Dr Nchimbi apeta!!!!!

kweli hawa wabeba mabox hawana maana. Unajua wanadhani eti PhD mtu anaweza kugawiwa, tatizo la watanzania ni wavivu kufikiri, na ni wepesi kudanganywa, nani kwa kuambia doctorate mtu anapewa? lazima uchakarike ili kuipata.
 
Wengine tuna argue nao hapa na form leaver wakaenda kujilipua ulaya basi wanaona wote ni wajinga wenzao kumbe sie tunakuja kutembea huko tunapata good time na kurudi zetu home tukiwaacha wao utumwani ulaya na usa wakiishi kama third citizens.....maisha bwana wababu zetu walikuwa wanakimbia kwenda kulima usa utumwani vijana wa leo wanalilia kubaki utumwani.
 
Huyu jamaa ni moja kati ya viongozi ninaowachukia sana
 
Nchimbi kafanya nini cha maana? Acheni longolongo PhD sijui nini.

Tatizo letu bongo tunaabudu title, mtu anaulizwa kwa nini wewe unataka kuwa rais, anajibu kwa sababu nimekuwa waziri miaka 20, hakuambii kafanya nini miaka 20 hiyo, kuwa waziri tu ni qualifications.

Ndio hawa wengine, Nchimbi kafanya nini? "Ana PhD, we unafikiri PhD mchezo?" kafanya nini cha kumdistinguish, PhD is a mean to an end, what is the end results? Au anakusanya mi degree tu na yeye aonekane msomi wakati hajui maana halisi ya usomi?

Hii PhD na usomi wake ndio vimemfanya a decree kutaka vazi la taifa kwa kutumia kamati? Ndio usomi huo?
 
Hatuiti qualifications, tunaita 'credentials', na huyo Nchimbi wenu ni kuruta tu hapa.

PDF attachment will do.

Mkuu habari ya siku nyingi? Unapoteza nguvu zako bure tu!!! Kwani hata hiyo tofauti anaijua?
 
Huyu jamaa ni moja kati ya viongozi ninaowachukia sana
Pole sana Chain Smoker, inawezekana ulishawahi kugongana naye. Ila kwa ufupi jamaa ni mtu wa watu, hana makuu kabisa na sifa yake pekee ni kuwa karibu na watu wa rika zote bila kujali ukwasi wa kifedha. Kuna jamaa yangu rafiki yangu professor mmoja toka ulaya alibahatika kuwepo siku moja before graduation mzumbe alikutana na nchimbi lumumba complex, alishangaa sana kuona anavyowachangamkia watu wote na kuongea nao kwa upendo.
 

Kafanya cha maana kwa kuangalia trend ya watu hasa vendors na wafanyabiashara wadogo ambao amefanya utafiti wa namna gani imekuwa na impact ktk maisha yao ana pengine namna bora ya kuimprove upande wa watoa mikopo na wapokeaji mikopo.sasa wewe unaposema utafiti wake hauna msaada umetumia vigezo gani?
 

Kwanza kabisa ume assume tu kwamba nimesema utafiti wake hauna msaada, sijasema hivyo, unaonekana huna umakini katika kusoma na kuelewa.

Mtu akiuliza "kafanya la maana lipi?" Hajasema "Hajafanya la maana". Jua tofauti ya swali na statement.

Matokeo yake (ya kuangali kwake, kila mtu anaweza kuangalia, the question is who can change?) yamewezaje kusaidia watu? kwa kipimo gani?
 

Kuwa karibu na watu si sifa ya uongozi, hiki ni kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho.

Mbona tunafanya standards zetu ziwe chini hivi?

Hizi ndizo sababu za kumfanya mtu kuwa kiongozi? Anajua kujimix na watu? No wonder tunaishia kuwa na marais wa ajabu ajabu kama kina Kikwete. Walianza hivi hivi nao, mara wamekuwa pale Magogoni bila vision wala ambition yoyote zaidi ya ku hold power.
 
Nimeshindwa kukuelewa hapo kwenye RED, halafu kwa haraka haraka wewe ni miongoni mwa wale wenye akili mgando wakadhani usomi ni vyeti au umahili wa kukaa darasani kwa miaka mingi bila tija, hivi unaweza kuniambia Marehemu Mzee Karume alikuwa na PHD au Degree ngapi? na ni kwa nini Zanzibar mpaka leo anakumbukwa Karume na sio hawa wasomi wenye madegree?

Je kama degree ni hoja, vipi hizi PHD za akina Balali kuna vyuo watu wanasomea wizi na kuhujumu nchi zao?
U need wake up call, bado umelala usingizi mzito sana young man kwa Elimu yako ya kukalili.
Am proud to be form four certificate holder who can compete with Udom degree holders. am very proud of it!!
 
mmmmmh sina uhakika sana na ubora wa PhD ya Nchimbi, kwangu huyu si daktari, angeipata SUA ningeitambua kwa sana kwani najua userious ulioko SUA, kuna kina Kamala na PhD zao za Mzumbe Univ ambazo zina utata, Je ya mh Nchimbi ni safi?. Nchi hii tumezidi kuwatunuku wanasiasa PhD ndio maana wanawadharau wanataaluma na wataalamu, kwa jinsi hii kila kitu kinaendeshwa kisiasa hapa nchini.
 
Hivi haya majina ya watu uloyabandika hapa umepata idhini yao?
Ungewezaiandikia thread pasipokuweka hayo majina na ukaeleweka.

Nyway aksante kwa taarifa na Hongera Mh.
 

Kwanza ili niwe katika nafasi ya kujua swali lako lina maana gani ningependa na wewe uniambie umeifanyia nini tanzania mpaka hapo ulipofikia maana kila siku tunawasema viongozi alafu nitakwambia nchimbi kafanya nini yeye
 

Wala sidhani wewe upo katilka kipimo cha mtu kuwa au kutokuwa daktari......wataalamu gani wa kuheshimiwa ndani ya tanzania ya leo....ebu niambie prof mukandala,prof liviga na prof kilian etc wao wameifanyia nini tanzania....kuna utafiti gani wamefanya wakabadili maisha ya mtanzania au kusimamia jambo gani
 
Kwanza ili niwe katika nafasi ya kujua swali lako lina maana gani ningependa na wewe uniambie umeifanyia nini tanzania mpaka hapo ulipofikia maana kila siku tunawasema viongozi alafu nitakwambia nchimbi kafanya nini yeye

1. Huhitaji kujua mimi nimeifanyia nini Tanzania ili kuweza kuniambia mimi Nchimbi kaifanyia nini Tanzania. Kama kuna kitu kiko wazi ambacho Nchimbi kaifanyia Tanzania, hiki (achievements) hakitakiwi kufichwa na wapenzi na washabiki wa Nchimbi, hakitaki mbinde za biashara za kubadilishana "wewe niambie umeifanyia nini Tanzania ili mimi nikwambie Nchimbi alichoifanyia Tanzania". Kiongozi mwenye accomplishment wala hahitaji kuulizwa yeye wala wapambe wake, kazi yake inaonekana. Na akipewa nafasi ndogo tu ya ku expose kazi zake kuna kitabu kizima cha kuandikwa, wala hawezi kuanza kushughulika kuchelewesha mjadala wa maswala aliyofanya. Ukiona mtu/ mpambe anaanza kuchelewesha mjadala kwa kuuliza viswali visivyo akili kama "kwanza wewe umeifanyia nini Tanzania" hapo unaona, ahaaaa, hapa watu hawana jibu, wana buy time tu kuangalia utasema nini. Hawana la kusema.

2. Mimi sijaomba uongozi. Sihitaji kufanya makubwa. Nikisema nimeitumia familia yangu US $ 1,000 kwa Krismasi juzi, na namlipia cousin wangu gharama za Chuo cha udaktari ili kuongeza madaktari Tanzania, na kusaidia watu to the tune of thousands of dollars a year, that is more than enough. Naweza kufanya mambo madogo tu kama kupeleka fedha kusaidia familia yangu Tanzania nikanawa mikono. Sijaomba dhamana ya uongozi. Kwa hiyo usitake kufanya standard ya kazi yangu mie nilieamua kupiga kura na miguu yangu bila kuomba uongozi na huyo Nchimbi anayekula kodi ya wananchi kuwa sawa. Hatuwezi kuwa sawa.

Wanasema "Noblesse Oblige". To whom much is given, much shall be required. I wasn't given much in terms of responsibility, therefore what is required of me is not much. Those who asked for much in terms of leadership / privileges, must be held highly responsible, accordingly.Not on a par with the Kirangas of this world.

Huwezi kutaka Kiranga ambaye hajachukua VX wala nyumba kwa dhamana ya wananchi wa Tanzania, hakai katika cabinet ya Tanzania wala kwenda mjengoni Dodoma, aulizwe kafanyia nini Tanzania on the same par with Dr. Nchimbi ambaye ana influence zote za kiserikali.

Kwa kufanya comparison hii tu unajionyesha wewe ni mmoja wa hao burlesques usiyejua kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…