Dr. Nchimbi: Wanaonung'unika sasa ni wasaliti

Dr. Nchimbi: Wanaonung'unika sasa ni wasaliti

mahwahwajr

Member
Joined
Jun 10, 2010
Posts
18
Reaction score
22
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr Emmanuel Nchimbi amesema wale wote wanaolalamika hivi sasa kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ni WASALITI.

Dr Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati kuu ya CCM amesema watu hao ni walafi wa madaraka na ni watu ambao hawana nia njema na wananchi na kamwe hawawezi kuleta mabadiliko wanayoyahubiri.

Amesema katika mchakato wowote kama waliokuwa nao, ni kawaida kuwa naz makundi yanayowaunga mkono wagombea mbalimbali lakini kwa watu wastaarabu makundi hayo hufa mara mgombea mmoja anapopatikana. Dr Nchimbi ambaye wakati wa mchakato kule Dodoma alitoka nje na kulalamikia uamuzi wa kuondoa baadhi ya majina, amesema CCM iko IMARA na kwamba mgombea aliyeteuliwa na chama Dr John Pombe Magufuli ni mchapa kazi hodari atakayeiletea nchi maendeleo.

"Mkifanya uteuzi, yeyote anayepinga baada ya hapo huyo ni MSALITI," alisema na kuongeza..."Kipimo cha uaminifu wa mtu kwa chama ni wakati wa michakato migumu kama hii...hawa walioondoka wametudhihirishia kwamba hata wakati wakiwa ndani ya chama walikuwa ni wasaliti tu.."

Amemwagia sifa Dr John Pombe Magufuli kwa kusema ni mtu asiyekuwa na makuu na ndio maana wakati wa mchakato hakuwa na makundi kama wagombea wengine.

Dr Nchimbi alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la vIjana wa CCM jijini Dar es Salaam hapo jana.

Pia alimsifu Dr Magufuli kwa mchango mkubwa wa kufanikisha ujenzi wa jengo la UVCCM jijini Dar es Salaam wakati akiwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

<font size="3">


 
Last edited by a moderator:
Nchimbi yuko sahihi kabisa, sehemu yeyote penye ushindani kuna anayeshinda na anayeshindwa, kama wote wanaoshindwa watahamia chama au taasisi sijui ingekuwaje. Ila ukisikiliza sababu zao za kuhama ki-ukweli hazina mashiko......wakati mwingine njaa inawasumbua sana wanasiasa.
 
Sidhani kama ndo huyu aliyekataa kuburuzwa ndo sasa ameamua kulamba matapishi.

Njaa yake imempanda kichwani,atakosa yote.
 
anachokisemaaa nchimbi si.ndicho anachokiishii moyoni lowasaaa DAMUUUUUU am sureee hata iwejeeeeeeeeeeeee
 
Nchimbi yuko sahihi kabisa, sehemu yeyote penye ushindani kuna anayeshinda na anayeshindwa, kama wote wanaoshindwa watahamia chama au taasisi sijui ingekuwaje. Ila ukisikiliza sababu zao za kuhama ki-ukweli hazina mashiko......wakati mwingine njaa inawasumbua sana wanasiasa.
namheshimu kwa msimamo wake kwani hakunong'ona pembeni alisema siku ile ile na baadae akaamua kumuunga mkono magufuli. Kuliko wale waliokaa kimya kipindi chote na kumsubiri EL aamue.mtu kama kijana milya ambaye miaka miwili aliamua msimamo wake na kujiunga na CDM hao ni viongozi wa kweli na wanatembeya na maamuzi yao.
 
Kazi nzuri kwa Nchimbi!!Najua wakongwe wa JF mtanielewa
 
je ? mchakato ulikuwa huru ?
ulilamika ,leo unasema wasioridhika ni wasaliti. Hatareeeeee
 
Dr.Nchimbi alitumwa kum frastrate Lowassa, wale wote watatu Nchimbi, Kimbisa na Sophia Simba ni kitengo. Jk anasema Mabua huwahi Kuwaka kwa haraka na pia huzima kwa haraka, Akina Mgeja wanasema Rais kishachaguliwa,October 25 ni kwenda tu kutimiza Sharti la kisheria. YETU MACHO!!
 
Mwanasiasa akiongea mbele yako ujue anakutongoza-anaetongoza siku zote hasemi ukweli.
 
mahwahwajr

Hapo mwishoni,kumbe akiwa waziri wa ardhi ndo ajenge jengo la Uvccm?hii siyo kashfa nyingine kubwa kiongozi wa nchi unajenga jengo la chama??wiziiii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom