Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,610
- 21,184
Dr. Mpango umesema:
Uzoefu unaonyesha kuwa fedha za misaada kutoka kwa wahisani zinapatikana kwa mbinde sana na wakati fulani ni ahadi hewa. Wananchi wanailalamikia serikali kuwa mikopo imezidi na deni limekuwa kubwa mno kulingana na uwezo wetu lakini wewe Dr. Mpango unasema deni ni himilivu!
Matokeo yake inafika mwisho wa mwaka fedha za maendeleo zinazokuwa zimetolewa na serikali ni wastani wa 30% ya bajeti uliyopanga. Sasa maswali:
- Mapato ya nchi ni wastani wa shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi;
- Mishahara kwa mwezi ni shilingi bilioni 500 kwa mwezi;
- Kulipa madeni ya ndani na nje ni shilingi bilioni 600 kwa mwezi;
- Fedha inayobaki kwa matumizi ya kawaida ya serikali, ulinzi na usalama wa nchi na viongozi ni shilingi bilioni 200 kwa mwezi.
Uzoefu unaonyesha kuwa fedha za misaada kutoka kwa wahisani zinapatikana kwa mbinde sana na wakati fulani ni ahadi hewa. Wananchi wanailalamikia serikali kuwa mikopo imezidi na deni limekuwa kubwa mno kulingana na uwezo wetu lakini wewe Dr. Mpango unasema deni ni himilivu!
Matokeo yake inafika mwisho wa mwaka fedha za maendeleo zinazokuwa zimetolewa na serikali ni wastani wa 30% ya bajeti uliyopanga. Sasa maswali:
- Kwanini unapanga bajeti kubwa kuliko uwezo wa serikali kimapato?
- Kwanini unaendelea kukopa huku ukijua fika uwezo wa serikali kulipa ni mdogo?
- Kwanini unasema uchumi unakuwa huku ukijua wazi kuwa wananchi wako hoi bin taabani mifukoni?
- Unatumia kigezo gani kuwa uchumi unakua?
- Kwanini usiachie ngazi haraka kuliko kuendelea kuwagandamiza wananchi?
- Je, hayo unayoyafanya si matumizi mabaya ya madaraka?