Nasikia Dr. Mwaka alimtibu mama mwenye tatizo la uzazi kwa kumjambia tumboni...mmeipata hiyo?
Alianza mama teri
Akaja Ndodi
Sasa hivi dr mwaka
Halafu wahanga wengi huwa ni wanawake....
na kuna mwingine anajikongoja ana kipindi kinaitwa 'the plants'
yaani utapeli ni ule ule ila madokta wanabadilika tu..
mama terry hata kuandikisha kadi tu ilikuwa utapeli mtupu
Hahah huyo "the plants" sijamsikia bado
Kweli mjini mipango....
Ana kipindi EATV na juzi nimemuona TV1
hahaaaaa hawa madaktari sijui wa tiba mbadala huwa wanachekesha sana.
Hivi yule Babu wa kikombe na Dr Mwaka nani zaidi? Maana nasikia tu matangazo mengiii waliopona sisikii ebu niambieni
HahahahahahahahahahahahahaHuyu Dr Mwaka ameinvest kwenye matangazo si mchezo ukimkwepa startv utamkuta eatv, ukimkwepa eatv utamkuta clouds TV, ukimkwepa kwenye tv utamkuta redioni. Huyu ni new version ya Dr. Ndodi, kama ni tapeli basi atawatapeli wengi. Vipi Dr Rahabu na Ndodi wameishia wapi?
Hivi yule Babu wa kikombe na Dr Mwaka nani zaidi? Maana nasikia tu matangazo mengiii waliopona sisikii ebu niambieni
Heri babu wa loliondo alikuwa anatoza 500/= tu, kuliko huyu dr wenu mwaka, anakusanya ndimu na tangawizi kariakoo mia mia, halafu anakupa dozi yenye ndimu moja na kipande cha tangawizi kwa 200,000/= kupona. Hakuna. Watanzania tuna shida kweli kweli, hii yote ni sababu ya kutokuwa na matibabu ya uhakika kweye hospitali zetuHivi yule Babu wa kikombe na Dr Mwaka nani zaidi? Maana nasikia tu matangazo mengiii waliopona sisikii ebu niambieni