Dr Mpoki Ulisubisya awa balozi wa Tanzania nchini Canada

Dr Mpoki Ulisubisya awa balozi wa Tanzania nchini Canada

Kuna dynamics nyingi ambazo hatutajua publicly.

Inawezekana anapelekwa huko nje kwa sababu za kisiasa, au kwasababu zingine. Atleast amepewa nchi yenye status. Wangeweza kumtupa libya huko.

Pamoja na hayo bado naamini sekta ya afya bado ilimhitaji sana huyu jamaa, ni gwiji. Kumbuka huyu ndio alimuokoa lissu.
Inawezekana hiyo ndiyo adhabu yake. Kilangila.
 
Yes. Ilikua bahati alikua dodoma siku ile. Yeye ndio alifanya huduma ya kwanza kuokoa maisha ya lissu kabla hajapelekwa nairobi.


..na ndiye aliyeruhusu Madaktari wa Dodoma Hospital wamsindikize TL na kumkabidhi Nairobi Hospital.

..TL amenukuliwa akisema wakati Mbowe na Ndugai wakivutana kuhusu Nairobi vs Muhimbili, Dr.Mpoki aliingilia kati na kusema " I am a Medical doctor, he[ lissu] he goes to Nairobi."

..Vilevile Katibu Mkuu Wizara ya Afya ndiye mwenye kauli ya mwisho ya mgonjwa kutibiwa nje ya nchi.

..Madaktari wa Muhimbili au daktari yeyote bingwa hupeleka mapendekezo ya mgonjwa kutibiwa nje kwa Katibu Mkuu Wizaya ya Afya ambaye huidhinisha au huyakataa maombi hayo.

..Wanaodai TL hakufuata taratibu kwenda Nairobi wanakwamishwa na ukweli kwamba Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dr.Mpoki, alitoa ruhusa ya mgonjwa kupelekwa Nairobi.

Cc Pascal Mayalla, Nguruvi3, Mag3
 
. Dk Mpoki Ulisubisya, leo Jumatatu Mei 20, 2019 ameapishwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada kuchukua nafasi ya Alphayo Kidata aliyevuliwa ubalozi.

Novemba, 2018 Rais Magufuli alimrejesha nchini Kidata na kumvua hadhi ya ubalozi bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Dk Ulisubisya aliyeteuliwa kuwa balozi Janauri 9, 2019 ameapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kabla ya uteuzi huo Dk Ulisubisya alikuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia afya na nafasi yake ilichukuliwa na Dk Zainabu Chaula.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Peter Eriksson
Hivi huko Canada sindo yupo dkt slaa au?
 
Na yeye ni mtu asiyejulikana? Maana wakurugenzi wastaafu wa Tiss hupelekwa Canada kama mabalozi,may be huko ndio kuna-coordinate Intel kimataifa kwa ulaya na marekani
 
Itakua anasoma magazeti tu nyumbani kwake,acacia walitaka kumtumia kupitia watanzania flani ambao walikua viongozi waandamizi wa acacia akashitukiwa,kina Deo Mwanyika na Assa Mwaipopo,pia Mzungu mmoja anaitwa Peter Geleta

Kina Mwanyika na Mwaipopo wananyea debe kwa sasa
Magu noma!!
 
Siku rais anamteua alisema ,amepata habari kwamba Mpoki anapenda sana kusafiri nje ya nchi hataki wengine waende inapotokea safari ya kikazi,akamwambia nakuteua ukakae hukohuko.
Inawezekana akawa kapotezwa chini ya uangalizi pia
Hatari sana,
 
Yule alitaka kwenda Islamabad ,Magu akamtia sijui Zambia ...Aliposemwa na Magu tu jioni yake nikamkuta Tunduma akiwa kwenye lori la Transit.
zilikua zimebaki dakika chache ,ingebaki simulizi,Magu hatabiriki[emoji23][emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Huu ni ukweli. Pamoja na kwamba kapewa ubalozi kwenye nchi nzuri, nadhani kama nchi tunawaste hazina kubwa sana. Mpoki ni daktari bingwa wa usingizi hapa nchini, madaktari wa namna hiyo wapo wachache sana bongo kwa sasa. Huyu ilibidi tumtumie hapa ili aweze kuwapa uzoefu na wengine.

Ila yote kwa yote pongezi kwake
Wapo wengine wanafyatuka kila uchao huko vyuoni na internship juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom