Huku kulia lia kwa wafuasi wa Lowassa kunaonyesha kabisa kwamba huyu bwana yuko desperate kujisafisha wakati alishapa nafasi ya kuyasema hayo na mbele ya bunge lakini kwa woga wake na kwa sababu ya kujua kwamba yeye ni mhalifu katika hilo, akakimbilia kuhusisha ripoti ile na uwaziri mkuu wake.
Leo kwa ulevi tu, watu wanaanza kuingiza concept za natural justice ambao hata hawana weledi nazo na kudhani kwamba uchafu uliomtapakaa bwana huyu utasafishwa kwa porojo za humu JF. Awadaganye hao hao wajumbe wa NEC na wafuasi na wapambe wake mbumbumbu, siyo watanzania wenye ufahamu.
Mkuu Mbopo,
Tangu Ripoti ya Mwakyembe itoke kuna mambo mengi sana yametokea na yana ashiria kuna uvundo mwingi sana ambao ulifichwa ili usijulikane kwa watu. Hoja ya Waberoya hailengi kumtetea Lowassa au kukubaliana na utetezi wa Lowassa. Hoja kuu hapa ni kwamba kuna mambo yalifichwa kwa malengo fulani.
Moja, Lowassa anadai hakuhojiwa na Kamati Teule ili na yeye aeleze upande wake na hivyo Kamati Teule iwe na ripoti yenye maelezo ya wahusika wote. Kuna dots nyingi sana ambazo zinahitaji maelezo kwamba ni kwanini Lowassa hakuitwa kuhojiwa. Hoja ya kwamba ni Waziri Mkuu, haikuwa na mashiko.
Mbili, baada ya JK kurudi Dar, akiwahutubiwa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alisema kwamba Lowassa amepata "ajali ya kisiasa". Hiyo kauli ilikuwa na maana pana sana na mpaka leo hii watu wanajiuliza maswali mengi sana.
Tatu, Lowassa akiwa anajitetea kwenye kipindi cha TBC, matangazo yake yalikatishwa ghafla bila hata kutoa taarifa. Hilo nalo linaweka alama kubwa ya kuuliza.
Nne, Dr. Mwakyembe kwa nyakati tofauti amesikika akisema kwamba kuna mambo ambayo hawakuyaweka kwenye ripoti kwa kuwa wangeyaweka wangeivua nguo serikali au kwamba walikuwa wanalinda heshima ya serikali, je ni serikali ipi na yupi hasa waliyekuwa wanamlinda.
Ukiunganisha hizo dots nne tu unaweza kukuta kwamba Mwakyembe na wenzake walisita kumwita Lowassa kwa lengo la kuilinda Ikulu kwa kuwa kama angeitwa basi lazima na Ikulu nayo ingehusishwa moja kwa moja. Lowassa juzi kasema kwamba alijiuzulu ili kulinda heshima cha chama na serikali. Lakini ukweli ni kwamba alikuwa analinda heshima ya mkuu wa kaya na ndio maana wameshindwa kumvua gamba.
Swala hapa sio Lowassa, swala ni ukweli ulio ndani ya Ripoti ya Mwakyembe. Ukiichunguza sana na ukaangalia mwenendo wa swala zima unapata mashaka sana.
Bunge lilipendekeza watu wengi sana wachukuliwe hatua kinidhamu na ikiwezekana kufikishwa mahakamani. Naomba niambie kati ya hao wote waliotakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu, ni nani alichukuliwa hatua ya kinidhamu na ni hatua gani ilichukuliwa? Dr. Mwakapugi alistaafu na kupewa haki zake zote. Mwanyika alistaafu na kupewa haki zake zote. Dr. Hosseah mpaka leo bado anadunda kama DG-PCCB. Bashir Mrindoko mwaka huu amepewa u-Naibu Katibu Mkuu. Kwanini serikali ilipata kigugumizi kuwachukulia hatua hao wote ambao walishiriki kwenye huo mchakato? Hilo pekee linatakiwa kukupa alama kubwa ya kuuliza.
Hakuna mtu anamtetea Lowassa, bali watu wanataka ukweli. Ripoti ya Mwakyembe ilisema mambo nusu ili kuilinda Ikulu na ndio maana Mwakyembe amebaki kuwa ni mtu wa kusema, nitasema ukweli, mara sijui warudishe hoja Bungeni ili tuseme kila kitu. Kwanini hakusema kila kitu tangu mwanzo?