Dr. Rugemeleza Nshala unafurahishwa na Wakili Fatma Karume anavyoikashfu Mahakama, Majaji na viongozi wa nchi hii?

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Dkt Rugemeleza Nshala, sisi wanachama wenzio wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) tunakuandikia kwa masikitiko makubwa sana kuhusu malalamiko yafuatayo:

Tumesikitishwa sana na Tamko lako la tarehe 23 Septemba, 2019 ulilotoa kwa Umma lenye kichwa cha habari kinachosomeka TLS GOVERNING COUNCIL STATEMENT POWERS OF CHIEF JUSTICE AND HIGH COURT JUDGES TO SUSPEND ADVOCATES UNDER THE ADVOCATES ACT CAP. 341 R.E 2002 ambalo umeishutumu Mahakama kutotenda haki kwa Wakili Fatma Karume ambaye amekuwa akitukana Majaji, Mawakili wenzake na Viongozi wa Kitaifa.

Tunafahamu, wewe ulichaguliwa kuwa Raisi wa Chama Cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) kwa kuwa ulionesha ungekuwa wa kuleta mabadiliko makubwa ndani ya TLS.

Kwa wajuzi wa mambo, wakati unachaguliwa, wengi waliona kuwa labda ni kweli una kusudi jema kwa Taasisi hii nyeti katika Tasnia ya Sheria Nchini na tunakumbuka hata Tundu Lissu alituma Waraka Maalumu kuwataka Wana TLS kukuchagua wewe na Fatma Karume ambaye alikuwa Raisi wa TLS wakati huo ambaye naye alikupigia debe sana.

Pamoja na kutuahidi kutoifanya TLS chombo cha kisiasa na kiuana harakati, sasa tuna mashaka makubwa kuhusu uwezo wako wa kulinda heshima ya chama. Umeshindwa kuleta hiyo heshima na sasa umevaa viatu vya watangulizi wako Tundu Lissu na Fatma Karume kuanza kuifanya hata Mahakama idharaulike.

Kwa muda mfupi tu wa uongozi wako, umeanza kujidhihirisha kuwa kamwe huwezi kuwa tofauti na watangulizi wako. Muda mwingi umeonekana kuendelea kuifanya TLS yetu kuwa kijiwe cha Siasa na hakika imepoteza sifa hata mbele ya Jamii.

Hivi, sisi Mawakili na TLS inaposhiriki kuwakashfu Majaji au kuuunga mkono Mawakili wenzetu waliokosa nidhamu kwa Mahakama, nini maana yake?.

Tarehe 20 Septemba, 2019, Mhe. Jaji Kiongozi alitoa uamuzi katika Kesi inayomhusu Bw. Ado Shaibu dhihi ya Mhe. Rais na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika Kesi hiyo, pamoja na mambo mengine, Mhe. Jaji Kiongozi alitoa amri ya kumsimamisha Uwakili Wakili Fatma Karume kutokana na yeye kutumia lugha isiyofaa kwenye nyaraka za Kimahakama. Mamlaka hayo yapo kwa Jaji Mkuu na Majaji wa Mahakama Kuu kwa mujibu wa KIfungu cha 22(2) (b) cha Sheria ya Mawakili sura ya 314 ya Sheria za Tanzania.

Hukumu hiyo wakati inatolewa, Bibi Fatma Karume hakuwepo Mahakamani. Cha kusikitisha, hata kabla ya kupata hukumu husika, Bibi Fatma Karume ambaye ni wakili wa muda mrefu, anayejua taratibu za Kimahakama na aliyewahi kuwa Raisi wa Chama cha Mawakili, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kutoa lugha za Kashfa na kukebehi Mahakama.

Bibi Fatma Karume alisikika katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BBC, VOA nk akitukana Majaji wa Mahakama Kuu ikiwemo Jaji Mkuu nk.

Kabla ya hapo, Fatma Karume pia amekuwa akitumia mitandao ya Twitter kwa akaunti yake ya jina la Shangazi kutukana viongozi wa nchi ikiwemo Majaji. Kumbukumbu zetu zinabainisha kuwa, Januari mwaka huu 2019, Fatma alimtukana sana Msajili wa Mahakama Kuu mheshimiwa Sarwat baada ya Mahakama kutoa maelekezo kwake juu ya namna bora ya yeye kuwasilisha maombi ya Mteja wake Mhe. Zitto Kabwe.

Kashfa zote kwa Viongozi wa Mahakama alizotoa Fatma zipo mitandaoni. Fatma Karume aliendelea kutoa kashfa kwa Jaji Mkuu, alimtukana Mhe. Jaji Matupa mara tu baada ya kutolewa kwa uamuzi kwenye Shauri lililofunguliwa na Mhe. Lissu ambalo yeye Fatma hakuwa hata wakili katika kesi hiyo.

Tunatambua kuwa, katika kutenda kazi, sisi Mawakili tunaongozwa na Sheria. Sheria ya Mawakili inayosimamia Taaluma inaweka misingi ya maadili ya Mawakili na misingi mingine ya maadili ipo pia katika Kanuni za Maadili za Mawakili za mwaka 2018 ambazo zinazuia Mawakili kutoa lugha za matusi, kebehi, dharau, kashfa au kubeza Mawakili wengine, Mahakama au Mtu yeyote katika Jamii. Fatma anajua hilo na Dr. Nshala unafahamu wazi.

Tulitarajia kuwa, kwa kuwa Majaji hawana sehemu ambapo wanaweza kusikilizwa, Dr. Nshala na TLS mlipaswa kwanza kabla ya kutoa Waraka wa Tarehe 23 Septemba, 2019 kukosoa maamuzi ya Mahakama kumsimamisha Bibi Fatma kwa kile mnachodai kutosikilizwa, mngemkemea Fatma Karume kwa kudharau Mahakama na kutukana Majaji na Viongozi wa Nchi hii.

Kukaa kimya kwa Baraza la TLS kutochukua hatua dhidi ya Fatma Karume na badala yake kuishambulia Mahakama kwa Taarifa kwa Umma ambayo inarejea Maamuzi mbalimbali ya Mahakama kuhusu haki ya Fatma Karume kusikilizwa, ni wazi kuwa TLS ina maslahi binafsi katika jambo hili na masilahi hayo yanatokana na Dr. Nshala kutumika kama Mwanaharakati ndani ya Chama.

Tunaomba sana Dr. Nshala usiitumie TLS kama kichaka cha watu wasio na Maadili. Tambua kuwa TLS japo ni chombo cha Wanachama, iliundwa na Serikali mwaka 1947 wakati wa Mkoloni na imeendelea kuwa chombo cha Serikali daima. Kama hutambui hilo, Soma kifungu cha 29 cha Sheria ya Tanganyika Law Society Sura 370 ambacho kinataka Baraza la TLS kutuma Mkaguzi aliyeidhinishwa na Waziri wa Fedha kufanya ukaguzi wa hesabu wa chama hicho na hesabu hizo zinapaswa kufikishwa Bungeni.

Cha kushangaza, TLS haijawahi kuwasilisha hesabu zake kwa Waziri wa Fedha, hali hii inatufanya sasa kuiomba Serikali iitake TLS kuwasilisha Hesabu zake kwa Waziri wa Fedha hii iwe kwa hesabu zote kutokea TLS ilipoanza mpaka sasa ili uhakiki ufanyike kujua fedha zinazoingia na kuliwa kwa kivuli cha Chama huru.

Dkt Rugemeleza, TLS isiongozwe kwa kiuana harakati na usitumie kivuli cha Chama chetu kupitishia mambo yako binafsi.

Majaji walipotukanwa na wanapoendelea kutukanwa, kwa nini TLS haitoi Tamko lolote badala yake inatoa Tamko la kuilamu Mahakama kwa uamuzi wake dhidi ya Fatma Karume kufungiwa kwa utovu wa nidhamu?.

Je, Dr. Nshala na Baraza letu la TLS unakubaliana na jinsi Fatma Karume anavyotukana na kudhalilisha Viongozi wakuu wa nchi, Majaji, Mwanasheria na watu wengine? Kwa nini hamumkemei kwa utovu wake huo wa nidhamu ili kulinda heshima ya viongozi wetu na Mahakama?.

Dr. Nshala, kutojitokeza kwako hadharani kwako hadharani wewe na Baraza lako kuilaumu Mahakama kwa kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu unaofanywa na Fatma Karume, inaonesha wazi kuwa wewe ni sehemu ya ukiukwaji huo wa maadili na utovu wa nidhamu unaoendelea wa Mawakili.

Dr. Nshala, kutokemea kwako utovu wa nidhamu wa Mawakili unaofanywa wazi wazi na Fatma ni dhahiri kuwa na wewe unaafikiana kuwa Mahakama ziendelee kudharaulika na watu wasiofahamu hadhi ya Mahakama. Kitendo hicho hakikuachi salama wewe kama Wakili na Afisa wa Mahakama

Dr. Nshala, unaweza kuonekana ni mnafiki kwenda Mahakamani ukawaita Majaji waheshimiwa wakati unafurahia pale wanapotukanwa na huchukui hatua dhidi ya wanachama wako na badala yake unasaini Tamko la Kuishutumu Mahakama!!.

NI SISI MAWAKILI WA KUJITEGEMEA NA WANACHAMA WA TLS TUNAOUMIZWA NA YANAYONDELEA NA WEWE KUUNGA MKONO
 
Mleta mbona hujaambatanisha hayo matusi au hata screenshot za hayo matusi maana wewe wakili inabidi usiwe biased inabidi uwe fair unaposema sarwat alitukanwa kwanini hata usi quote hayo unayoyaona wewe ni matusi..chombo fair lazima kiwe neutral au wewe ni mawakili wa serikali sema unajificha tu nyuma
 
Pia mimi natamani kuona hayo matusi.
 
[In Nyerere's Voice]

"Popote ukimtaja T. Lisu kwenye mambo ya kipumbavu basi moja kwa moja unaonyesha upumbavu wako wazi wazi kabsa, nasema wazi wazi kabsa kabsa watu watajua wewe ni Mpumbavu na huna la kufanya zaidi ya kufanya upumbavu huo..

Ndugu zangu Tundu Lisu ni mtu muhimu na kafanya mambo makubwa makubwa katika nchi yetu..

Kwanza katoa elimu ya utambuzi wa kisheria na self awareness..

TL amekuwa mstari wa mbele kukemea hasa viongozi wanaoenda kinyume na katiba ya nchi

TL amekuwa mtetezi wa wanyonge hasa katika maswala ya kisheria, ni mtu asiyependa watu waonewe..

Kwa hiyo kwa mtu yeyote anayefata angalau nukta tu za huyu mtu naye lazmaa tumweke kwenye watu majasiri na muhimu katika ustawi wa nchi..

Na watu hao ni Fatma Karume na Rais wa sasa TLS , watu hawa ni muhimu..

Sasa wanaojitokeza kuwapinga waje na hoja za MSINGI na si kubadilisha au kuwawekea maneno ambayo either hawakuyasema na wala hawakuyafikiria kuyasema..

Kama watasema jambo lolote ambalo halipo kwa nia ya kuwaangusha basi wajiandae kuanguka wao ..."
 
Huyo ni rafiki kindaki ndaki na Tundu Lisu, na utundu lisu ni moja ya agenda zake.

TLS sio taasisi ya kitaaluma tena limeshageuka uwanja wa vita wa wanasiasa.
 
Kila mtu anapenda kutafuta Kiki lakini kwa Sasa watanzania sio wajinga, wengi wanaweza kuyapima mambo hivyo watu kujifanya wanaitetea jamii ya watanzania tofauti na uhalisia wanaonekana kituko. Watu kutokuandika sio kwamba hawana Cha kuandika, hebu tubadilike Mara zote ukweli ni mchungu hivyo inahitaji moyo kuukubali. Watanzania wanatazama Kila Jambo kwa jicho pevu ila NI wapole usifikiri hawaelewi Kama unvyopambanua mambo hapo juu.Tafakari kabla ya kuandika unachokiandika.
 
Mleta mada mbona hukujitokeza kukemea shambulio dhidi ya wakili mwenzio Lisu alipopigwa risasi?
 
Dkt Rugemeleza Nshala, sisi wanachama wenzio wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) tunakuandikia kwa masikitiko makubwa sana kuhusu malalamiko yafuatayo:
Tumesikitishwa sana na Tamko lako la tarehe 23 Septemba, 2019 ulilotoa kwa Umma lenye kichwa cha habari kinachosomeka TLS GOVERNING COUNCIL STATEMENT POWERS OF CHIEF JUSTICE AND HIGH COURT JUDGES TO SUSPEND ADVOCATES UNDER THE ADVOCATES ACT CAP. 341 R.E 2002 ambalo umeishutumu Mahakama kutotenda haki kwa Wakili Fatma Karume ambaye amekuwa akitukana Majaji, Mawakili wenzake na Viongozi wa Kitaifa.
Tunafahamu, wewe ulichaguliwa kuwa Raisi wa Chama Cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) kwa kuwa ulionesha ungekuwa wa kuleta mabadiliko makubwa ndani ya TLS.
Kwa wajuzi wa mambo, wakati unachaguliwa, wengi waliona kuwa labda ni kweli una kusudi jema kwa Taasisi hii nyeti katika Tasnia ya Sheria Nchini na tunakumbuka hata Tundu Lissu alituma Waraka Maalumu kuwataka Wana TLS kukuchagua wewe na Fatma Karume ambaye alikuwa Raisi wa TLS wakati huo ambaye naye alikupigia debe sana.
Pamoja na kutuahidi kutoifanya TLS chombo cha kisiasa na kiuana harakati, sasa tuna mashaka makubwa kuhusu uwezo wako wa kulinda heshima ya chama. Umeshindwa kuleta hiyo heshima na sasa umevaa viatu vya watangulizi wako Tundu Lissu na Fatma Karume kuanza kuifanya hata Mahakama idharaulike.
Kwa muda mfupi tu wa uongozi wako, umeanza kujidhihirisha kuwa kamwe huwezi kuwa tofauti na watangulizi wako. Muda mwingi umeonekana kuendelea kuifanya TLS yetu kuwa kijiwe cha Siasa na hakika imepoteza sifa hata mbele ya Jamii.
Hivi, sisi Mawakili na TLS inaposhiriki kuwakashfu Majaji au kuuunga mkono Mawakili wenzetu waliokosa nidhamu kwa Mahakama, nini maana yake?.
Tarehe 20 Septemba, 2019, Mhe. Jaji Kiongozi alitoa uamuzi katika Kesi inayomhusu Bw. Ado Shaibu dhihi ya Mhe. Rais na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika Kesi hiyo, pamoja na mambo mengine, Mhe. Jaji Kiongozi alitoa amri ya kumsimamisha Uwakili Wakili Fatma Karume kutokana na yeye kutumia lugha isiyofaa kwenye nyaraka za Kimahakama. Mamlaka hayo yapo kwa Jaji Mkuu na Majaji wa Mahakama Kuu kwa mujibu wa KIfungu cha 22(2) (b) cha Sheria ya Mawakili sura ya 314 ya Sheria za Tanzania.
Hukumu hiyo wakati inatolewa, Bibi Fatma Karume hakuwepo Mahakamani. Cha kusikitisha, hata kabla ya kupata hukumu husika, Bibi Fatma Karume ambaye ni wakili wa muda mrefu, anayejua taratibu za Kimahakama na aliyewahi kuwa Raisi wa Chama cha Mawakili, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kutoa lugha za Kashfa na kukebehi Mahakama.
Bibi Fatma Karume alisikika katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo BBC, VOA nk akitukana Majaji wa Mahakama Kuu ikiwemo Jaji Mkuu nk.
Kabla ya hapo, Fatma Karume pia amekuwa akitumia mitandao ya Twitter kwa akaunti yake ya jina la Shangazi kutukana viongozi wa nchi ikiwemo Majaji. Kumbukumbu zetu zinabainisha kuwa, Januari mwaka huu 2019, Fatma alimtukana sana Msajili wa Mahakama Kuu mheshimiwa Sarwat baada ya Mahakama kutoa maelekezo kwake juu ya namna bora ya yeye kuwasilisha maombi ya Mteja wake Mhe. Zitto Kabwe.
Kashfa zote kwa Viongozi wa Mahakama alizotoa Fatma zipo mitandaoni. Fatma Karume aliendelea kutoa kashfa kwa Jaji Mkuu, alimtukana Mhe. Jaji Matupa mara tu baada ya kutolewa kwa uamuzi kwenye Shauri lililofunguliwa na Mhe. Lissu ambalo yeye Fatma hakuwa hata wakili katika kesi hiyo.
Tunatambua kuwa, katika kutenda kazi, sisi Mawakili tunaongozwa na Sheria. Sheria ya Mawakili inayosimamia Taaluma inaweka misingi ya maadili ya Mawakili na misingi mingine ya maadili ipo pia katika Kanuni za Maadili za Mawakili za mwaka 2018 ambazo zinazuia Mawakili kutoa lugha za matusi, kebehi, dharau, kashfa au kubeza Mawakili wengine, Mahakama au Mtu yeyote katika Jamii. Fatma anajua hilo na Dr. Nshala unafahamu wazi.
Tulitarajia kuwa, kwa kuwa Majaji hawana sehemu ambapo wanaweza kusikilizwa, Dr. Nshala na TLS mlipaswa kwanza kabla ya kutoa Waraka wa Tarehe 23 Septemba, 2019 kukosoa maamuzi ya Mahakama kumsimamisha Bibi Fatma kwa kile mnachodai kutosikilizwa, mngemkemea Fatma Karume kwa kudharau Mahakama na kutukana Majaji na Viongozi wa Nchi hii.
Kukaa kimya kwa Baraza la TLS kutochukua hatua dhidi ya Fatma Karume na badala yake kuishambulia Mahakama kwa Taarifa kwa Umma ambayo inarejea Maamuzi mbalimbali ya Mahakama kuhusu haki ya Fatma Karume kusikilizwa, ni wazi kuwa TLS ina maslahi binafsi katika jambo hili na masilahi hayo yanatokana na Dr. Nshala kutumika kama Mwanaharakati ndani ya Chama.
Tunaomba sana Dr. Nshala usiitumie TLS kama kichaka cha watu wasio na Maadili. Tambua kuwa TLS japo ni chombo cha Wanachama, iliundwa na Serikali mwaka 1947 wakati wa Mkoloni na imeendelea kuwa chombo cha Serikali daima. Kama hutambui hilo, Soma kifungu cha 29 cha Sheria ya Tanganyika Law Society Sura 370 ambacho kinataka Baraza la TLS kutuma Mkaguzi aliyeidhinishwa na Waziri wa Fedha kufanya ukaguzi wa hesabu wa chama hicho na hesabu hizo zinapaswa kufikishwa Bungeni.
Cha kushangaza, TLS haijawahi kuwasilisha hesabu zake kwa Waziri wa Fedha, hali hii inatufanya sasa kuiomba Serikali iitake TLS kuwasilisha Hesabu zake kwa Waziri wa Fedha hii iwe kwa hesabu zote kutokea TLS ilipoanza mpaka sasa ili uhakiki ufanyike kujua fedha zinazoingia na kuliwa kwa kivuli cha Chama huru.
Dkt Rugemeleza, TLS isiongozwe kwa kiuana harakati na usitumie kivuli cha Chama chetu kupitishia mambo yako binafsi.
Majaji walipotukanwa na wanapoendelea kutukanwa, kwa nini TLS haitoi Tamko lolote badala yake inatoa Tamko la kuilamu Mahakama kwa uamuzi wake dhidi ya Fatma Karume kufungiwa kwa utovu wa nidhamu?.
Je, Dr. Nshala na Baraza letu la TLS unakubaliana na jinsi Fatma Karume anavyotukana na kudhalilisha Viongozi wakuu wa nchi, Majaji, Mwanasheria na watu wengine? Kwa nini hamumkemei kwa utovu wake huo wa nidhamu ili kulinda heshima ya viongozi wetu na Mahakama?.
Dr. Nshala, kutojitokeza kwako hadharani kwako hadharani wewe na Baraza lako kuilaumu Mahakama kwa kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu unaofanywa na Fatma Karume, inaonesha wazi kuwa wewe ni sehemu ya ukiukwaji huo wa maadili na utovu wa nidhamu unaoendelea wa Mawakili.
Dr. Nshala, kutokemea kwako utovu wa nidhamu wa Mawakili unaofanywa wazi wazi na Fatma ni dhahiri kuwa na wewe unaafikiana kuwa Mahakama ziendelee kudharaulika na watu wasiofahamu hadhi ya Mahakama. Kitendo hicho hakikuachi salama wewe kama Wakili na Afisa wa Mahakama
Dr. Nshala, unaweza kuonekana ni mnafiki kwenda Mahakamani ukawaita Majaji waheshimiwa wakati unafurahia pale wanapotukanwa na huchukui hatua dhidi ya wanachama wako na badala yake unasaini Tamko la Kuishutumu Mahakama!!.
NI SISI MAWAKILI WA KUJITEGEMEA NA WANACHAMA WA TLS TUNAOUMIZWA NA YANAYONDELEA NA WEWE KUUNGA MKONO
Sugu alitolewa Bungeni kwa nguvu za ziada zilizosababisha uharibifu wa kipazasauti kwa madai ya kumtukana Waziri Mkuu, Sugu alifunguliwa mashitaka polisi na kufikishwa mahakamani. Sugu alisikilizwa na mahakama na kuonekana hakumtukana Waziri Mkuu hivyo akaachiwa. Jaji ni mtendaji mkuu kwenye mahakama na anajua taratibu za tuhuma kwa mtuhumiwa kuwa hatakiwi kuhukumiwa bila ya kusikilizwa na ni ajabu kuona eti wewe wakili haukubaliani na maoni ya Rais wa TLS kuwa Karume lazima asikilizwe; Nina mashaka kama kweli wewe ni wakili.
 
Tulitegea wewe mwanasheria ujue hatua za kuchukua dhidi ya hayo matusi yanayotolewa na sehemu ya ya kupata hiyo haki yako ni mahakamani badala ya kulialia hapa jf!
 
Back
Top Bottom