Dr Mpoki Ulisubisya awa balozi wa Tanzania nchini Canada

Dr Mpoki Ulisubisya awa balozi wa Tanzania nchini Canada

mwananyaso

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,995
Reaction score
3,402
. Dk Mpoki Ulisubisya, leo Jumatatu Mei 20, 2019 ameapishwa na Rais John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada kuchukua nafasi ya Alphayo Kidata aliyevuliwa ubalozi.

Novemba, 2018 Rais Magufuli alimrejesha nchini Kidata na kumvua hadhi ya ubalozi bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Dk Ulisubisya aliyeteuliwa kuwa balozi Janauri 9, 2019 ameapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine waliohudhuria ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kabla ya uteuzi huo Dk Ulisubisya alikuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia afya na nafasi yake ilichukuliwa na Dk Zainabu Chaula.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden, Peter Eriksson
 
Hongera kwake Mhe. Balozi, akawe mwakilishi mzuri kwa nchi na akatusaidie vyema katika uwekezaji, utalii na diplomasia
 
Kidata alichomkosea mkuu inaonekana ni kikubwa sana
 
Angemrudisha MNH amempeleka kijiweni
Huu ni ukweli. Pamoja na kwamba kapewa ubalozi kwenye nchi nzuri, nadhani kama nchi tunawaste hazina kubwa sana. Mpoki ni daktari bingwa wa usingizi hapa nchini, madaktari wa namna hiyo wapo wachache sana bongo kwa sasa. Huyu ilibidi tumtumie hapa ili aweze kuwapa uzoefu na wengine.

Ila yote kwa yote pongezi kwake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom