DR Ndalichako na JOGRAFIA

mchukiaufisadi

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
546
193
Namshukuru Mh. Mbatia kwa kwa kunipunguzia fikra mbovu dhidi ya Dr. Ndalichako wa NECTA. Dr. Ndalichako alisoma shule na kuitambua JIOGRAFIA, hivyo NECTA wakitunga mitihani huwa wanatunga ya JIOGRAFIA na wasahishaji hutakiwa wasahishe mitihani ya JIOGRAFIA. Bahati mbaya Wizara ya Elimu wanafundisha watoto wetu JOGRAFIA na wakiingia kwenye mitihani wanajibu JOGRAFIA sio JIOGRAFIA na kuwafanya NECTA kuwapa ZERO maana wamejibu ambacho hawakuulizwa. Katika hali hii, ni vyema wakurugenzi wote katika Wizara ya Elimu pamoja na Katibu Mkuu watimuliwe wote na mwisho Waziri awajibike yeye mwenyewe bila kulazimishwa na Rais au wananchi.

Hapa ndipo alipojikwaa Mheshimiwa James Francis Mbatia (Mb)
Na. Huruma K. Joseph
Alipokuwa akichangia hoja ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mbunge wa Kuteuliwa Mheshimiwa Mhandisi James Francis Mbatia (katika makala hii atafahamika kwa kifupi kama Mheshimiwa) aliweka wazi udhaifu katika wizara ya elimu ambayo kwa kupitia kitengo chake ya kuidhinisha machapisho na vifaa vya elimu, ilikuwa imepitisha vitabu vyenye makosa.

Mbatia alianika makosa mbalimbali kutoka kitabu kimoja baada ya kingine. Vitabu hivyo ni kile cha hisabati kinachoonyesha sifuri ukigawa kwa sifuri jibu ni sifuri, na uwepo wa hesabu za kukokotoa senti wakati katika uhalisi wa maisha ya kila siku hatuna tena mambo ya senti senti. Pia alionesha kitabu cha uraia kinachosomeka kuwa mtaa hundwa na vitongoji na kuwa wakazi wake wengi ni waajiriwa. Aidha Mheshimiwa pia alikosoa kitabu kuandikwa Jografia badala ya Jiografia. Binafsi nilimwona kupitia runinga nikiwa macho kodokodo huku Waziri na Naibu wake wakiwa wamenywea. Nampongeza kwa utafiti huo ambao kwa kiasi umedhihirisha kuwa kuna watu wanaocheza na elimu ya watoto wetu. Kabla sijaendelea naomba nitangaze msilahi katika jambo hili. Mimi ni mwandishi wa vitabu vya kiada vinavyofikia 12 vinavyotumika katika shule za Tanzania. Kitabu changu mashuhuri (si cha kiada) ni kile cha "40 Big Lies in Civics for Tanzania schools" ambacho tarehe 4/6/2013 kiliingia rasmi kwenye hansard kupitia hotuba ya msemaji wa upinzani.

Pamoja na juhudi hizo za Mheshimiwa ambazo si za kubeza, lakini bado tunahitaji tafakuri tunduizi (critical thinking) ili kujiridhisha kama alikuwa sahihi katika maeneo aliyoyagusa.

Kufundisha senti
Kwa mfano, Mheshimiwa, anasema watoto hawana haja kufundishwa mambo ya senti kwa vile hazitumiki tena siku hizi Je, ni kweli kuwa senti hazitumiki? Itakumbukwa kuwa siku hiyo hiyo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba alitoa maelezo yafuatayo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CUF) Mh. Mhonga Said Ruhwanya "kupiga simu kutoka mtandao moja kwenda mwingine gharama imeshuka kutoka sh. 115 mwaka 2012 kwa dakika hadi kufikia sh. 34.92 Machi mwaka huu" sasa kudai kuwa senti hazitumiki unadhihirisha kuwa utafiti wa Mbatia katika swala hili ulikuwa kondefu. Je, Mbatia hafahamu kuwa katika Jumuiya ya Afrika ya mashariki ulinganifu wa bei za bidhaa mbalimbali hufanywa kwa dola ya kimarekani ambazo huambatana na senti. Kwa mfano takwimu za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zinaonyesha bei ya reja reja ya Nyama ya ng'ombe kwa kilo katika nchi wanachama ni kama ifuatavyo: Tanzania dola 3.17, Burundi dola 4.14, Uganda dola 3.17, Kenya dola 3.21, Rwanda dola 2.49, wastani EAC, dola 3.24. Tukiacha hayo ya Afrika Mashariki ambayo kila siku wabunge wanasema tuwaandae watoto wetu kwenda kushindana, swali jingine muhimu ni kweli kuwa mheshimiwa hajawahi kwenda katika duka la kubadilisha fedha (Bureade Change) na kukokotoa (au kukokotolewa) hesabu yenye senti. Sasa inakuwaje aseme watoto wetu wasifundishwe mambo ya senti?

Jiografia au Jografia
Jambo jingine la kujadili ni neno lipi ni sahihi kati ya Jiografia na Jografia. Kwa mujibu wa Mheshimiwa, Neno sahihi ni Jiografia. Hapa kuna sintofahamu. Wakati kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI inalitambua neno Jiografia, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) inalitambua neno Jografia. Aidha machapisho mbalimbali yanayotolewa na Taasisi ya Elimu (TIE) mojawapo ikiwa ni MUHTASARI WA MAFUNZO YA UALIMU WA ELIMU YA MSINGI NGAZI YA CHETI, pia inalitambua neno jografia. Ikumbukwe kuwa BAKITA ndiyo chombo ambacho ni "authoritative" (kwa sheria ya Bunge) katika lugha ya Kiswahili kikiwa juu ya TUKI. Ningekuwa naandika kitabu cha somo hilo, kamwe nisingelitumia neno Jiografia. Kufikia hapo naweza nikabashiri kwamba mhandisi huyu atataka kuona neno jiometri katika vitabu vya hisabati badala ya jometri, kitu ambacho si sahihi.

Wakazi wengi wa mtaa ni waajiriwa
Si makosa hata kitabu kusomeka kuwa wakazi wengi wa mtaa wameajiriwa na utumishi wa umma, viwanda na makampuni. Kwa mfano, wakazi wengi wa mtaa wa Unga limited (Arusha) wameajiriwa katika makampuni (ujenzi, maduka, hotel n.k), viwanda (bia, uchapaji, nguo nk), ofisi za umma na wengine wamejiajiri wenyewe. Msisitizo wa mwandishi wa kitabu ni kuonyesha kuwa katika maeneo ya mjini hakuna shughuli za kilimo.

Mitala kukuza watoto kijamii
Hainishangazi nisomapo kuwa Mtala wa elimu ya awali unamwezesha mwanafunzi kukua kiuchumi, kisiasa na kijammii. Achilia mbali mtala, mbona mtoto wangu aliyeko shule ya awali makuzi ninayompa nyumbani ni ya kumpa msingi/kumkuza katika nyanja mbalimbali za maisha. Maathalani ninapomwambia asichezee chakula ninamkuza kiuchumi. Shuleni hufunzwa human relation kwa kucheza na wenzake bila kgombana huku ni kumkuza kijamii.

Jina la mwandishi kuwa kampuni ya uchapishaji.
Katika mfumo wa uandhishi wa vitabu mwandishi yaweza kuwa taasisi au shirika, hivyo mahali pa jina litaonekana jina la taasisi/shirika hilo.

Maathalani kampuni ya uchapishaji pia inaweza kuwa author kwa maana ya kutumia rasilimali watu iliyonayo. Chuo kikuu cha Harvard kinafafanua vyema hili. When a book is authored by an organization rather than an individual, put an organization name. In APA styles, if the author and publisher are the same corporation/institution, list publisher as author .

Vitabu kukosa wasifu wa waandishi
Mheshimiwa alinukuliwa akisema, "hakuna hata kitabu kimoja chenye wasifu wa waandhishi, karibu vitabu vyote havina wahariri" Mheshimiwa angefanya utafiti mdogo tu angegundua kuwa hata vitabu vya shule za msingi vya nchi mbalimbali ikiwemo zile ziliozoendelea wasifu wa waandishi kwenye kitabu si kpaumbele, na isitoshe hata vitabu alivyokuwa akitumia mheshimiwa shule ya msingi, vile vya KIBANGA AMPIGA MKOLONI havikuwa na "majisifu" ya waandishi. Vitabu vya Yusuf Halimoja ambavyo ndivyo vilivyonipa hamu ya kuwa mwandishi havikuwa na wasifu wake hadi nilipokutana naye miaka ya karibuni na kunipa historia yake. Mwanafunzi hana haja na wasifu wa mwandishi. Kwa kawaida wasifu huhifadhiwa kwenye data base ya publisher. Kuhusu vitabu kutokuwa na wahariri, mimi sio msemaje wa wachapishaji wote, wao wenyewe waje waseme lakini katika makampuni niliyoandikia vitabu wahariri ( na wasaidizi wao) wapo na ninamawasiliano nao mara kwa mara katika ku -update facts. Hata hivyo utafiti uliofanywa na TAMNGSCO (2012) haukuonyesha kukosekana kwa wahariri bali ilipendekeza wahariri hao wasajiliwe na EMAC.

Pamoja na Mheshimiwa na dhamira nzuri ya kuonyesha kuwa kuna udhaifu mkubwa katika sekta ya elimu hadi kufikia EMAC kufutwa, ukweli unonyesha kuwa hata yeye "amebugi" kwa asilimia kubwa. Mwendo kasi aliokuwa nao umemfanya ajikwae. Naomba kutoa hoja.
Huruma K. Joseph ni mwandishi mkongwe wa vitabu nchini ambaye kwa sasa anayeishi Jijini Arusha. Mwendelezo wa makala hii utakuwa katika lugha ya kiingereza katika gazeti la Arusha Times. josephhuruma@gmail.com
 
utafiti wako umejikita katika majungu zaidi na wala siyo uhalisia wa jambo kwani majukumu ya Dr ndalichako kazi yake yeye ni kuhakikisha ya kuwa mitihani imetungwa vizuri na kusahihishwa vyema na wala siyo kusanifu majina ya masomo kuwa ni jografia au jiografia kwa sababu hujui utaendelea kutojua mpaka ubadili msimamo wako wa kutafuta ukweli pole sana katika kutafuta ukweli
 
Hapa ndo uvivu wetu wa kufikirisha akili zetu unapoonekana,mtoa mada kajieleza vizuri,wachangia mada tunahoji sentensi moja nayo bila kuielewa.Ni sawa ndo mitaala yetu inavyotuongoza labda.
 
mchukiaufisadi nisaidie kwanza hapa kabla sijachangia hii mada, tofaut kati ya JIOGRAFIA na JOGRAFIA ni ipi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom