Dr Njelekela mwanamke bora wa mwaka

Dr Njelekela mwanamke bora wa mwaka

Mujumba

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
853
Reaction score
306
MWENYEKITI wa Chama cha Wanawake Madaktari (Mewata), Dk. Marina Njelekela juzi alitunukiwa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Dk. Njelekela ambaye pia alishinda katika kipengele cha Mwanamke Bora katika Sekta ya Afya, katika nafasi hiyo alishindana na Dk. Mwale Malecela na Salome Yakieli.

Tuzo hizo ziliandaliwa na kutolewa na Kampuni ya matangazo na uhusiano wa umma, Frontline ambapo wanawake 24 walishindania tuzo hizo kupitia sekta mbalimbali.

Akizungumzia ushindi huo muda mfupi baada ya kukabidhiwa tuzo yake na Meneja wa Mradi wa Wanawake katika Umoja wa Mataifa hapa nchini, Anna Collins- Falk, Dk. Njelekela alisema tuzo hiyo imemuongezea moyo wa kutoa huduma ya afya kwa wananchi.
 
Kwa walio Jitokeza...ndio bora sio bora kwa wote...tupe na list za wengine walio shindanishwa tuone...vigezo na masharti kuzingatiwa.
 
Frontline ya Nancy Sumari na Irene Kiwia??? aya bwana.....

Hongera sana Dr....keep up the good work!
 
Kwa walio Jitokeza...ndio bora sio bora kwa wote...tupe na list za wengine walio shindanishwa tuone...vigezo na masharti kuzingatiwa.

I agree with you....hiyo title ni kubwa sana.....ningefurahi kujua alioshindanishwa nao na amefanya nini na kwa impact ya wangapi nchi hii?

Ishakuwa kwamba mtu akishateuliwa na Rais....ni mtoto wa fulani....anajuana na watu fulani basi anaweza pewa title yeyote......!!
 
Hongera zake kamanda. amesaidia kina mama kupitia mewata.

Dr Marina Njelekela Conferred The Martin Luther King, Jr. Drum Major for Justice Award, 2010
 
I agree with you....hiyo title ni kubwa sana.....ningefurahi kujua alioshindanishwa nao na amefanya nini na kwa impact ya wangapi nchi hii?

Ishakuwa kwamba mtu akishateuliwa na Rais....ni mtoto wa fulani....anajuana na watu fulani basi anaweza pewa title yeyote......!!

Trust me...Dr....bigwa wapo kibao...busy na kazi zao.....huyu profile yake kwa kweli inabidi iwekew hapa,hatuwezi tengua...kwanza hata frontline yenyewe hawa warembo ndio viongozi..sasa unategemea kuweza kumcredit Dr.Bigwa wa kisukari Mhimbili...kwanza hawezi hata jitokeza..Nawafahamu wengi tu wako busy kuhudumia wagonjwa..hawalali...akitoka kazini Muhimbili,anafundisha,anatibu at the same time asoma tena...achilia mbali kwenda hospitali zingine kutoka support.
 
Prevention is better than cure.

Naamini watu wa public health was impact kubwa kuliko Dr moja anayekimbizana na wagonjwa. Sipingi kazi ya madr wetu wanaohangaika kutibu.

Ni bora tuweke categories za zawadi hata kwenye hiyo health sector.
 
Hongera sana Marina kwa utendaji wako mzuri hadi kufanikiwa kupata tuzo kubwa kama hii. Hongera pia kwa Mwele na Salome kwa kuwemo katika Wanawake bora watatu nchini hii inatokana na juhudi zenu kubwa na utenaji mzuri wa kazi zenu. Hongereni sana.
 
Back
Top Bottom