Dr. Omar Nundu (mbunge) awasha moto Tanga

Dr. Omar Nundu (mbunge) awasha moto Tanga

Nurdin said

Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
29
Reaction score
3
Mwana JF na Mbunge wa jimbo la TANGA MJINI MH Omari R Nundu, AMEITAKA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA INAWATENGEA VIJANA NA AKINA MAMA PESA ZA HALMASHAURI ZILIZOTAKIWA ZITENGWE KUANZIA MWAKA 1993 AMBAPO KWA MKOA WA TANGA ZIMETOLEWA MIAKA MITATU TU HUKU MIAKA 18 ILIYOFUATA ZIKIWA HAZITOLEWI NA AU KUTOKUTENGWA KABISA.

MH. NUNDU AMBAE ANATUMIA AHADI YA 4 NA 8 ZA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA KULIENDESHA JIMBO LA TANGA AMEWATAKA VIJANA KUTOKUDANGANYWA KUWA YEYE NDIE ANAYEZUIA MIKOPO HIYO ISITOKE BADALA YAKE AMEWATAKA VIJANA NA AKINA MAMA WA MKOA WA TANGA KUCHANGAMKIA FURSA HIYO AMBAYO NI YA KILA KIJANA BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA.

MH.NUNDU ALIFIKA MBALI SANA KWA KUWATAKA VIJANA WAJIJENGEE KUAMINIKA MARA WATAKAPOPATA MIKOPO HIYO KWA KUHAKIKISHA WNAITUMIA KWA MALENGO.

IKUMBUKWE MBUNGE OMAR R. NUNDU ALISAMEHE MSHAHARA WAKE WA MIAKA MITANO ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 111 KWA KUWAKOPESHA WAKAZI WATANGA ILI WAJIKWAMUE KIUCHUMI NA WAONDOKANE NA LINDI LA LA UMASIKINI ULIOPO MKOANI HAPA,PAMOJA NA JUHUDI HIZO PESA HIZO ZILIRUDI MILIONI NANE NA IDADI KUBWA YA WALIOKOPESHWA WAKISHINDWA KUZIRUDISHA KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI IKIWEMO WATU WANAOPITA WAKISEMA PESA ZA MBUNGE HUYO ZILIKUWA ZA MISAADA.

MBUNGE OMAR NUNDU ANABAKI KUWA MBUNGE WA KWANZA KATIKA HISTORIA YA MKOA WA TANGA KUSAMEHE MSHAHARA WAKE KWA AJILI YA KUWAKOMBOA WANANCH
 
Last edited by a moderator:
Tanga kuendelea kuikumbatia CCM mtabaki kuwa Masikini Mpaka mwisho wa Dunia
 
2015 ileeee,naona washaanza mbwembwe sasa wataanza kutuamkia hawa kutuita waheshimiwa
 
Nundu mtetezi wa wanyonge tanga wanamuogopa sana maana anasimamia ukweli
tanga zindabaa

Pesa hizi ameanza kuzitetea tangu mwaka 2012 ila halmashauri ya jiji ndi wamekuwa na uzembe katika kutenga na hili suala ni la kitaifa na mh.rais jakaya kikwete ameagiza ikifika desemba 31 mwaka kila halmashauri ieleze fedha zilizotengwa zimewasaidiaje vijana na akina mama.

Nundu ni mchapa kazi na mwenye weledi na ndio maana nikasema anaongozwa na kanuni makini za chama chake kanununi namba 4 na 8 zisome katika katiba ya chama

Umoja ni nguvu ni wazi sasa chaguo tunalolihitaji kwa tanga ni kiongozi makini na mtetezi wa wananchi.

Sasa tunasonga na kauli mbiu tanga kwanza vyama baadae
 
Nachotaka kukwambia bado asilimia 95 ya wananchi wana imani na nundu na wanajua aliondolewa kimakosa
mbona alipokuwa rais wa anga dunia hakufanya ufisadi mnaouzungumza
 
2015 ileeee,naona washaanza mbwembwe sasa wataanza kutuamkia hawa kutuita waheshimiwa

tatizo sio 2015 na hapa sio kampeni huu ni ukweli ambao hata ww katika m eneo lako unatakiwa ufuatilie hizi pesa kumbuka ni mpango wa serikali uliokubaliwa na bunge tangu mwaka 1993
 
tatizo sio 2015 na hapa sio kampeni huu ni ukweli ambao hata ww katika m eneo lako unatakiwa ufuatilie hizi pesa kumbuka ni mpango wa serikali uliokubaliwa na bunge tangu mwaka 1993

Hilo tatizo ndo kaliona leo toka alipokuwa waziri? Hapo target ni 2015 tu hakuna kingine
 
Nurdin said

Namaini unaweza ukawa mtu wa karibu na Mbunge, Mwabie aangalie jinsi ya kufanya Tanga Tech kiwe chuo kikuu cha ufundi kama ilivyo Mbeya leo, hakika kwa eneo amabalo tanga tech ipo na hakika wana eneo kubwa sana, inaweza kusaidia sana kiuchumi wakazi wa tanga Mjini maana kuna uwezekano wakuwepo mzunguko mkubwa wa pesa ambao utasaidia kukwamua wenyeji wanozunguka hiko chuo, ambacho aridhi yake kubwa imebaki Vichaka na pori tena kati kati ya Mji.
 
Huyu nae anataka uraisi au anaupalilia ubunge wake..?
 
Nurdin said

Namaini unaweza ukawa mtu w akaribu na Mbunge, Mwabie aangalie jinsi ya kufanya Tanga Tech kiwe chuo kikuu cha ufundi kama ilivyo Mbeya leo, hakika kwa eneo amabalo tanga tech ipo na hakika wana eneo kubwa sana, inaweza kusaidia sana kiuchumi wakazi wa tanga Mjini maana kuna uwezekano wakuwepo mzunguko mkubwa wa pesa ambao utasaidia kukwamua wenyeji wanozunguka hiko chuo, ambacho aridhi yake kubwa imebaki Vichaka na pori tena kati kati ya Mji.

nitalifikisha ombi lako ni muhimu kuikuza tanga na hilo eneo ambalo ni pori palichukuliwa na muwekezAji ambae hajapanyia kazi jitihada zinafanyika kubadilisha matumizi.
 
hujui tanzania ni shamba la bibi?

twende na uhalisia na tuwe makini katika kuitafsiri nchi yetu
tambua kuwa wabadhirifu wachache ndo wanaturudisha nyuma
ila mpaka sasa nundu,kangi lugola,kigwangala,nchemba,lekule leiza wanabaki kuwa wazalendo
 
Yaani Tanga hadi inatia huruma. Serikali ya CCM imeizika kabisa Tanga na kubaki kupiga porojo tu za kuombea kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Ova
 
Jamaa anaona 2015 inakaribia....nywele anazitia maji
 
nitalifikisha ombi lako ni muhimu kuikuza tanga na hilo eneo ambalo ni pori palichukuliwa na muwekezAji ambae hajapanyia kazi jitihada zinafanyika kubadilisha matumizi.

PORI ?
Mkuu sizungumzii Kiwanda cha Mbolea, nazungumzia tanga tech, wana eneo kubwa sana na linatosha kujenga chuo kikubwa kabisa.

au unataka kuniambia eneo la chuo hiko limechukuliwa?
 
Back
Top Bottom