Dr. Mwakyembe kufikishwa mahamakani kwa Utapeli

Dr. Mwakyembe kufikishwa mahamakani kwa Utapeli

Kama ulivyoandika tu inaonyesha una utofauti sana na kitu unachotetea. Habari imekaa kama karatasi iliyookotwa kwenye "dustbin". Haivutii wala haileti maana.
Habari kama hizi hazionyeshi ukweli wowote. Mwakyembe anahusika vipi? Nilibahatika kusoma "Business Laws", hakuna mahakama inashitaki mtu eti kwa sababu ya kosa la kampuni. Kama nakosea wale wanaojua sheria, wanaweza elezea.

Ndo maana nasema kuna habari za kishabiki na za kweli.

Mkuu naona umetoka nje ya mada yangu kabisa. Mimi nimetoa muongozo wa mtirirko wa habari husika, sijazungumzia mvuto wa habari sababu mivuto iko ya aina nyingi na kila mtu ana wake sababu hiyo ni "intrinsic issue" lakini kwenye umaana wa habari kwangu still ina maana.

Pia sija-question taaluma yako sababu naelewa kabisa hiyo ni LTD company na vitu vyote titled Dr. Mwakyembe haviko reliable na hiyo company.

Lakini Dr. Mwakyembe kama owner wa kampuni analo la kujibu sababu wamevunja masharti ya mkataba wa kampuni yake na kampuni inayolalamika.

Misleading of stakeholders for personal enrichment and lack of transparency are unfair/illegal commercial practices which might be treated as fraud or other criminal conduct.

Sina taaluma ya business law ila kwa uelewa wangu mdogo tu wa biashara Dr. Mwakyembe ana lakujibu kama Mkurugenzi au mmiliki wa kampuni..
 
Sijaongelea habari za yeye kushtakiwa! ninachomaanisha ni kuwa as long as na yeye ni mtu ambaye yuko kwenye hiyo scandal tayari anakuwa ashachafuka.

Zingatia maneno hayo hapo chini

Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Tayari Chris amemlima barua kampuni ya Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk. Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari 2014.
Katika barua hiyo, kampuni ya Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.
Anasema, 22 Februari 2010, kampuni yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika mradi huo.
Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, “deni hilo, linayaweka mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya macho ya kimataifa.”
Aidha, katika makubaliano mengine, kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).
Nyaraka zinaoyesha, kufuatia malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.

Usisahau kuwa hizo ni tuhuma tu.
 
Huo upuuzi unaouongea ni kwa Afrika tu, ndio unafanyika, na kuonekana ni inshu ndogo tu, ila ingekuwa kwa wenzetu hapo ni doa kubwa sana kwa mtu kama yeye.

Nadhani ni kasumba yetu tu. Umesahau Bill Clinton na Lewinsky! Clinton alibakia madakani pamoja na yale yote kuwa zilikuwa ni scandals. Hata huko kwa wenzetu sio kweli kwamba hata uzushi wa kipuuzi unatiliwa maanani.
 
Hana la kujibu. kwa sababu watashitaki kampuni na si Mwakyembe.
Mkuu naona umetoka nje ya mada yangu kabisa. Mimi nimetoa muongozo wa mtirirko wa habari husika, sijazungumzia mvuto wa habari sababu mivuto iko ya aina nyingi na kila mtu ana wake sababu hiyo ni "intrinsic issue" lakini kwenye umaana wa habari kwangu still ina maana.

Pia sija-question taaluma yako sababu naelewa kabisa hiyo ni LTD company na vitu vyote titled Dr. Mwakyembe haviko reliable na hiyo company.

Lakini Dr. Mwakyembe kama owner wa kampuni analo la kujibu sababu wamevunja masharti ya mkataba wa kampuni yake na kampuni inayolalamika.

Misleading of stakeholders for personal enrichment and lack of transparency are unfair/illegal commercial practices which might be treated as fraud or other criminal conduct.

Sina taaluma ya business law ila kwa uelewa wangu mdogo tu wa biashara Dr. Mwakyembe ana lakujibu kama Mkurugenzi au mmiliki wa kampuni..
 
Mkuu naona umetoka nje ya mada yangu kabisa. Mimi nimetoa muongozo wa mtirirko wa habari husika, sijazungumzia mvuto wa habari sababu mivuto iko ya aina nyingi na kila mtu ana wake sababu hiyo ni "intrinsic issue" lakini kwenye umaana wa habari kwangu still ina maana.

Pia sija-question taaluma yako sababu naelewa kabisa hiyo ni LTD company na vitu vyote titled Dr. Mwakyembe haviko reliable na hiyo company.

Lakini Dr. Mwakyembe kama owner wa kampuni analo la kujibu sababu wamevunja masharti ya mkataba wa kampuni yake na kampuni inayolalamika.

Misleading of stakeholders for personal enrichment and lack of transparency are unfair/illegal commercial practices which might be treated as fraud or other criminal conduct.

Sina taaluma ya business law ila kwa uelewa wangu mdogo tu wa biashara Dr. Mwakyembe ana lakujibu kama Mkurugenzi au mmiliki wa kampuni..

Nextime usiandike kitu ambacho huna uhakika nacho. Usikubali kushikiwa akili na mafisadi.
 
Nextime usiandike kitu ambacho huna uhakika nacho. Usikubali kushikiwa akili na mafisadi.

Watu wakija jf wanajifanya engineer,tiss mara askari kumbe mburura tu.wewe unajifanya knowldg ya biashara unayo kumbe mwisho chekechea.

Yaani kampuni yako ishtakiwe wewe usiwe na kesi?
 
Watu wakija jf wanajifanya engineer,tiss mara askari kumbe mburura tu.wewe unajifanya knowldg ya biashara unayo kumbe mwisho chekechea.

Yaani kampuni yako ishtakiwe wewe usiwe na kesi?

ukute huu ni uzushi tu
 
mumeanza kumchafua?
Mumejua kuwa amepanga kuleta ushaidi wa walimpa sumu mnaanza kuweweseka subili ,
ungeleta zile nyaraka za fisadi papa alizokuwa anatuonyesha slaa zidi ya lowasa ndo tungejua wewe ni binadamu,

hivi na wewe, ukitumwa kazi huifanya yote au nusunusu? Mwakyembe atuambie alipewa kiasi gani hadi azuie anazodai nyaraka muhimu za Richmond. Aliwavunja moyo wasomi wenzake kwa kitendo chake cha kufanya kazi chini ya kiwango na kujidai kuficha nyaraka ili azitumie kudai rushwa na kuwatisha watendaji wa serikali. Kwanini akae na nyaraka hizo miaka yote hiyo kama hakuwa na nia mbaya?
 
mkuu alikutapeli sh ngapi nikulipe?

Kubenea yupi, yule bendeara ya Mengi, sasa bendera ya Lowassa? Naapa, hata kama sina ushahidi kuwa kwenye taarifa hii Kubenea kavuta kutoka kuwa bilionea EL.Lengo linaweza kuwa kumdhoofisha Mwakyembe asimshughulikie EL kuhusu Richmond.
 
kimbegu njia

Namfahamu sana Kubenea na namfahanu sana Chris Chae ni tapeli wa kimataifa anayejitambulisha kuwa ni Mkorea na ndugu wa Ban-ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wakati yeye ni Mmarekani na hana undugu na kiongozi hiyo. Katutapeli sana wafanyabiashara wa hapa Bongo wenye nia ya kupanuka kibiashara kwa kudai anatuunganisha na makampuni ya Korea. Kaziliza kampuni nyingi vilevile za Korea. Ni MTU mazishi sana na ana lugha laini ya kumlainisha hata shetani. Mimi siamini kama ametapeliwa, maana jamaa ni mwongo sana. Anatumia jina la Mwakyembe kimkakati hapa na sidhani mwanasiasa msomi kama Mwakyembe anaweza kuwa mkurugenzi wa kampuni wakati ni Waziri.

Kubenea ni mtu wa kutumika sana, pengine ni kwa sababu ya elimu ndogo. Ni kipeperushi cha Mengi sasa ameamua kuwa kipeperushi cha Lowassa ili asimuudhi Mengi. Ameandika habari hii kiumbeaumbea tu: BRELA wanasemaje, Mwakyembe ndo CEO wa kampuni hiyo? Anasema ameongea na IKULU, IKULU nani? Salva Rweyemamu wa Richmond? Na kwa nini madai haya yajitokeze wakati huu wa uchaguzi kama si umamluki tu wa Kubenea? Kama kampuni inadaiwa, inadaiwa magazetini au mahakamani? Extremely childish!
 
Last edited by a moderator:
acha sheria ya mitandao ianze make nyie ndo tunawatafuta kwa habr za kuzusha,na msipoacha upumbavu huo mtajuta,hii mitandao si kusudi lake hilo
 
ww bwana ww nakuhisi utakuwa Richard lowasa wa monduli ww.
Maana unampiga vita sana mwakyembe

Ha! Ha! Haaaa!! hapana mkuu mimi ni mkazi wa kajunjumele na mwakyembe ni rafiki yangu sana , isipokuwa mimi namkataa mtu yeyote anayejihusisha na ccm .
 
credibility ya hii taarifa ni ya mashaka. Kwanza ni taarifa ya siku nyingi na hivi sasa imeletwa kwa misingi ya kisiasa zaidi. Pamojana kuwepo chembe za kuwepo uhusiano wa kibiashara kati ya kampuni mbili tajwa na siyo Mwakyembe kama moja wa share holder, taarifa imeharibiwa na kuhusishwa kwa Ikulu, na Serikali ya Korea. Chris Chae hana mahusiano mazuri na Serikali ya Korea kwa kuwa naye aliwahi kuishitaki Serikali hiyo kuhusiana na masuala ya biashara zake za kimagumashi. Ikumbugwe kuwa Chris siyo Mkorea bali Mmarekani mwenye asili ya Korea.
 
Waziri wa JK kuburuzwa mahakamani

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, aweza kufikishwa mahakamani, kujibu shitaka la utapeli. Anatuhumiwa kumtampeli raia kutoka Korea, Chris Incheul Chae.

Mwingine awezaye kufikishwa mahakamani pamoja na Dk. Mwakyembe, ni Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa (CCM) na msemaji wa familia ya waziri huyo.

Aidha, Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia ya mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa mahakamani katika shauri hilo.

Dk. Mwakyembe na washirika wake hao wawili, ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo ya Power Pool East Africa Limited.

Dk. Mwakyembe na kampuni yake, wanatuhumiwa kwa utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa na Chris.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk. Mwakyembe na nyaraka mbalimbali, wamiliki wa kampuni hiyo wanatuhumiwa kumtapeli Chris mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.

Chris alitoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.2 milioni (zaidi ya Sh. 2.6 bilioni), ili kufidia ardhi na mali mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida. Eneo la Kisasida ndiko Dk. Mwakyembe na washirika wake wanakodai kukabidhiwa na serikali kuzalisha umeme wa upepo.

Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Tayari Chris amemlima barua kampuni ya Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk. Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari 2014.

Katika barua hiyo, kampuni ya Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

Anasema, 22 Februari 2010, kampuni yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika mradi huo.

Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, “deni hilo, linayaweka mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya macho ya kimataifa.”

Aidha, katika makubaliano mengine, kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).

Nyaraka zinaoyesha, kufuatia malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Mwakyembe anapaswa pia kushitakiwa kwa kushindwa kutoa taarifa yote kuhusu Richmond
 
Back
Top Bottom