Dr. Mpango alalamika Wajapan kufanyia mkutano hotelini badala ya kumbi za serikali, wenyewe wamsuta

He yamekua hayo sasa....tutadumazwa akili kama wana Pyoungyang.....kule ukiingia kwa kinyozi kuna picha zina onesha style za nywele zinazo ruhusiwa ....ukinyoa kama Bekham basi ..jela
 
Shirika la Japan(JICA) liliandaa semina ya kuwafunda Internal Auditors wa serikali. Semina ikafanyika Morogoro,kwa gharama za JICA.

Dr Mpango akiwa ni mualikwa,akamkoromea waziwazi Internal General Auditor wa serikali Mohamed Mtonga. Kwamba kwanini hafuati utaratibu wa serikali wa ubanaji matumizi.

Akamwambia alitakiwa awashauri JICA wafanyie mkutano serikalini halafu fedha zilizokuwa zikodie hotel zipelekwe serikalini kufanyia mambo mengine.
Mwakilishi wa JICA Tanzania Toshio Nagase akamkoromea wazi wazi ,namnukuu ''Hizi fedha ni zetu,na sisi ndio tunajua tuzitumieje''

Ngase akaongeza kuwa semina hiyo ni muhimu sana hivyo ni lazima waitoe kwenye sehemu yenye kutia hamasa ya kujifunza(motivation). Akasema hata posho yakuwa nje ya kituo cha kazi 45,000 wanaitoa wao wenyewe.

Chanzo ni gazeti la The Citizen www.thecitizen.co.tz
Inaonekana upo msuguano kati ya Ofisi ya CAG na Serikali.
 
Ninachozungumzia hapa ni lengo la Waziri na siyo utekelezaji, lengo la Waziri na Serikali kwa ujumla kukata vikao kufanyika Mahotelini badala ya Kumbi za Serikali ni kuokoa fedha ambazo tunazihitaji, kwa mambo mengine muhimu zaidi, hilo ndiyo lengo sasa kama kunatokea kutokuelewana na Wajapani kuhusu nani katoa fedha hilo halipaswa kuwa jambo la kuchakekelea na kuanza kumdhihaki Waziri, mtu mwenye akili ya kawaida anapswa kuisifu Serikali kwa kuzuia upotevu wa fedha zetu ambazo tunazitolea jasho!
Kaka mimi nimekuelewa. Na huo ushauri ni mzuri.. Ila kiuhalisia ni ushauri kwenye wrong place.. Hivi kwani pesa za jica zikibaki serikali inapewa hizo pesa? Kivipi?
Kubana matumiI sio kitu kibaya na serikali imejitahidi sana.. Ila kuwapangia watu cha kufanya ni ujuha tena hao watu ndio wanaokupa misaada.. Ni kama masikini anamfundisha tajiri matumizi.. Ni ujuha na kituko cha karne
 
Hela za mjapani unalazimisha ziwe zako?! Aibu sana tangu lini ukapanga matumizi ya pesa za nyumba ya jirani? Japani wanajua tunashida ndio sababu wanatusaidia hata kufundisha hawa wataalam na kutupa mikopo, hii ya kutaka kupanga matumizi yao ni upumbavu.
 
Duh! Kweli adui wa Afrika ni Mwafrika mwenyewe, kwa maana anachojaribu kukifanya Waziri Mpango ni kuhakikisha kwamba fedha za Serikali hazitumiki hovyo kwa mambo ambayo siyo ya lazima, hizo fedha Waziri Mpango hazichukui yeye bali anataka kuziokoa lkn umeandika kishabiki kana kwamba unatafuta kumkomoa Waziri Muhongo, binadamu mwenye IQ ya wastani kabisa angeweza kumsifu Waziri Mpango hata kwa nia yake tu, na siyo kukaa na kusubiri kosa limefanywa wapi na kuanza kuponda, kumbuka hizi fedha ambazo zitaokolewa ni kwa ajili ya watz masikni ambao wanazihitaji na siyo za waziri Mpango!
Sio pesa za serikali ndugu.!
 
Kwa ukumbi ambao JICA walifanyia mkutano uko nchi nyingine au Tanzania !!! Hizo kumbi zinaingiza pesa Tanzania humo humo, aidha, kama hizo kumbi zikinyimwa mikutano, ina maana watu waliajiriwa katika hizo kumbi watakosa ajira.
JICA wanalipa kumbi na kumbi zina waajitiwa watanzania.. Si kitu kile kile..?
Na serikali ikipewa pesa lets say ikamlipa mkuu wa wilaya.. Na kumnunulia shangingi japani.. Na mkuu wa wilaya akaenda kula nyama choma na familia yake kwenye ukumbi ule ule .. Si kitu kile kile? Sasa hapo kuna tofauti gani?
Huyu waziri ni mweupeeeeeeeee!!!!
 
Mnajua kua hizo fedha walizokodia ukumbi mwisho wa siku zinajumlishwa ndo mnaambiwa msaada mliopata kutoka serikali ya Japani.

Mnaposikia wajapani au wamarekani wametoa msaada kwa serikali ya TZ msidhani kua wameleta fedha pale hazina.

Kinachofanyika inakuja organization ambayo ni ya kwao inafanya shughuli kama ni kutoa chanjo au capacity building ktk maeneo mbalimbali.

Sasa zile gharama zote ikiwemo mishahara yao na ya watanzania watakaoajiriwa, gharama za magari, gharama za kuendesha semina nk ndo zinajumlishwa na kuambiwa kua serikali ya japani au ya marekani imetoa msaada wa dola kadhaa kuisaidia Tanzania
 
Mnajua kua hizo fedha walizokodia ukumbi mwisho wa siku zinajumlishwa ndo mnaambiwa msaada mliopata kutoka serikali ya Japani. Mnaposikia wajapani au wamarekani wametoa msaada kwa serikali ya TZ msidhani kua wameleta fedha pale hazina. Kinachofanyika inakuja organization ambayo ni ya kwao inafanya shughuli kama ni kutoa chanjo au capacity building ktk maeneo mbalimbali. sasa zile gharama zote ikiwemo mishahara yao na ya watanzania watakaoajiriwa, gharama za magari, gharama za kuendesha semina nk ndo zinajumlishwa na kuambiwa kua serikali ya japani au ya marekani imetoa msaada wa dola kadhaa kuisaidia Tanzania
Sasa tatizo liko wapi?
 
Mpango hajajua kuwa wajapani walishabana matumizi kitambo ndio maana wakaja huku kwetu tena porini morogoro kufanya vikao vya bei nafuu...Wangekuwa hawajabana matumizi wangewaita wajumbe waende tokyo na kikao kifanyike 5star hotel na posho na nauli za watanzania walioalikwa walipwe kwa midolar....Ila wametuhurumia na kutusaidia kubana matumizi.

Sasa huyu mpango anataka wajapani wateseke kwenye viofisi vya serikali havina hata ac joto kama muko kuzimu...Akwendreeeeeeee kule akabane matumizi ya mafuta na mashangingi ya serikali. Asisahau pia wakuu wa mikoa na wilaya na mbio za mwenge nayo ni matumizi mabovu anaona pesa ya wajapani.

Kweli roho mbaya haina mwenyewe...Mtu huzaliwi nayo unajifunza tuu ukubwani.
 
Tatizo JICA hawabani matumizi zipo kumbi za bure za serikali!
Kuna watu Fulani walikuja Na semina yao kutoka Marekani kwa ajili ya watu Fulani serikalini. Wakaomba kifanyia semina hiyo Blue Pearl hotel. Tukawaeleza serikali haitaki hivyo inabidi tufanyie kumbe za serikali. Wakasema pesa ni zao Na namna ya kutumia wanapanga wao. Ndio kama hizo za jica serikali haiwezi kuwaingilia.!
 
JICA wanalipa kumbi na kumbi zina waajitiwa watanzania.. Si kitu kile kile..?
Na serikali ikipewa pesa lets say ikamlipa mkuu wa wilaya.. Na kumnunulia shangingi japani.. Na mkuu wa wilaya akaenda kula nyama choma na familia yake kwenye ukumbi ule ule .. Si kitu kile kile? Sasa hapo kuna tofauti gani?
Huyu waziri ni mweupeeeeeeeee!!!!
Kuna mambo ambayo viongozi wetu wanafanya na kusababisha watu wajiulize mara mbili, unapobana matumizi kwa kuzuia matumizi ya pesa ndani ya nchi yako na wananchi wako kutolipwa vizuri, unaongeza umasikini badala ya kuupunguza.
 
Mpango kama vipi atembelee boda boda basi
MPANGO HAJAJUA KUWA WAJAPANI WALISHABANA MATUMIZI KITAMBO NDIO MAANA WAKAJA HUKU KWETU TENA PORINI MOROGORO KUFANYA VIKAO VYA BEI NAFUU...WANGEKUWA HAWAJABANA MATUMIZI WANGEWAITA WAJUMBE WAENDE TOKYO NA KIKAO KIFANYIKE 5STAR HOTEL NA POSHO NA NAULI ZA WATANZANIA WALIOALIKWA WALIPWE KWA MIDOLAR....ILA WAMETUHURUMIA NA KUTUSAIDIA KUBANA MATUMIZI.

SASA HUYU MPANGO ANATAKA WAJAPANI WATESEKE KWENYE VIOFISI VYA SERIKALI HAVINA HATA AC JOTO KAMA MUKO KUZIMU...AKWENDREEEEEEEE KULE AKABANE MATUMIZI YA MAFUTA NA MASHANGINGI YA SERIKALI. ASISAHAU PIA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NA MBIO ZA MWENGE NAYO NI MATUMIZI MABOVU ANAONA PESA YA WAJAPANI.

KWELI ROHO MBAYA HAINA MWENYEWE...MTU HUZALIWI NAYO UNAJIFUNZA TUU UKUBWANI.
 
Back
Top Bottom