Dr. Ramadhan Dau, Asharose Migiro na Mathias Chikawe wateuliwa kuwa Mabalozi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Ikulu.PNG


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi Ia Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.

Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

1. Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

2. Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki.

Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

3. Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ).

4. Kamishna Msaidizi Mwanda mizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongozaIdara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasiiliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzwake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaa nzia leo tarehe 15 Februar i, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenziwa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam
15 Februari,2016


1455542632587.jpg


1455542648889.jpg
 
Mpango ule ule wa kupeana zawadi as if Tanzania haina vijana! Ni lipi Dr. Dau,Migiro na Chikawe wanatuongezea kwenye Dunia hii inayoenda Kasi.
Wapeni vijana wadadisi na wenye damu kuchemka watatufungulia milango mingi mipya ya kuchangamana na wenzetu walioendelea. Sie wenye wivu wa kike wacha tuendelee kulalama.


cc. Mzee Mwanakijiji
 
Mpango ule ule wa kupeana zawadi as if Tanzania haina vijana! Ni lipi Dr. Dau,Migiro na Chikawe wanatuongezea kwenye Dunia hii inayoenda Kasi.
Wapeni vijana wadadisi na wenye damu kuchemka watatufungulia milango mingi mipya ya kuchangamana na wenzetu walioendelea. Sie wenye wivu wa kike wacha tuendelee kulalama.


cc. Mzee Mwanakijiji

Kwani nani kasema nchi ni ya vijana tu? Na uwape vijana nafasi gani za Ubalozi au Ukamishna wa Polisi. Kwani uongozi unatolewa kama zawadi.

Wote waliotajwa hapo tayari wana uzoefu wa kutosha tu katika uongozi; ukiondoa Dau ambaye anaingia kwenye utumishi wa kidiplomasia kwa mara ya kwanza wengine wote hao sioni tatizo. Kijana gani ulitaka ateuliwe kuwa Balozi ili isifiwe tu "kijana kapata"?

Uongozi huu hauangalii umri na haupaswi kuangalia umri kama kigezo cha kwanza. Hili tulishalikataa miaka mingi nyuma sijui kwanini bado watu mnaangalia umri!
 
Walewale eti mabadiliko vijana wapo unawapa hao hao mtoto wa Tandale lini utakuwa kiongozi hata kwenye mashirika ya umma eti unajiita ccm
 
Rais hebu kumbuka na viajana basi maana hao unao wateua walisha chuma vya kutosha, hivi uanataka baadhi ya watu waozee serikalini?

Wengine toka enzi za Mkapa mpaka leo bado wako serikalini mnachokifanya ni kuwabadilishia vyeo tu leo yuko hapa kesho yuko pale, badilika ujitofautishe na wenzako.

Nakumbuka wakati wa kampeni zako ulikataa suala la Experience ambalo ni kikwazo kwa vijana lakini mbona unafanya yale yale mh.
 
Dr. Kipilimba angepumzishwa kama wengine aliruhusuje, epa, escrow na madili mengi ya hela kutoka hovyo pale?
 
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Hapa kwa dau kafanya ujanja kweli, maana unamuondoa alafu unaanza kuiangalia NSSF akiwa hayupo japo atakuwa kapandikiza 'walinzi' wake. Kwa Dr. Migiro nailiangalia kwa jicho la tatu, inakuwaje mtu atoke cheo cha naibu katibu mkuu wa UN alafu awe balozi. Tufafanulie wajuzi wa mambo ya promotion na demotion tafadhali.

Ukweli mkuu ni kuwa ukiangalia majina ni yale yale yaliyotufikisha kwenye hali ambayo JPM mwenyewe anailalamikia siku zote 101 alizokaa Magogoni!
 
Back
Top Bottom