAS
Uwezo wa Salim kiuongozi unatambuliwa na watu wanaojua uongozi wa umma. Baada ya Nyerere, hakuna liyebaki huko kwenye uongozi wa CCM anayeweza kutambua uwezo wa Salim. By inference, nadhani unaweza kuhua ni nani waliobaki kwenye uongozi wa CCM.

Hongera Dr. Salim
 
Hongera SAS. Wengi wanadhani ungekuwa Rais mzuri Tanzania. Mimi siamini hilo. Hauijui Tanzania na Watanzania. Ulikuwa Balozi wetu kule Misri at the age of 22! Uliporudi ukawa waziri wa mambo ya nje. Ukawa WM kwa kipindi kifupi sana. Ulipwaya sana kwenye nafasi ile iliyokuwa imeshikwa vilivyo na mtangulizi wako Sokoine.
 
Hongera sas!!!! lakini mo na salim ni marafiki kuna wakati mo alipokuwa mmiliki celtel salim alikuwa mwenyekiti wa bodi ya celtel kwahiyo hawa watu wanajuana siku nyingi
 
Hongera sas!!!! lakini mo na salim ni marafiki kuna wakati mo alipokuwa mmiliki celtel salim alikuwa mwenyekiti wa bodi ya celtel kwahiyo hawa watu wanajuana siku nyingi
SAS na Mo ni kama RA na Al Adawi wa DOWANS. Wengi hili hawalijui.
 
Kwanini 2005 CCM walimpa Mkwere? Tunaacha viongozi tunachukuwa Mafisadi VERY SAD

Hongera Dr. Waukweli S.A.S

Wewe hujui? Dr SAS ni mhanga wa ukabila na udini. Hukumbuki mwaka 1985 na 2005 alipojaribu kugombea Urais alipachikwa UKABILA (eti ni mwarabu, mara ooo hizbu, mara ni muOman). Na wahariri wa magazeti ya bongo wakafanya biashara ya kuuza magezi kwa ku-publish ujinga huo. 2005 yaleyale yaliompata 85 yakamdondokea kwa nguvu. Mapadre wakasema SAS hapana, chaguo la Mungu ni JK.
Jamani, ukabila na udini unaitafuna nchi.. hamuoni?

Nachikia tabia hii.
 
Hongera sana dr achana na hawa wanaoona umepewa kwa upendeleo wamechanganyikiwa bcs waliona jk labda angefaa kupewa! Hongera sana mkuu!
 
Wewe hujui? Dr SAS ni mhanga wa ukabila na udini. Hukumbuki mwaka 1985 na 2005 alipojaribu kugombea Urais alipachikwa UKABILA (eti ni mwarabu, mara ooo hizbu, mara ni muOman). Na wahariri wa magazeti ya bongo wakafanya biashara ya kuuza magezi kwa ku-publish ujinga huo. 2005 yaleyale yaliompata 85 yakamdondokea kwa nguvu. Mapadre wakasema SAS hapana, chaguo la Mungu ni JK.
Jamani, ukabila na udini unaitafuna nchi.. hamuoni?

Nachikia tabia hii.
Mchakato wa Urais mwaka 1985 anayeweza kuuelezea vizuri ni JS Warioba na Getrude Mongela. SAS aliitwa tena mwaka 1995. Akadengua. Baada ya kifo cha Mwalimu mwaka 1999, nyota ya SAS nayo ilipotea kabisa. Mwaka 2005 alikosea kuchukua fomu huku akijua hana mtu kama Mwalimu ndani ya CCM na wanavisasi wa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom