Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,338
33,163
Dr. Mwaka amjibu Shekhe wa Mkoa wa DSM







Dr. Mwaka amesema kuwa watanzania siyo wajinga na wanayofanyiwa wanayaona, Masheikh wachafu na wasafi wapo na watanzania wanawajua. Ushahidi wa Masheikh hawa wachafu, watanzania wanao na hata yeye Mwaka mwenyewe anao pia.

Akasema kuna watu ambao kwa sura ya nje wanaonekana ni Masheik/Wachungaji lakini ndani yao ni wachoyo, wasengenyi, wazinzi, walafi na kila aina ya takataka na baadhi yao wanafanya mambo yao kwenye ofisi zao.

Akaendelea kusema kuna baadhi ya viongozi wa kiislamu ambao wanafatwa na wanawake kwaajili ya kuomba ushauri dhidi ya ndoa zao lakini wanaishia kupewa dola 100/200 kuomba namba za simu na kuanza kuwatongoza. Ushahidi anao lakini hawaweki hadharani kufunika kombe mwanaharamu apite, na akitaka Mwaka atoe ushahidi huo aseme "Suuu!"




Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam alisema watu wanaharibu sana dini na kuingilia fani ambazo si zao, akisema mtu ambaye alisema Muislamu kuombewa dua na Mkristo ni sawa, na pia mtu anaweza kwenda kuomewa dua na Sheikh/Mchungaji wakati Mungu hana hata muda naye wakati Sheikh wa Mkoa akisema hii si sawa na haifai, ibada ya muislamu haiwezi kufanywa na asiyekuwa muislamu.

Waislamu na wakristo wasaidiane katika mambo mengine lakini sio kuombeana dua. Akasema Masheikh wafungue vituo vya dua vyao kuwasaidia wenye matatizo ili wasikimbilie kwa Mwamposa kwasababu haifai na siyo sawa kwa Mkristo kumuombea dua Muislam.
 
Kwa hiyo si sawa, kwa mfano makanisani huwa kuna maombi ya kuliombea taifa na hususani kumuombea rais wa nchi sasa ina maana maombi hayo yanayofanyika makanisani kumuombea rais muislam ni batili na kamwe Mungu hayasikii??!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom