Dr. Mpango alalamika Wajapan kufanyia mkutano hotelini badala ya kumbi za serikali, wenyewe wamsuta

Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
4,722
10,475
Shirika la Japan(JICA) liliandaa semina ya kuwafunda Internal Auditors wa serikali. Semina ikafanyika Morogoro,kwa gharama za JICA.

Dr Mpango akiwa ni mualikwa,akamkoromea waziwazi Internal General Auditor wa serikali Mohamed Mtonga. Kwamba kwanini hafuati utaratibu wa serikali wa ubanaji matumizi.

Akamwambia alitakiwa awashauri JICA wafanyie mkutano serikalini halafu fedha zilizokuwa zikodie hotel zipelekwe serikalini kufanyia mambo mengine.
Mwakilishi wa JICA Tanzania Toshio Nagase akamkoromea wazi wazi ,namnukuu ''Hizi fedha ni zetu,na sisi ndio tunajua tuzitumieje''

Ngase akaongeza kuwa semina hiyo ni muhimu sana hivyo ni lazima waitoe kwenye sehemu yenye kutia hamasa ya kujifunza(motivation). Akasema hata posho yakuwa nje ya kituo cha kazi 45,000 wanaitoa wao wenyewe.

======

Govt, donor disagree on cost-cutting initiative
mpango+pic.jpg


Morogoro. There was a confrontation of sorts here yesterday between finance minister, Dr Philip Mpango, and officials from the Japan International Cooperation Agency (JICA) over the implementation of government directive requiring official meetings to be held in government boardrooms instead of private venues such as hotels.

This happened during the opening of a five-day workshop for government’s internal auditors, sponsored by Jica, which Dr Mpango officiated.

The minister reprimanded Internal Auditor General, Mohammed Mtonga for failing to brief the sponsors on government’s new cost-cutting directive—included in the June national Budget speech—which forbids holding meetings and seminars in private hotels. Such meetings, the directive prescribes, should be held in government boardrooms.

Dr Mpango, who is a former World Bank economist, said holding the seminar in a private hotel was a waste of money, which could have been used to fund some development projects.

“This should end today. You should follow government directives, otherwise if you repeat this next time you shall have your salaries cut. There are many government institutions in Morogoro that could have provided us with a venue for this workshop. You were supposed to advise the sponsors to hold this seminar in a government boardroom and see if they could commit the money to some development projects,” Dr Mpango said, addressing Mr Mtonga.

In a rebuttal to the minister, Chief Representative of Jica in Tanzania, Toshio Nagase said they were not happy being told how to spend their money.

“This money is ours. And only we can decide how to spend it. No one else has the right to direct us how to spend it,” he told reporters after the end of the seminar held at the Edema Hotel here. Mr Nagase said the idea to hold the workshop at a private hotel was Jica’s and no government official should be blamed for that. He said they decided to take 100 internal auditors from ministries, departments, agencies and local government from seven regions and 14 local government authorities to a hotel in Morogoro and pay them allowances to serve as a motivation.

“We took them out of their work stations and we had to motivate them. Motivation is crucial in training programmes such as this one. That is why we have paid each of the participants Sh45,000 per diem for the five days they stayed here in Morogoro,” Mr Nagase said, adding that all the expenses, including accommodation, transport and meals, were paid for by Jica.

The government has adopted a number of cost-cutting measures under the 2016/17 budget including the use of government boardrooms for all meetings and seminars, banning printing and photocopying of official documents of more than 50 pages and giving a priority to government owned commercial organisations when procuring goods and services.

Chanzo: The Citizen
 
Nadhani kuna tatizo kwa weledi wa viongozi wetu hasa katika suala zima la leadership. Kabla ya kukurupuka alitakiwa kujua utaratibu uliopo.

Fedha zilizotumika JICA au Serikali ya Japan ilishaamua zitatumikaje, hakuna namna ambayo matumizi hayo yangeweza kubadilishwa.

Hata kama wasingeeda Morogoro fedha hizo sisingeweza kuingizwa katika mfumo mwingine, na huenda ikawa baada ya mwaka wa fedha kuisha zingerudi kwao.

Wenzetu wanaheshimu bajeti, na siyo tu ukijisikia kubadilisha kitu unaweza kufanya hivyo. Its pity it has happened that way.
 
Duh! Kweli adui wa Afrika ni Mwafrika mwenyewe, kwa maana anachojaribu kukifanya Waziri Mpango ni kuhakikisha kwamba fedha za Serikali hazitumiki hovyo kwa mambo ambayo siyo ya lazima, hizo fedha Waziri Mpango hazichukui yeye bali anataka kuziokoa lkn umeandika kishabiki kana kwamba unatafuta kumkomoa Waziri Muhongo, binadamu mwenye IQ ya wastani kabisa angeweza kumsifu Waziri Mpango hata kwa nia yake tu, na siyo kukaa na kusubiri kosa limefanywa wapi na kuanza kuponda, kumbuka hizi fedha ambazo zitaokolewa ni kwa ajili ya watz masikni ambao wanazihitaji na siyo za waziri Mpango!
 
Huyo mipango naanza kumshtukia ni mtu asiye na thinking capacity ya kutosha.Ndio maana kodi zake zimeleta mtafaruku kila mahali kuanzia miamala hadi watalii. Watu makini hufanya mambo baada ya kuangalia critically prons and cons zake. Wakurupakuji...........
 
Duh! Kweli adui wa Afrika ni Mwafrika mwenyewe, kwa maana anachojaribu kukifanya Waziri Mpango ni kuhakikisha kwamba fedha za Serikali hazitumiki hovyo kwa mambo ambayo siyo ya lazima, hizo fedha Waziri Mpango hazichukui yeye bali anataka kuziokoa lkn umeandika kishabiki kana kwamba unatafuta kumkomoa Waziri Muhongo, binadamu mwenye IQ ya wastani kabisa angeweza kumsifu Waziri Mpango hata kwa nia yake tu, na siyo kukaa na kusubiri kosa limefanywa wapi na kuanza kuponda, kumbuka hizi fedha ambazo zitaokolewa ni kwa ajili ya watz masikni ambao wanazihitaji na siyo za waziri Mpango!
Unamaanisha waziri mpango yeye ana akili sana kuliko hao wajapani??
Yeye hajataka kuziokoa.. Kasema zibanwe ili serikali ipewe hizo pesa zitakazobakia.. Serikali ikipewa si ndio ili ikawalipe mshahara wakuu wa wilaya au? Na mbio za mwenge? Au?
 
When in Rome do as the Romans do.

Wajapan waendelee kutikisa kiberiti, lakini serikali ikianza kufanya yake wasianze kulalamika Tanzania inapendelea nchi nyingine.
 
Sasa serikali ina vita na wafanya biashara?
Pesa siyo yako bado unakomaa kumpangia mtu matumizi
Mbona wivu umewazidi?
 
Unamaanisha waziri mpango yeye ana akili sana kuliko hao wajapani??
Yeye hajataka kuziokoa.. Kasema zibanwe ili serikali ipewe hizo pesa zitakazobakia.. Serikali ikipewa si ndio ili ikawalipe mshahara wakuu wa wilaya au? Na mbio za mwenge? Au?
Ninachozungumzia hapa ni lengo la Waziri na siyo utekelezaji, lengo la Waziri na Serikali kwa ujumla kukata vikao kufanyika Mahotelini badala ya Kumbi za Serikali ni kuokoa fedha ambazo tunazihitaji, kwa mambo mengine muhimu zaidi, hilo ndiyo lengo sasa kama kunatokea kutokuelewana na Wajapani kuhusu nani katoa fedha hilo halipaswa kuwa jambo la kuchakekelea na kuanza kumdhihaki Waziri, mtu mwenye akili ya kawaida anapswa kuisifu Serikali kwa kuzuia upotevu wa fedha zetu ambazo tunazitolea jasho!
 
Mambo mengine aibu tupu hebu nenda hapo ADEM Bagamoyo uangalie huo ukumbi wao kisha vuka bara bara upande wa pili nenda kwenye zile hotel uone kumbe zao kisha uamue value for money itakua upande gani
 
Huyo mipango naanza kumshtukia ni mtu asiye na thinking capacity ya kutosha.Ndio maana kodi zake zimeleta mtafaruku kila mahali kuanzia miamala hadi watalii. Watu makini hufanya mambo baada ya kuangalia critically prons and cons zake. Wakurupakuji...........
Kaka huyu jamaa hakuna kitu.. Ni mweupe kichwani... Haiwezekani waziri mzima analeta unoko kama huu... Hamna kitu kichwani aisee
 
Back
Top Bottom