Dr. Mwakyembe kufikishwa mahamakani kwa Utapeli

Shobi

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,401
Reaction score
4,371
Waziri wa JK kuburuzwa mahakamani

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, aweza kufikishwa mahakamani, kujibu shitaka la utapeli. Anatuhumiwa kumtampeli raia kutoka Korea, Chris Incheul Chae.

Mwingine awezaye kufikishwa mahakamani pamoja na Dk. Mwakyembe, ni Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa (CCM) na msemaji wa familia ya waziri huyo.

Aidha, Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia ya mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa mahakamani katika shauri hilo.

Dk. Mwakyembe na washirika wake hao wawili, ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo ya Power Pool East Africa Limited.

Dk. Mwakyembe na kampuni yake, wanatuhumiwa kwa utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa na Chris.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk. Mwakyembe na nyaraka mbalimbali, wamiliki wa kampuni hiyo wanatuhumiwa kumtapeli Chris mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.

Chris alitoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.2 milioni (zaidi ya Sh. 2.6 bilioni), ili kufidia ardhi na mali mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida. Eneo la Kisasida ndiko Dk. Mwakyembe na washirika wake wanakodai kukabidhiwa na serikali kuzalisha umeme wa upepo.

Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Tayari Chris amemlima barua kampuni ya Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk. Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari 2014.

Katika barua hiyo, kampuni ya Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

Anasema, 22 Februari 2010, kampuni yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika mradi huo.

Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, "deni hilo, linayaweka mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya macho ya kimataifa."

Aidha, katika makubaliano mengine, kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).

Nyaraka zinaoyesha, kufuatia malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.

Chanzo: Mwanahalisionline
 
Ukitumwa unawambia sijasoma shule. Andiko kama la mtu wa Darasa la Saba. Nchi inakufa.

"Ikulu jijini Dar es salaam, nchini Korea ..."

Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa bodi ya kampuni
ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia
ya mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa
mahakamani katika shauri hilo.

Dk. Mwakyembe na washirika wake hao wawili, ni
miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme
kwa njia ya upepo ya Power Pool East Africa Limited.
Dk. Mwakyembe na kampuni yake, wanatuhumiwa kwa
utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa
kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa
na Chris.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu jijini
Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk.
Mwakyembe na nyaraka mbalimbali,
wamiliki wa
kampuni hiyo wanatuhumiwa kumtapeli Chris mamilioni
ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.
 
Mwakyembe asipokuwa mwangalifu atafungwa .

Tusiyoyajua ni vizuri kuyaacha yapite. Kesi ya madai kwenye biashara kama hiyo mara nyingi huishia kwenye kuifilisi kampuni daiwa na sio kuwafunga wakurugenzi au wamiliki.
 
baadae akihamia chadema utasikia wanamsafisha pamoja na wakina kubenea wakisema ni mfumo wakati mfumo unatengenezwa na watu
 
KIkwete-na-Mwakyembe-620x309.jpg

Rais Jakaya Kikwete, (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe
Waziri wa JK kuburuzwa mahakamani

Posted by: Saed Kubenea 1 hour ago 0 Comments 511 Views
6

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, aweza kufikishwa mahakamani, kujibu shitaka la utapeli. Anatuhumiwa kumtampeli raia kutoka Korea, Chris Incheul Chae. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
Mwingine awezaye kufikishwa mahakamani pamoja na Dk. Mwakyembe, ni Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa (CCM) na msemaji wa familia ya waziri huyo.
Aidha, Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia ya mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa mahakamani katika shauri hilo.
Dk. Mwakyembe na washirika wake hao wawili, ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo ya Power Pool East Africa Limited.
Dk. Mwakyembe na kampuni yake, wanatuhumiwa kwa utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa na Chris.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk. Mwakyembe na nyaraka mbalimbali, wamiliki wa kampuni hiyo wanatuhumiwa kumtapeli Chris mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.
Chris alitoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.2 milioni (zaidi ya Sh. 2.6 bilioni), ili kufidia ardhi na mali mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida. Eneo la Kisasida ndiko Dk. Mwakyembe na washirika wake wanakodai kukabidhiwa na serikali kuzalisha umeme wa upepo.
Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Tayari Chris amemlima barua kampuni ya Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk. Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari 2014.
Katika barua hiyo, kampuni ya Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.
Anasema, 22 Februari 2010, kampuni yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika mradi huo.
Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, “deni hilo, linayaweka mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya macho ya kimataifa.”
Aidha, katika makubaliano mengine, kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).
Nyaraka zinaoyesha, kufuatia malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.

MWANAHALISI ONLINE

Tusiyoyajua ni vizuri kuyaacha yapite. Kesi ya madai kwenye biashara kama hiyo mara nyingi huishia kwenye kuifilisi kampuni daiwa na sio kuwafunga wakurugenzi au wamiliki.

Lakini credibility yake Mwakyembe si itakuwa imeshuka? maana huwa anajifanya ni mtu mwenye moral authority ya kusema wenzake kuwa ni wachafu ili hali ya kuwa kumbe na yeye ni takataka tu!
 
mumeanza kumchafua?
Mumejua kuwa amepanga kuleta ushaidi wa walimpa sumu mnaanza kuweweseka subili ,
ungeleta zile nyaraka za fisadi papa alizokuwa anatuonyesha slaa zidi ya lowasa ndo tungejua wewe ni binadamu,
 
lakini credibility yake mwakyembe si itakuwa imeshuka? Maana huwa anajifanya ni mtu mwenye moral authority ya kusema wenzake kuwa ni wachafu ili hali ya kuwa kumbe na yeye ni takataka tu!

yule ni mtu makini,
ukitaka kumjua kaulize mashariti ya phd yake ndo umjue mwakyembye,

mwakyembe usimlinganisha na fisadi papa lowasa chini ya document za slaa,lililompa sumu,najua mshahara wa zambi ni mauti mwaka huu yatamtokea puani,
 
Tusiyoyajua ni vizuri kuyaacha yapite. Kesi ya madai kwenye biashara kama hiyo mara nyingi huishia kwenye kuifilisi kampuni daiwa na sio kuwafunga wakurugenzi au wamiliki.
unaambiwa hiyo kampuni haina hata senti tano ! sasa utafirisi nini ?
 
Lakini credibility yake Mwakyembe si itakuwa imeshuka? maana huwa anajifanya ni mtu mwenye moral authority ya kusema wenzake kuwa ni wachafu ili hali ya kuwa kumbe na yeye ni takataka tu!
ishuke mara ngapi ? alishaporomoka tangu alipolikataa andiko lake kwenye BMK .
 
Ukitumwa unawambia sijasoma shule. Andiko kama la mtu wa Darasa la Saba. Nchi inakufa. "Ikulu jijini Dar es salaam, nchini Korea ..."

Mkuu heshima yako kabla hujawa mwepesi wa kutusi watu jitasmini kwanza uwezo wako wa kusoma na uelewa wa habari kabla ya kusema.

Kikubwa ulichokikosa au kushindwa kutambua katika usomi wako ni maneno "taarifa zilizopatikana kutoka...".

Pili ujue umuhimu wa alama ya mkato (comma) " , " ina maana taarifa imetoka kwenye vyanzo mbali mbali ikiwemo Ikulu jijini Dar , nchini Korea , watu wakaribu wa Mwakyembe na mwisho nyaraka mbalimbali.

Sasa cha kufanya ni kurudia tena kusoma halafu muombe msamaha mleta habari sababu kwa haraka haraka unaonyesha unakaogonjwa fulani kanaitwa "DISLEXIA".
 
Ndugu chunga ndimi zako,mwakyembe hafai,atakufuatilia humu jf na kukupata,muulize mwenzako aliyemzushia mwakyembe amesema hamtaki lowassa awe rais,ananyea debe mpaka saa hizi yuko segadance,aisee acha kabisa jamaa ukimchafua anakuvalia njuga mpaka mwisho
 
Ushahidi wa Richmond utawasilishwa siku mbili kabla ya uchaguzi.. Wachaga lazima mtapike mbege siku hiyo.
 
Lakini credibility yake Mwakyembe si itakuwa imeshuka? maana huwa anajifanya ni mtu mwenye moral authority ya kusema wenzake kuwa ni wachafu ili hali ya kuwa kumbe na yeye ni takataka tu!

Hivi unadhani atashitakiwa yeye kama Mwakyembe?
 
Back
Top Bottom