Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Nimejitahidi sana kufuatilia hotuba za marais mbalimbali duniani waliopita na waliopo madarakani. Zaidi ya hapo nimejitahidi kufuatilia maongezi mbalimbali ya wasomi mbalimbali duniani nimegundua kuwa katika kujenga hoja mbalimbali wamekuwa wakitumia mifano mbalimbali ya matukio ya nyuma, maandiko ama tafiti mbalimbali zilizofanywa hapo nyuma, pamoja na theories (nadharia) mbalimbali za wasomi waliotangulia.
Nimejitahidi kufuatilia hotuba za Rais wangu Jakaya Mrisho Kikwete toka akiwa Waziri wa mambo ya nchi za nje na mpaka sasa Rais, sijabahatika kumsikia akinukuu kitabu, tafiti wala theory yeyote duniani kitu ambacho ni tofauti na wasomi wote duniani.
Kwahili sitaki kuamini kuwa JK ni msomi na anajua kila kitu hana haja ya kunukuu taaluma za wasomi wengine, bali napata mashaka kiasi kwa sababu mzee wetu anashahada ya Uchumi, sitaki kuamini hata ile theory ya DEMAND & SUPPLY anashindwa kuichomekea popote katika hotuba zake.
Mara nyingi nimekuwa nikimsikia hata katika vitu ambavyo ni quantifiable (vinavyohesabika) mwenzetu huyu amekuwa akivitamka anavyojua mwenyewe. Mfano, katika hotuba yake ya Juzi mzee alishindwa kutaja jumla ya pesa waliokuwa wakigawiwa wanufaika mbalimbali katika account ya Escrow balada yake alikuwa anasema Anna tibaijuka alipewa sh. bilion 1 na "ushee".
Kwa wale wataalamu wa Mahesabu ya kifedha jaribuni kutoa elimu ili tusiendelee kuchezea taaluma za watu.