Inapofika wakati kama huu ambapo uhai wa mTanzania una tishiwa na genge la mafisadi,kila mTanzania inabidi achukie suala hilo na kichukua hatua binafsi ya kupambana nalo.
Utetezi wa haki si suala la chama bali wananchi wote wenye uelewa wa utawala bora.
Kimsingi CCM inaanza kukosa uhalali wa kuwepo madarakani kama kinafikiri kinaweza kuwafurahisha mafisadi na wapinga ufisadi kwa pamoja, na chama kuendelea kuishi kama kawaida.
- Bahati mbaya ni kwamba huyo Mtanzania anayetishiwa uhai na hilo genge la mafisadi wote wanalala kitanda kimoja.
- Kama CCM inakosa uhalali wa kuwepo madarakani, huyo Mtanzania anapata wapi uhalali wa kuwa mwana CCM?
- CCM kimeweza sana kuwafurahisha mafisadi na wapinga ufisadi kwa pamoja, ndio sababu Mwakyembe anaikumbatia.
- Utamteteaje anayejiita mpinga ufisadi ndani ya CCM wakati ni ukweli usiopingika kuwa birds of a feather fly together?
- Kama kweli ndani ya CCM yupo anayechukia ufisadi, huyo ni hatari zaidi kuliko hata huyo fisadi, ama ni mwoga au mnafiki.