Dr Mhede aja kijapani zaidi, hamna tena mambo ya Yono, minada ya TRA sasa kielectronic

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,080
10,041
TRA yasitisha minada ya hadhara, sasa kufanyika kielektroniki

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede amesitisha kuuza bidhaa balimbali kwenye minada ya hadhara ambayo awali ilikua ikitumia madalali.

Amesema minada hiyo kwa sasa itakuwa kwa njia ya mtandao na kulipiwa kwa njia hiyo licha ya kwamba mteja ataruhusiwa kuona bidhaa alizochagua kwa njia ya mtandao.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali wa minada ya forodha kwa bidhaa mbalimbali ulikuwa ukifanywa kupitia dalali aliyepewa kandarasi na TRA kufanya minada hiyo.

“Wakati tulikuwa tukitumia madalali kumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwamo kufanyika mara moja kwa wiki na kusababisha bidhaa hizo kutouzwa kwa wakati hivyo serikali kutokomboa kodi kwa wakati pia.

“Pia washiriki wa mnada wamekuwa ni wale wale kwa kujirudia rudia na hata hivyo wengi wao kutokuwa wanunuzi na mara kadhaa kuingilia minada na kuharibu na kufanya wanunuzi wenye nia kushindwa kununua bidhaa hizo,” amesema.

Aidha, amesema kumekuwa na vitendo vya kuzuia wengine na kupanga bei ambayo ni kinyume na busara ya msingi ya uchumi kunakofanywa na baadhi ya watu wenye hila kwa mtandao waliouweka.

Pamoja na mambo mengine, amesema pia tuhuma mbalimbali na vitendo vya rushwa vikihusisha hata baadhi ya Maofisa wa TRA.

Chanzo: Mtanzania
 
"Well done"
Hata kwenye kulipia magari bandarini wange install appl maalumu baada ya ku feed full details ina calculate inaleta kiasi cha malipo,hivyo hivyo kwa kampuni za bima.
my expriences;-
Japon bima yako inapoisha tu kule makao yao makuu kuna blinc red,so wanajua gari yako iko wapi mara moja na kuifuata.ha ha ha its very funny games,mambo haya yakija hapa kwetu sijui itakuwaje?.
 
"Well done"
Hata kwenye kulipia magari bandarini wange install appl maalumu baada ya ku feed full details ina calculate inaleta kiasi cha malipo,hivyo hivyo kwa kampuni za bima.
my expriences;-
Japon bima yako inapoisha tu kule makao yao makuu kuna blinc red,so wanajua gari yako iko wapi mara moja na kuifuata.ha ha ha its very funny games,mambo haya yakija hapa kwetu sijui itakuwaje?.
Taratibu tunasogea itakuwa utaratibu mzuri sana. Tuepuke hizi kazi za karatasi
 
Modern IT technologies ndio inayoleta mapinduzi katika ukusanyaji wa mapato ULAYA NA MAREKANI.
HIVI VIJIKAMPUNI VYOTE NI VYA WAPIGA DILI. (havina nia ya kweli ya kuisaidia serekali) / WANAILALIA SEREKALI,HALAFU WAO WANAUZA KWA KWA BEI KUBWA ILI WAPATE KWELI KWELI ABOVE.
 
Back
Top Bottom